Kurudi Kwa Nabiy ‘Iysaa (عَلَيْهِ السَّلام) Na Kumua Masiyhud-Dajjaal Ni Kweli?

 

Kurudi Kwa Nabiy ‘Iysaa (عَلَيْهِ السَّلام) Na Kumua Masiyhud-Dajjaal Ni Kweli?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Asalam Aleikum WarahmatuLlahi wabarakatu, Naomba nifahamishwe vizuri kuhusu kureje kwa Nabii Issa (Aleihi Salaam). Kuna mambo ambayo yanayotatiza kuhusu kurejea kwake. Kwanza Nabii Issa alitumwa na Allaah kwa Umma wa Banii Israil ambao walimkataa na kukufuru na alikuja na injili ambayo wakristo wametengeneza yao. Jambo linalonitatiza ni kuwa sisi ni umma wa Mohammad (S.A.W) Na Tumefundishwa Kuwa Hakuna Nabiy Mwingine Atakae Kuja Baada Yake Na Kitabu Cha Koran Ni Mwisho (last Testament). Na Wakristo Wanadai Nabii Issa (yesu) Atakuja Ku-uokoa Ulimwengu Na Kumuua Anaempinga Yeye (ant-christ) Na Sisi Waislamu Tunasema Atakuja Kuvunja Misalaba Na Kumuua Masihi Dajjal (anti Christ) Na Ni Kweli Imani Yetu Haitimii Mpaka Tuamini Nabii Issa Kurudi?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Sisi Waislamu hatuna shida, tatizo wala utata kuhusiana na Nabii ‘Iysa (‘alayhis-salaam) kwani Allaah Aliyetukuka na Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wametuelezea kila kitu kuhusu yeye, kuanzia kuzaliwa kwake, utoto wake, kupazwa kwake mbinguni pasi na kuuliwa na Mayahudi na pia kurudi kwake.

 

Mayahudi na Wakristo wana yao kuhusiana na Masihi mtarajiwa kwa miono yao au maandiko yao. Nasi kama Waislamu tunao yetu ambayo mengine yanafanana na yao na mengine ni yetu khaswa yasiyofanana kabisa na waliyonao wao. Hadiyth sahihi za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) zimetuelezea kwa kina kuhusu kurudi tena Nabiy ‘Iysa (‘Alayhis-salaam). Kuja kwake si kuendelesha utume wake bali ni kufuata yale yote aliyokuja nayo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa njia ambayo atakapokuja hatokuwa ni mwenye kuswalisha bali atamuacha Imaam wa Waislamu awe ni mwenye kuongoza Swalaah.

 

Hili ni suala muhimu la kiimani na jambo la kuamini ghaibu. Na kuamini mambo ya ghaibu ni katika mambo ya Ki-Itikadi na Imani. Allaah Aliyetukuka Amewasifu wale wenye kuamini ya ghaibu kwa kusema:

 

الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْغَيْبِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿٣﴾وَالَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ وَبِالْآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ ﴿٤﴾

Ambao huamini ya ghayb na husimamisha Swalaah na katika vile Tulivyowaruzuku hutoa.Na ambao huamini yaliyoteremshwa kwako (ee Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kabla yako na ni wenye yakini na Aakhirah. [Al-Baqarah : 3 – 4]

 

Bonyeza upate manufaa  zaidi:

 

Hadiyth Ya Al-Jassaasah

Nabii ‘Iysa Atakua Katika Kundi Gani Miongoni Mwa Makundi 72?

Nabii ‘Iysa Ametabiriwa Katika Qur-aan Kuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)?

Nani Aliyesulubiwa Badala ya Nabii 'Iysa ('Alayhis Salaam)?

Nini Ukweli Kuhusu Kupandishwa Nabii 'Iysa عليه السلام

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share