Mwanamke Kuwa Imaam Kwa Wenzake Katika Swalaah

SWALI:

 

Assalam alaikum warahmatullahi wabakatuh, baada ya salam hiyo ya mweyezi mungu nilikuwa na swali, je mwanamke anaweza kuwa imam upande wa wanawake,

 

 


JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mwanamke kuwa Imaam kwa wanawake wenziwe. Ndio mwanamke anaweza kuwa Imaam kwa wanawake wenziwe lakini hawatasimama kama wanavyosimama wanaume. Wanawake walio maamuma husimama takriban sawa na Imaam upande wa kulia na kushoto kwake, tofauti na wanavyotakiwa wanaume wasimame nyuma ya Imaam wao.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share