Kashika Mimba Ya Zinaa, Mumewe hana uzazi, Amjulishe Mumewe Au Atoe Mimba?
SWALI
Assalam alaikum, Namshukuru Mungu Mola wa viumbe vyote. Ama baada ya haya nina tatizo naomba nisaidiwe mimi ni mwanamke ambaye nimeolewa na huu ni mwaka wa 3 lakini sikujaaliwa kupata mtoto na kwa upande wangu sikuwa na tatizo ila mume wangu ndio mwenye tatizo la kizazi lakini anatumia dawa za sunna. Kwa bahati mbaya na kwa hamu niliyokuwa nayo ya mtoto nikafanya kosa nikatembea nje siku 1 na wala sikukusudia kuwa nitakuwa na mimba Ibilisi tuu kanihadaa, baada ya 2 weeks nikajihisi nina mimba na hivi ni miezi 2.
Jamani sasa mtoto wa mume au wa nje nifanyeje, nilipomueleza mume alifurahi
JIBU
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mimba ya zinaa. Mara nyingi sisi hufanya makosa yaliyo makubwa mbele ya Allaah Aliyetukuka nasi tukawa ni wenye kusema bahati mbaya au Iblisi ndiye aliyekushawishi. Kudhania hivyo halitusaidii sisi na lolote wala chochote bali linatupatia sisi muhula na nafasi ya kufanya mengine na kisha kutoa hoja hizo hizo.
Haiwezekani kuwa ukawa umefanya tendo kama la zinaa kisha useme sikukusudia kwani kitendo hicho kinajumlisha mambo mengi
Kitendo ulichokifanya kimekufikisha katika njia panda na
Ushauri wetu ni kuwa sema ukweli kwa mumeo na huenda ikawa na natija nzuri zaidi. Baada ya hapo unafaa ufanye toba ya kweli kweli kwa Mola wako kwa kutekeleza masharti yafuatayo:
1. Kuacha maasiya hayo.
2. Kujuta kwa kufanya uovu huo.
3. Kuazimia kuwa hutarudia tena kosa
Twakutakia kila mafanikio hapa duniani na Akhera.
Na Allaah Anajua zaidi