Mwanamme Amefanya Liwati Akatubu, Mwanamke Anafanya Mapenzi Lakini Hajaingiliwa, Je, Wanaweza Kuoana?
SWALI:
Asalaam alaykum.
Shukrani kwa kutupatia nafasi adhym ya kujifunza. nauliza kijana wakiume amewahi kufanya liwaat ya kwa mwanaume mwenzake na mwanamke kwa wakati tofauti,akalia sana na kuazimia kutofanya tena, hukonyuma hakuwahi kuzini ila kwa hao wawili. akabahatika kupata mchumba.kwa sharti waish kiislam, kwani mwanamke alikuwa ana mazingira yote ya zinaa anatoka mpaka sannane usiku kwenye starehe kwenye mahoteli na wanaume mbali mbali na wanafanya romance,ila hakuwahi kuingiliwa,nae shart lake kuish kiislam, mahari tayari,ila mwanamke anasema yeye yuko tohara hajawahi kuzini na kamna mwanaume amewahi kuzini, hawafanani akamuo mzinifu mwezake,yeye ni tahara mwanaume amejibu k hakuwahi kuzini ila aliwahi kufikia asilmia tisni ya kuzini. Lakini kweli kila akiingiza tu uume anamaliza kabla ya kufanya, sasa jee hawa watu hawawezi kuona kwasababu mwanaume kasema uongo?
SWALI KALIRUDIA:
Asalaam, alaykum,
ALLAH subnhaana wataala akulipeni kwa kutuelimisha, swali ukawahi kufanya liwaat, halafu ukAjuta na kuazimia kutofanya tena, jee hamfanani kwa kuoana na mwanamke anayefanya mapenzi yote ila haruhusu kuingiliwa. Na pia akawa mwanamke anakwenda kwenye kumbi za starehe na wanaume mbali mbali.haifai kumokoa kwa kumoa na kukubaliana kuishi kwa kufata dini ya kiislam katika maisha yenu,
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mwanamme aliyefanya liwati na mwanamke anayekwenda kwenye nyumba za starehe.
Swali lako linaonyesha kuwa hao watu wameshaoana na unataka kujua
Hata hivyo, tukijibu swali lako, ni kuwa wote wawili hao wana madhambi japokuwa dhambi la mwanamme ni kubwa zaidi kuliko la mwanamke. Hakika hakuna aliye twahara kati ya hao wawili kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Ameonya:
“Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya” (al-Israa’ 17: 32).
Na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatumbia:
“Zinaa ya jicho ni kutazama, ya mkono ni kushika, ya masikio ni kusikiliza na ya miguu ni kutembea katika maasiya”.
Hivyo, inatakiwa kila mmoja kati
1. Kujiondoa katika maasiya.
2. Kujuta kwa kufanya dhambi
3. Kuazimia kutorudia tena kosa
Mwenye kutubia kisawa sawa, Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Humsamehe na kwa hiyo huwa hana tena dhambi. Na watu hao Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anawazungumzia:
“Isipokuwa wale waliotubu baada ya hayo na wakatengenea; kwani bila ya shaka Allaah ni Msamehevu, Mwenye kurehemu” (an-Nuur 24: 5).
Na Anasema (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa uwazi zaidi:
“Isipokuwa atakayetubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Allaah Atayabadilisha maovu
Kwa kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Husamehe madhambi yote (az-Zumar 39: 53), mtu anayetubia huwa hana tena dhambi kwa hivyo anaweza kuoa au kuolewa na mwanamke twahara au mwanamme wa aina hiyo.
Kitu muhimu ni kujaribu kumchunguza
Kwa muhtasari ni kuwa, ikiwa kweli wametubia wanaweza kuoana bila ya matatizo yoyote yale.
Bonyeza viungo vifutavyo upate manufaa zaidi:
Mwenye Kufanya Maasi Ya Liwati Anaweza Kurudi Kwa Allah Kutubia?
Na Allaah Anajua zaidi