Rafiki Yake Amekiri Kuwa Ametenda Maasi Ya Zinaa Sasa Hamuamini Tena, Je Aachane Naye Au Aendelee Naye
SWALI:
Asalam ‘alaykum warahmatullahi wabarkat.
Nina rafiki yangu tuseme
Wabillahi tawfiiq
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mchumbako aliyeteleza na kuingia katika dhambi kubwa la zinaa. Tufahamu kuwa kila mwanadamu ni mkosa na bora wa mwenye kukosa ni mwenye kutubia na kurudi nyuma na akaweka ahadi ya kutorudia tena.
Na kwa kuwa umesema kuwa una muda kabla ya harusi huenda akashawishika tena kwani kitendo cha ndoa kina utamu wake na ushawishi kutoka kwa aliyefanya naye kitendo huenda ukazidi mpaka awe na Imani kubwa ya kutorudia. Bila shaka, una haki ya kukasirika lakini mliingia katika mtengo kuanzia mlipofanya urafiki baina yako na wewe na mkaanza kuzungumza kwani jambo
Hata hivyo, katika suala lako
1. Kumsamehe, na kuolewa na mwengine awe ni halali yako kuzungumza naye. Ukichagua kipengele hiki itabidi usahau kabisa yaliyopita na ugange yajao. Ukiwa hutaweza basi, kipengele cha pili ni,
2. Umsahau kabisa na umtoe katika mawazo yako. Tatizo la kuolewa naye ukiwa na mawazo ya yaliyotendeka kila wakati yatakuwa yanajitokeza baada ndoa na kitu kidogo huenda kikakufanya umkumbushe jambo
Ushauri wa mwisho ambao tunaweza kukupa ni uswali Swalah ya Istikhaarah kabla ya kuamua lolote lile. Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Akufanikishe uchague lililo na kheri nawe katika maisha yako na Akhera pia.
Na Allaah Anajua zaidi.