Anapotoa Sadaka Kwa Ajili Ya Kutaka Shifaa Ya Mgonjwa, Je, Atapata Thawabu Za Sadaqah Pia?
SWALI:
Asalam Alaykum Mtume salawah alayh wasalam anasema: "Waponesheni wagonjwa wenu kwa kuwatolea sadaqa". Je
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kutoa Sadaqah kwa ajili ya kutaka Shifaa ya mgonjwa.
Kwa hakika Hadiyth ulizozitaja hapo juu zipo wazi kabisa katika suala hili. Kwa kuwa lafdhi iliyokuja katika Hadiyth ni kuwa watoleeni Sadaqah wagonjwa wenu kumaanisha unapokuwa na mgonjwa na ukatoa Sadaqah ili apate Shifaa unapata thawabu za Sadaqah na kuponeshwa kwa mgonjwa mwenyewe.
Na Allaah Anajua zaidi