Nilizini Kwa Sababu Wazazi Walikataa Tuoane Sasa Tumeoana Najuta Kuzini
SW
Bismillah rahman rahim, naomba mnisaidie kwa kunijibu swali hili linalonipa dhiki moyoni mwangu; mie katika kukua kwangu nilipendana na mchumba wangu ambae wazee wake walikataa asinioe. Na sisi hatukuweza kuachana kwa sababu tulipendana
je hii ndoa na mtoto niliyemzaa na watoto nilozaa baadae na kila tendo la ndoa nnalofanya na mume wangu tangu aliponioa mpaka hii leo ni halali? Nifanye nini au niombe msamaha vipi ili Allaah (swt) anihalalishie yote hayo pamoja na wanangu?
Najuta kila siku naomba msamaha kwenye msala mpaka nalia na inshAllaah mwaka huu nakwenda kuhiji Allaah (swt) akitupa khatua, nitajitahid kuomba msamaha
(YAARAB TUSAMEHE MADHAMBI YETU YOTE UTUHAL
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Mtume, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.)
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu ndoa baada ya zinaa. Tufahamu kuwa Allaah Aliyetukuka Ametukataza sio tu kuzini bali hata kukaribia zinaa (17: 32). Na ajabu
Yaonyesha kuwa huyo mchumba wako amekosa kuifahamu Dini yake ya Kiislamu na hivyo kuona njia ya pekee ya kukupata wewe ni kukutia mimba. Tufahamu kuwa mume katika kuoa hahitaji kupata idhini ya wazazi wake tofauti na mwanamke. Na ni ajabu kuwa hata baada ya kufanya dhambi mkaendelea kukaa pamoja na kuzidisha kufanya madhambi hayo ya uzinzi. Ajabu ni kuwa wazee wako wamekubali ambao ndio sharti kwa kusihi ndoa yenu lakini hamkuweza kuitumia hiyo kwa maslahi yenu.
Naona dada yetu umekosea kabisa kwa kudai kuwa wazazi wa mume wako ndio waliowafanya kuzini kuondoa kosa kutoka kwako. Nyinyi wote wawili tayari mmebaleghe na hivyo madhambi mnaandikiwa nyinyi na sio wazazi wenu. Kwa hiyo, msitafute visingizio bali mnatakiwa murudi kwa Mola wenu Mlezi. Lau mgetaka nasaha kuanzia wazazi wake walipokataa hamgeingia katika dhambi
Hakika katika sheria ya Kiislamu mlikuwa hamfai kuoana ukiwa na mimba mpaka uzae. Lakini
Ama yale ambayo unaweza kupata msamaha kutoka kwa Allaah Aliyetukuka ni ile zinaa mliyofanya kabla ya kuoana. Toba inakubaliwa na Allaah Aliyetukuka baada ya kufuata masharti yafuatayo:
1. Kujuta kwa uliyofanya.
2. Kuweka azma ya kutorudia kosa
3. Kutorudia tena kosa na dhambi
Na inaonekana kulingana na swali lako masharti haya umeyatimiza lakini hata hivyo fanya bidii zaidi kufanya mambo yaliyo mema na kuleta istighfaar kwa wingi na kuwasaidia wengine.
Unaweza kusoma zaidi kuhusu masuala hayo kwenye viungo vifuatavyo:
Watoto Baada Ya Ndoa Ya Uzinifu
Wazinifu Waliotubu Wanaweza Kufunga Ndoa Na Waliotakasika
Waliofanya Zinaa Wanaweza Kuoana?
Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Akusamehe na Akupe hima ya kufanya amali njema kwa wingi.
Na Allaah Anajua zaidi