Kusoma Aayah Fulani Au Surah Mara Kadhaa

 

Kusoma Aayah Fulani Au Surah Mara Kadhaa

 

Alhidaaya.com

 

SWALI:

 

A.w.w.katika Ibada Zetu Tunaambiwa Soma Aayah Hiyi Mara Kadha Allah Atakuzawadiya Hiki. Je Hiyo Ni Shirki?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Tunatakiwa tufahamu kuwa ikiwa kusoma huko mara hizo kumetokana na Hadiyth zilizo Swahiyh utakuwa ni mwenye kupata thawabu na kupata hicho ulichoambiwa.  Ikiwa kusoma huko ni katika Itikadi zetu, au maneno ya kutungwa kwa kuzuliwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) utakosa thawabu na kukuingiza katika madhambi. Hivyo, ni muhimu kutazama usahihi wa visomo hivyo kabla ya kuvishika na kuvifuata.

 

 

Lazima kutahadhari na mas-ala ya uzushi kwani yamezidi mno kutokana na wepesi wa mawasiliano. Hivyo ni wajibu wa Muislamu kuhakikisha kwanza habari inayomfikia kuhusu ibada zake kabla ya kuzifanyia kazi au kuzisambaza.  Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi: 

 

 

Hatari Ya Kueneza Hadiyth Dhaifu Na Visa Vya Uongo

Suratul-An'aam Isomwe Siku 40 Kuondosha Mitihani Ya Dunia?

Kusoma Majina Ya Allaah Kwa Idadi Maalum

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share