Kuweka Du’aa, Qur-aan Au Adhaan Kuwa Mlio Wa Simu

 

Kuweka Du’aa, Qur-aan Au Adhaan Kuwa Mlio Wa Simu

 

  Alhidaay.com

 

 

SWALI LA KWANZA:

 

asalam alaikum narudia kutuma ili swali mwanzo sikujibiwa.swali ni kwamba inafaa kutumia quraan kama mlio wa simu? kuweka liowa mpigaji au miito ya simu kutumia sura yeyote au adhana & dua najua unaweza kutumia qaswida. nitashukuru sana kila la kheri katika kuendeleza mtandao wa alhidaaya.

 

SWALI LA PILI:

 

Assalam alaikum, swali langu ni kwamba mtu anaposeti mlio wa simu msomaji wa quram ni sahihi maana sio wote tunaepokea na na kupiga ni waisilam, pia simu inapoita kwa aya ya quran jina la Allah hata alijaisha ikapokelewa sijui inafaa au haifai au tanafanya tukitu hatuna hakika nacho in shaa Allah nitakua nimeeleweka,

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

   

Hakika ni kuwa Muislamu hafai kuweka mlio wa simu kuwa ni Aayah au Suwrah ya Qur-aan kwani Qur-aan haikuteremshwa kwa lengo hilo. Allaah ('Azza wa Jalla)  Anasema:

 

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ  

Mwezi wa Ramadhwaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na pambanuo (la haki na batili).  [Al-Baqarah: 184]

 

Na kisha Qur-aan haifai kusomwa katika sehemu fulani mojawapo ikiwa ni chooni. Mfano umeingia chooni na ikaanza kulia utafanya nini? Itabidi uizime lakini hasara tayari itakuwa imepatikana. Pia ikianza kuita au kulia nawe uipokee, hata kabla ya kumalizika Aayah itakuwa ni utovu wa adabu.

 

Ama sauti ya Qur-aan kusikika na asiye Muislamu haina shida kabisa bali ndio lengo lake, Kitabu hicho kitukufu. Ikiwa asiye Muislamu anataka kujua kuhusu Uislamu licha ya kusikiliza hata kuisoma kwa kupatiwa tafsiri kwa lugha anayoielewa ndio bora na lengo.

 

Kwa hiyo, jambo hilo halina shida kabisa katika shari’ah.

 

Bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:

 

Kuweka Milio Ya Miziki Kwenye Simu Za Mkononi Au Qur-aan Inayosomwa Au Adhaana

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share