Wazinifu Waliotubu Wanaweza Kufunga Ndoa Na Waliotakasika
SWALI
(Nimeona nakala ilitumwa katika moja ya sites za Kiswahili muandikaji katika kujibu nakala za mwengine alitoa hoja kuwa,
Mtume SAW alipokuja kuwaleta watu katika haki na kuacha machafu, hajawaamrisha wale walioowana kabla ya Uislam waowane kwa mara ya pili, na pia aliuliza kama kuna hadithi au Aya ambayo jambo kama hili lilitokezea wakati wa Mtume SAW nae Mtume akawaambia watu wavunje ndoa yao kwasababu walizini kabla ya hapo, na hoja nyingi alizitoa muandikaji kwa kusema jee kwa wakati wa leo watu
JIBU:
Kwa mafunzo sahihi kwa mujibu wa itikadi ya Salafus Swaalih (wema waliopita) ambayo ndio Itikadi ya Ahlus Sunnah wal Jama'ah, wanamzingatia mwenye kufanya madhambi makubwa
Kwa hiyo Muislamu aliyetubu kikweli kutokana na kitendo cha zinaa, akafuata shuruti za Tawbah ikawa Tawbatun-Nasuuha na akazidisha na kuendelea kufanya vitendo vyema badili yake, basi alama ya zinaa huondoka, yaani haitwi tena mzinifu, bali husamehewa kama yule aliyefanya matendo ya shirki, kuua ambayo ni maasi yenye madhambi makubwa kama ilivyo zinaa. Mwenyeezi Mungu Anasema:
}}وَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّهِ إِلَهًا آخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ وَمَن يَفْعَلْ ذَلِكَ يَلْقَ أَثَامًا{{
}}يُضَاعَفْ لَهُ الْعَذَابُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَيَخْلُدْ فِيهِ مُهَانًا{{
}}إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُوْلَئِكَ يُبَدِّلُ اللَّهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا{{
{{ Wale wasio mwomba mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi aliyo iharimisha Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwa haki, wala hawazini - na atakaye fanya hayo atapata madhara}}
{{azidishiwa adhabu Siku ya Kiyama, na atadumu humo kwa kufedheheka}}
{{Isipokuwa atakaye tubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu
Al-Furqaan: 68-70
Hadithi hii hapa chini pia inathibitisha kusamehewa huko kwa vitendo
((عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ نَاسًا مِنْ أَهْلِ الشِّرْكِ كَانُوا قَدْ قَتَلُوا وَأَكْثَرُوا وَزَنَوْا وَأَكْثَرُوا ، فَأَتَوْا مُحَمَّدًا صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ، فَقَالُوا : إِنَّ الَّذِي تَقُولُ وَتَدْعُو إِلَيْهِ لَحَسَنٌ ، لَوْ تُخْبِرُنَا أَنَّ لِمَا عَمِلْنَا كَفَّارَةً ، فَنَزَلت:
}}والذينَ لا يَدْعُونَ مَعَ اللَّهِ إِلَهًا آخَرَ وَلا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلا بِالْحَقِّ وَلا يَزْنُونَ {{ وَنَزَلَتْ : }} قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَى أَنْفُسِهِمْ لا تَقْنَطُوا مِنْ رَحْمَةِ اللَّهِ{{ ))
روى البخاري (4436) ومسلم (174)
((Imetoka kwa Ibn 'Abbaas رضي الله عنهما ambaye kasema; baadhi ya watu Mushrikiin ambao waliua
الله عليه وآله وسلم na kumwambia; Unayotuitia (katika Uislamu) ni mazuri, lakini tujulishe tu kama kuna kafara ya yale maovu tuliyoyafanya; hapo zikateremshwa aya hizi:
{{Na wale wasio mwomba mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi aliyo iharimisha Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwa haki, wala hawazini} Al-Furqaan: 68
Na ikateremka:
{{Sema: Enyi waja wangu walio jidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu}})) Az-Zumar: 53 (Al-Bukhari na Muslim)
Kisha baada ya kutubu anatakiwa Muislamu ajistiri kwa kuficha siri yake ya mambo aliyofanya maovu kabla, na sio kujifehedhesha kwa kuyatangaza maovu hayo na kujisifu nayo,
(( اجتنبوا هذه القاذورة التي نهى الله عز وجل عنها ، فمن ألم فليستتر بستر الله عزوجل)) رواه البيهقي وصححه الألباني في السلسلة الصحيحة 663
((Jiepusheni na uchafu huu alioukataa Allaah عزوجل, na atakaye tenda dhambi ya aina hiyo, basi ajisitiri kwa stara ya Allaah ((عزوجل [Al-Bayhaaqiy na Amesahihisha Saykh Al-Albaaniy katika Silsilatus Swahiyhah: 663.]
Kwa hivyo suali lako kuhusu Aaya katika Suratun-Nuur
}}الزَّانِي لَا يَنكِحُ إلَّا زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لَا يَنكِحُهَا إِلَّا زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ وَحُرِّمَ ذَلِكَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ{{
{{Mwanamume mzinifu hamwoi ila mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina. Na mwanamke mzinifu haolewi ila na mwanamume mzinifu au mshirikina. Na hayo yameharimishwa kwa Waumini.}} An Nuur:3
inakusudiwa wale ambao bado wanaendelea katika katika kitendo hicho cha zinaa. Ama waliotubu kikweli wanaweza kuoa na kuolewa na waliotakasika.
Wa Allaahu A'alam