Mke Akitaka Talaka, Alipwe Nini?
SWALI:
A, alaikum jina issa mussa swali langu ni kama mke wangu akitaka talaka ana haki ya kupata mahari yake kani mm nilioa mwaka 2008 mwezi wa 8 na tunaishi mbali kidogo sijamuona mke wangu toka nimuoe kwa sababu ya kisheria mm siruhusiwi kusafiri na mke wangu ana haki ya kusafiri na anakazania kumuona mama yake ambaye hayuko karibu naye anasema hajamuona mama yake naomba mnisaindie kwani mke wangu ni msilamu lakini hajue ndini ya Kiislamu.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mke kutaka talaka. Hakika hili na matatizo mengine ya kinyumba ni matatizo sugu
Kwa ajili hiyo, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) alituuisia
Ikiwa mke anataka talaka inategemea anataka talaka kwa sababu gani. Ikiwa anataka kujivua kutokana nawe, bila ya wewe kuwa na makosa itabidi yeye akulipe mahari uliyompatia wakati wa ndoa yenu. Hata hivyo, akiomba talaka kupitia kwa Qaadhi kwa sababu ya makosa uliyonayo wewe basi Qaadhi ataweza kuwaachisha baada ya kusikiliza pande zote mbili. Na katika hali hiyo, hutarudishiwa mahari uliyotoa wakati wa ndoa.
Na jambo la ajabu
Ulipoona kuwa wewe huruhusiwi kabisa kusafiri ilikuwa uliweke wazi
Kukusaidia katika tatizo
Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:
Kujivua Mwanamke Katika Ndoa (Khul'u) Na Hukumu Zake
Mut’ah (Kiliwazo, Kustarehea, Kitoka Nyumba, Masurufu) Ya Kumpa Mke Anayeachwa
Je, Inafaa Mume Na Mke Kuishi Mbali Kwa Muda Mrefu?
Na Allaah Anajua zaidi