Anataka Kukutana Naye Kwa Kutenda Maasi Naye Kabla Ya Kumuoa Apate Kujua Kama Anajua Mapenzi

SWALI:

 

Ikiwa mwanamke ampe mpata mwanaume ambe anania ya kumuoa lakini mwanaume huyo anapendekeza waanze kukutana kimwili kwa kisingizio anataka ajue kama mwanamke anayajua mapenzi je huyu mwanaume ni mwema??

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mwanamme kutaka kukuoa baada ya kujua kama unajua mapenzi.

Kukutana kimwili baina ya mwanamme na mwanamke kabla ya ndoa ni zinaa. Na tufahamu kuwa zinaa ina adhabu hapa duniani kabla ya kesho Akhera mbali na kuwa tumeamriwa tusikaribie zinaa kwani ni uchafu na ni njia mbaya kabisa (al-Israa’ [17]: 32).

 

Mwanamme wa Kiislamu aliye mwema ni yule anayekaa mbali na madhambi yote makubwa na madogo ikiwemo zinaa. Kwa ajili hiyo, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawausia wazazi:

Akikujieni yule ambaye mnaridhia Dini na maadili basi mwozesheni” (at-Tirmidhiy).

 

Mtu ambaye anataka kuzini na mwanamke kabla ya kumuoa hana Dini wala maadili. Kwa hiyo, inatakiwa umuepuke mwanamme huyo na uwe mbali sana naye kwani si mwema hata chembe. Hakika ni kuwa anataka kukuchezea baada ya hapo akutupe jaani kama taka.

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate manufaa zaidi:

 

Mawasiliano Na Mchumba Baada Kuposa Na Kabla Ya Ndoa

 

Anaweza Kuzungumza Na Kuonana Na Aliyemposa?

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share