Ameoa Kisha Ameacha Kwa Vile Mke Hana Maadili – Anataka Kumrudia Mkewe Lakini Mama Hayuko Radhi
SWALI:
Assalam aleykum Werahmatolah Wabarakatuh.
Shukrani nyingi
Ningependa kuuliza
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mama kutokuwa radhi kwako kumuoa au kumrudia mkeo. Hakika mara nyingi vijana huchukulia mambo mengine kuwa sahali na hivyo kukiuka maadili ya Kiislamu katika suala
Wazazi na hasa mama wana haki kubwa kwa watoto wao. Hii ni kwa jinsi pindi kijana mmoja alipokwenda kumshitakia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa babake amechukua baadhi ya
“Na Mola wako Mlezi Ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa heshima. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyonilea utotoni” (17: 23 – 24).
Unatakiwa uwasikilize katika wema na kutowasikiliza ni thibitisho kuwa uko hasarani hapa duniani na kesho Akhera. Kufanya hivyo, utakuwa umekiuka maagizo ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye amekuagiza na kukuamuru uchague binti katika ndoa yako mwenye Dini na maadili. Ukitazama kwa mujibu wa swali lako ni kuwa wewe unamtaka binti au kumrudia mkeo ambaye hana maadili. Ukosefu wa maadili ni kumaanisha kuwa na Dini hatokuwa nayo. Mama yako anatakutakia wema kwa kukuepusha katika janga
Nasaha yetu ni kuwa mama anakuelekeza kwema nawe unatakiwa ufuate anayokwambia na uyashike kwa magego yako. Tunakutakia kila la kheri na Allaah Mtukufu Akuwezeshe pamoja na kukupatia hima ya kuweza kumfuata mamako bila tatizo lolote.
Na Allaah Anajua zaidi