Umri Gani Mtu Anaweza Kutoa Mawaidha?

 

Umri Gani Mtu Anaweza Kutoa Mawaidha?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Asallam Allaikum

            

Je, ni umri upi  mtu afa kutoa mawaitha ama kuna masharti yoyote  kisheria

   

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Uislamu haujaweka umri maalumu wa mtu kutoa mawaidha isipokuwa masharti yanayohitajika kuwepo. Yakiwepo masharti hayo mtu ataweza kutoa mawaidha na yakikosekana hata mtu awe mkubwa namna gani hatofaa kutoa mawaidha. Masharti ni kama yafuatayo:

 

1.     Awe Muislamu.

2.     Awe mwenye akili timamu, yaani asiwe mwendawazimu.

3.     Awe anaweza kutofautisha mambo.

4.     Awe ana elimu ya hayo anayozungumza.

 

 

Kwa minajili hiyo, Imaam ash-Shaafi‘iy alipokuwa na miaka kumi na nne (14), Imaam Maalik alimpatia fursa ya kutoa mawaidha ndani ya Msikiti wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Madiynah. Na Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhuma) naye alikuwa akiingia katika Shuuraa ya ‘Umar bin al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akiwa ni kijana hata wakongwe miongoni mwa Swahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum) walioshiriki katika Vita vya Badr wakaanza kulalamika.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share