Hadiyth Kuhusu Kuteremka Nabii ‘Iysaa Na Kutokeza Mahdi Ni Sahihi?

SWALI:

 

Assalaam Aleykum Warahmatullahi. Jee Vipi Katika Hadiysi Hii Mapokezi Yake Yapo Sawa Hapa?

Hakutakosekana kuwa na kikundi katika Ummah wangu, wakipigana juu ya haki wakiwa washindi haki Siku ya Qiyaamah… kisha 'Iysaa bin Maryam atashuka, na Amiri wao (Waislamu) atasema: 'Njoo utuswalishe katika Swalah!' Atasema: 'Hapana, nyinyi ndio ma-Amiri juu ya kila mmoja kama heshima kutoka kwa Allaah kwa Ummah huu'" (Muslim).


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola  wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu usahihi wa Hadiyth uliyoiataja

"Hakutakosekana kuwa na kikundi katika Ummah wangu, wakipigana juu ya haki wakiwa washindi haki Siku ya Qiyaamah… kisha 'Iysaa bin Maryam atashuka, na Amiri wao (Waislamu) atasema: 'Njoo utuswalishe katika Swalah!' Atasema: 'Hapana, nyinyi ndio ma-Amiri juu ya kila mmoja kama heshima kutoka kwa Allaah kwa Ummah huu'" (Muslim).

Hadiyth hiyo iko katika Swahiyh Muslim na imepokewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba Jaabir bin ‘Abdillaah (Radhiya Allaahu ‘anhuma). Hadiyth hiyo ni sahihi kabisa na haina tashwishi yoyote ile.

Na makusudio hapo juu kwenye Hadiyth kwa neno' "Amiri wao (Waislamu) atasema: "Njoo utaswalishe katika Swalah", makusudio hapo 'Amiri' ni Mahdi. Kutokana na mapokezi yaliyosimuliwa na Abu Na'iym na Al-Haarith bin Usaamah, yanasema hivi: "Amiri au Kiongozi wao Mahdi atasema..." Ibnul-Qayyim anasema, "Isnaad yake ni Nzuri."

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share