Swalaah Ya Ijumaa Inajuzu Katika Kumbi Zinazofanyiwa Kamari, Disko Na Pombe?
SWALI:
Assalaam alaikum, ningependa kujua kama hapa ninapoishi u.k milton keynes) kuna miskiti zaidi ya mmoja lakini miskini mengine ya mambo ya bid'a, na mengine wakimaliza kuswali watu wengine watachelewa makazini, au wanatoa khutba kwa lugha yao ya kihindi hatuelewi sasa tumekua na maholi kama matatu ambayo yaswaliwa ijumaa, kuna holi la wasirlanka khutba yatolewa kwa kisirlanka, kuna maholi mawili yatolewa khutba kwa kizungu, nama holi haya yanatumika kwa sherehe nyenginezo kama (bingo, bada za Wakristo, mbali napati ambazo kunanywiwa pombe na disko ndani yake) je yafaa kuswali ijumaa katika maholi haya au hayafai? Assalam alaikum
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu Ijumaa katika majumba ya madisko na mfano wake.
Kwa hakika
Haijapatikana katika historia kuanzia wakati wa Mtume Muhammad (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hadi katika miongo ya karibu Waislamu kuswali Swalah hiyo katika kumbi za disko na kadhalika. Na sisi inatakiwa tuihifadhi hali hiyo mpaka siku ya Qiyaamah. Kwa hivyo, Swalah ya Ijumaa inatakiwa iswaliwe Misikitini peke yake. Ni bora zaidi kuiswali katika Msikiti ambao huelewi khutbah kuliko kuiswali katika kumbi zenye kufanya maasiya, na hivyo kuwasaidia katika kuzidisha maasiya hayo. Na Allaah Aliyetukuka Ametuambia:
“Na saidianeni katika wema na ucha Mungu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Allaah. Hakika Allaah ni Mkali wa kuadhibu” (al-Maaidah [5]: 2).
Kwa kuwa Misikiti tayari ipo ni bora kuswali katika Misikiti hiyo na haitofaa kwenu kwenda katika maholi hayo uliyoyataja. Ama kule kutolewa khutbah kwa lugha ambayo nyinyi hamuelewi
Bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaid:
Na Allaah Anajua zaidi