Kusalimia Watu Mikitini Wakati Wa Khutbah

 

 

SWALI:

 

Asalaam aleykum waislam wenzangu wa alhidaaya. Napenda kuchukua fursa hii kwenu kutaka kufahamu niliyonayo ili nizidi kuelimika toka kwenu nyie wenzangu.

Kwanza, je waweza ingia msikitini siku ya ijumaa ikiwa imamu ameshaanza kutoa hotuba watu wapo kimya ukatoa salaam je nisawa?

 

 

 


 

 

 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 

 

Kuzungumza au kufanya mchezo kwa kuchezea vijiwe, tasbihi na mfano wake (kama mobile/ simu ya mkononi) wakati Imaam anapokhutubu ni jambo ambalo limekatazwa. Hii ni kwa kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Utakapomwambia mwenzako siku ya Ijumaa nyamaza na Imaam anakhutubu basi umefanya upuuzi” (Ahmad na Muslim).

 

Kwa ajili hiyo haifai kutoa salaam kwani kwa kufanya hivyo utawafanya watu washughulike na mengine badala ya khutbah.

 

Ikiwa kumwambia mwenzako nyamaza haifai, hivyo mazungumzo mengine yoyote hata salaam haifai wakati huo.

 

Jambo ambalo mtu anafaa kufanya ikiwa amefika Msikitini kwa kuchelewa siku ya Ijumaa na Khatiyb tayari anakhutubu ni kuswali rakaa mbili za Tahiyyatul Masjid na azifanye nyepesi [fupi]. (Ahmad na Muslim).

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share