Mwanaume Kamuingilia Kwa Nguvu Hadi Ametokwa Damu, Je, Amevunja Bikra?
SWALI:
Assalam alaikoum!
Mimi nina rafiki yangu ambaye jina
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu uchumba ya wapendanao. Mara nyingi nyingi matatizo yanatufikia kwa sababu ya kuyachuma kwa mikono yetu miwili
“Na misiba inayokusibuni ni kwa sababu ya vitendo vya mikono yenu. Naye Anasamehe mengi” (42: 30).
Matatizo haya na majuto baadaye yanatufikia kwa sababu ya kuacha mafunzo ya Dini na maadili yake. Uislamu umetukataza kabisa kuwa na urafiki baina ya mvulana na msichana ambao wanaweza kuoana. Lakini kwa kutosikia kwetu hayo tunafikiwa na majanga na tunajuta lakini majuto hayo hayafalii chochote. Huwa wakati huo maji yashamwagika na inakuwa ni vigumu kuyazoa na hayawezi tena kutumiwa. Mara nyingi wasichana kwa udhaifu wao mkubwa huwa wanadanganywa na wavulana kuwa hawatofanya chochote na akadanganywa kuwa ataolewa naye n.k.. lakini baada ya muda inafikia kupigwa teke na kuachwa baada ya kubikiriwa.
Huwa tunapambiwa na Shaytwaan kuwa sisi hatutafanya lolote. Je, nyinyi ni Malaika? Jawabu linakuja ni la. Na ndio Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasisitizia
Kutokwa na damu si lazima awe amebikiriwa, kwani hukutuelezea kiasi cha damu ambayo huyo msichana ametoka. Huenda ikawa ni damu kutoka sehemu nyingine kwani damu ya kubikiriwa inakuwa kidogo
Hiyo ndiyo nasaha ambayo twaweza kumpatia ili aweze kujijua hali yake. Hata hivyo anatakiwa ajichunge
Na Allaah Anajua zaidi