Maamuuma Hawataki Kujaza Nafasi Katika Safu Za Swalaah

 

 SWALI:

  

The second is.The brothers here in the western countries, they dont pay attention on the gaps while praying, and if u try move close to him, he  moves a bit away from you. Please I need explanation on these two issues as soon as possible.

 

Wabillahi tawfiyq.wassalama alaykum.

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kujaza safu katika Swalah ya jamaa. Hakika hili ni tatizo nyeti si katika nchi za Magharibi peke yake bali hata katika nchi nyingine na hasa India, Uarabuni na hata Afrika Mashariki.

 

 

 

Mara nyingi suala hilo hujitokeza kwa sababu ya ujinga wa Maamuma, au Imaam kutosisitiza umuhimu wake au kwa ajili ya ada na desturi za kijahiliya. Huenda Maamuma wakawa hawajui, hivyo mwanzo ni wajibu wa Imaam kuweza kuwafunza kwa njia iliyo nzuri, kwa hekima na utaratibu mpaka waelewe. Hii inatokana na Hadiyth ambayo Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) amesikika akisema: “Mtaendelea kutengeneza safu au Allaah Atageuza nyuso zenu (yaani atatia baina yenu uadui, chuki na tofauti za nyoyo)” (al-Bukhaariy na Muslim). Na katika riwaya ya Muslim: “Alikuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) akitengeneza na kuzinyoosha safu zetu kama kwamba alikuwa anapanga mishale katika uta wake mpaka alipoona kuwa tumefahamu umuhimu wa hilo. Kisha akatoka siku moja, akasimama mpaka akawa yuakaribia kutoa Takbiyr, pale alipomuona mtu kifua chake kimetoka mbele, hapo akasema: ‘Waja wa Allaah! Mtaendelea kutengeneza safu au Allaah Atabadilisha nyuso zenu’”.

 

 

 

Kisha Imaam mwenyewe ni lazima awe na hima ya hali ya juu katika kurekebisha tatizo hilo. Bila ya juhudi hiyo kutoka kwake basi tatizo hilo litabakia daima dawamu katika Misikiti yetu hapa duniani.

 

Na ikiwa ni ada au desturi za kitaifa au ki-ukoo basi hakuna budi kwa Imaam kuchukua fursa ya kuwaelemisha Waumini kuhusu umuhimu wa kufuata Sunnah na kuacha ada ambazo zinakwenda kinyume na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) kwa njia ya mawaidha mazuri na busara. Kwani Allaah Aliyetukuka Anasema: “Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hekima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora” (an-Nahl [16]: 125).

 

Kwa kufuata njia hizo huenda mambo yakarekebishika kuielekea sunnah inavyotakiwa.

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

 

Share