Mtoto Wao Amelawiti Mtoto Mwengine, Wamfanye Nini?
SWALI:
Assalam aleikum
Nalileta suali langu kwenu nikitarajia ufafanuzi.
Nina kijana alipofika umri wa 15yrs nikamuona hana raghba ya masomo ya kiengereza. Nikaamua bila kumpotezea wakati afadhali nimpeleke hifdhil quran! La kunihuzunisha ni kua baada ya mwaka na nusu -niliitwa nilipofika nikapewa khabari yakuhuzunisha!!! Niliambiwa kua mtoto wako ameshikwa na kitendo cha qaumulut. Tukajaribu kujadiliana mbele
Mwanipa fikra gani ama ushauri gani kwa huyu mtoto??? Kwani nilimdhihirishia kua lau kungekua na hukmu ya kiislaam wallahi ninge mhukumu!! Mwaeza nipa fikra ama ushauri!??? Shukran!
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu liwati.
Tufahamu kuwa liwati ni katika madhambi makubwa yaliyokatazwa na Uislamu kwa kauli za wazi kabisa. Ni nasaha kwa kila mmoja wetu anapotaka kumpeleka mtoto kwenye Madrasah basi achague Madrassah za Sunnah za watu wenye kuaminika maadili yao na elimu yao, kwani Madrasah nyingine hawaoni umuhimu mkubwa wa uasherati aina hiyo kwa kuweka waalimu wasio na maadili na wenye tabia chafu ambao wamevaa vazi la watu wa dini na hali ni waharibifu wa maadili. Na Madrasah kama hizo waalimu wenyewe ndio wanaowafanya watoto kitendo cha liwati.
Kwa hiyo ni muhimu kuwa na tahadhari kubwa
Kwa kila njia, hata
1. Kumtoa Madrasah hiyo na kumtafutia nyingine yenye misimamo ya Sunnah baada ya kuichunguza na kuiona kuwa iko sawa. Ni muhimu kumbadilishia mazingira ya masomo na sehemu. Na ukimpeleka Madrasah nyingine isiwe ni kuhifadhi tu bali kuwe na masomo mengine kama , ‘Aqiydah na Tawhiyd, Qur-aan na tafsiri yake, Hadiyth, Fiqh, Siyrah, Lugha na masomo mengineyo.
2. Ni muhimu mtoto azungumziwe kuhusu mas-ala ya Imani, kutii amri za Allaah Aliyetukuka na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na katika
3. Ni muhimu huyo mtoto apatiwe nasiha za nguvu kuhusu suala
Kisha suala la kuwa alionekana akifanya kitendo hicho ni upande mmoja. Je, mtoto mwenyewe amekiri kuwa amefanya kweli? Na waliomuona ni wangapi katika hao walioshuhudia? Suala la zinaa na liwati ni suala gumu, na shari’ah haikubali mpaka kuwa na mashahidi wanne walioona kihakika kitendo hicho kikifanyika, la sivyo katika shari’ah yule aliyekuja ndio mwenye kuadhibiwa. Na suala
Na kukiwa na shari’ah ya Kiislamu, si wewe utakayemhukumu bali ni Khalifa au Qadhi wa mji wako au sehemu mnayoishi. Na mtu hawezi kuhukumiwa mpaka kuwe na ushahidi wa kutosha kuhusu tuhma hiyo.
Kwa hivi sasa fanyeni juhudi za kumpatia nasiha, na InshaAllaah, atakuwa ni mwenye kuacha ikiwa kweli alitumbukia katika kitendo hicho.
Na Allaah Anajua zaidi