Mfano Wa Nabii Ismaa’iyl (‘Alayhis Salaam) Unafaa Kuigwa Katika Kutaliki Mke?
SWALI:
Assalam alaykhum ndugu zangu wa alhidaaya, Ninahitaji ufafanuzi juu ya suala hili; Je? ni sunnah kwetu tuwe tunawatariki wake zetu tunapokuwa na shida, dhiki, au karaka zinapotufika kwa muda mrefu
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani kwa swali lako kuhusu yaliyotokea baina Nabii Ibraahiym (‘Alayhis Salaam) na mwanawe Ismaa’iyl (‘Alayhis Salaam) na agizo la baba kwa mama amtaliki mkewe. Hakika hili ni swali ambazo wengi wanatatizika nalo kwa sababu ya amri ya baba pasi na kuangalia suala
Sote twaelewa kuwa Nabii Ibraahiym (‘Alayhis Salaam) alikuwa ni Mtume tena miongoni mwa wateule miongoni mwa Mitume. Alikuwa pia yeye ni mtume aliyekuwa na azma kubwa
Tukio kama hilo lilitokea wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pale ‘Umar al-Khatwtwaab (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipomuagizia mtoto wake, ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhuma) amwache mkewe. Na mtoto alipokwenda kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kumuuliza
Ama sisi tumeagiziwa tuishi na wake zetu kwa wema na inapotokea tatizo basi tutafute ufumbuzi kwani unaweza kumchukia mkeo kwa ila au kasoro moja lakini upande mwengine akawa ana kheri nyingi
Ama mzazi akikushauri au kukuamrisha wewe kumuacha mkeo kwa sababu za msingi za kishari’ah basi hakuna ubaya wala kizuizi cha kuwatii kwa
Na Allaah Anajua zaidi