Atoe Zakaah Ya Mwaka Uliopita? Je, Mtu Analazimika Kutolea Zakaah Mali Ya Bosi Wake Asiyetoa Zakaah?

SWALI:

 

Assalaam Alaykum waba'ad kwa mfano ndugu kapewa biashara na kaka ake ya milioni 3 lkn huyu kaka mwaka wa nyuma hajaitolea zaka (duka) lake je uyu ndugu anawajibika yeye kulitolea zakah ule mwaka ulopita au aanze pale alipokabiziwa yeye kwenda mbele? Na je ipo sharia yakuitolea zakah mali ya bosi wako asiyetaka kutoa zakah pasi naye bosi kujua?

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kumtolea nduguyo Zakaah.

Zakaah ya mali inatolewa kwa kupatikana masharti yaliyowekwa na Shari’ah. Masharti ni kama yafuatayo:

 

1.     Kufikiwa na Niswaab (kiwango cha chini cha kutolewa Zakaah). Kiwango hicho ni kuwa na na pesa sawa na gramu 85 za dhahabu safi.

 

 

2.     Kiwango hicho kipitiwe na mwaka bila ya kurudi chini ya hapo.

 

Ikiwa masharti hayo yatafikiwa, mwenye mali inabidi aitolee Zakaah mali hiyo yake nako ni kuisafisha hiyo mali. Mtu mwengine halazimiki kutoa Zakaah ya mali ya mtu mwengine mpaka awe atakuwa amempa shughuli hiyo. Kwa ajili hiyo, jambo ambalo unaweza kufanya ni kuzungumza na ndugu yako au bosi wako umkinaishe ya kwamba ni muhimu yeye aitolee Zakaah mali yake, ikiwa hatatoa basi madhambi ni ya ndugu yako na sio yako. Kuitoa bila ya ruhusa yake ni makosa na madhambi kwako.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share