Nilikuwa Muasi Kisha Nimetubu Namuomba Allaah Mume Mwema Je Allaah Ataitikia Du’aa Yangu?

SWALI:

 

Asalam aleykum,

Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 28 nilifanya uzinzi kipindi cha nyuma lakin toka mwaka 2006 mwishon nilitubu na kujiweka mbali na zinaa mpaka sasa je, maomdi ninayoomba kwa mwenyezi mungu anipe mume awe mwaminif kama mimi nitapata?


 

JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kutubia, kujirekebisha baada ya kuasi kwako. Ni jambo linalofahamika kuwa Allaah Aliyetukuka ni Msamehevu sana kwa kiasi ambacho Anasamehe madhambi yote. Allaah Aliyetukuka Anasema: “Sema: Enyi waja Wangu walio jidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Allaah. Hakika Allaah Husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu” (az-Zumar [39]: 53). Na tena pale Alipotaja madhambi kadhaa ambayo Anamkubali mja huyo pindi anapotubia. Bali si hivyo tu ila hata hayo mabaya Huyabadilisha yakawa mema. Anasema Aliyetukuka: “Na wale wasio mwomba mungu mwengine pamoja na Allaah, wala hawaui nafsi aliyo iharimisha Allaah isipokuwa kwa haki, wala hawazini - na atakaye fanya hayo atapata madhara, Atazidishiwa adhabu Siku ya Kiyama, na atadumu humo kwa kufedheheka. Isipokuwa atakaye tubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Allaah Atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Allaah ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. Na aliye tubu na akafanya mema, basi hakika huyo ametubu kweli kweli kwa Allaah” (al-Furqaan [25]: 68 – 71).

 

Ikiwa umefanya madhambi, ukatubia ni kama kwamba huna tena madhambi tena hivyo kuwa msafi kama ule wakati ulipozaliwa na mamako. Kwa hiyo, baada ya hapo ukiomba Allaah Aliyetukuka bila shaka Atakujibu kwa lile ulilo liomba bila ya tatizo lolote lile.

 

Bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:

 

Tawbah

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

 

Share