Amekopeshwa Kwa Pesa Za Kigeni, Je, Anaweza Kulipa Kwa Pesa Za Kwao?
SWALI:
ASSALLAM ALAIKUM
suala langu liko hivi:Mimi nilitumiwa (U.A.E Dirham 20,000) sawa sawa na (TZ shiling millioni 3 na nusu) mwaka 1996 , lakini huyu sasa hivi anataka mimi lazima nimlipe dirham , lakini mimi nimepokea tanzania shillingi million 3 na laki 5 kwa wakati huo ,yeye anataka mimi nimlipe dirham wakati mimi nimepokea tanzania shilingi.Je nafaa mimi kulipa dirham
wabillah tawfiq
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Kuhusu
Amekufadhili na amekufanyia ihsani kwa muda wote huo wa miaka 14 hadi leo bila ya kukulazimisha ulipe.
Juu ya hivyo yeye anataka umlipe kama alivyotoa yaani Dhs 20,000/- na hali wakati huo ilikuwa thamani yake kama unavyosema kuwa ni hizo Shilingi za
Tambua kwamba kwa hivi sasa hizo Dhs 20,000 kwa hivi sasa, thamani yake ni ndogo sana kuliko ilivyokuwa hapo alipokupa mwaka 1996 na kwa hiyo angeliweza kufaidika nazo kwa kufanya mengi kuliko sasa. Kadhalika ana haki hiyo kwani yeye alitoa Dirhamu na hakutoa Shilingi wakati alipokutumia, na hivyo ni haki yake kupewa kilekile alichotoa.
Isitoshe mtu huyo hakutaka faida au Ribaa au kudai kiwango cha hizo Dirhamu kwa thamani ya hivi sasa ambayo bila shaka ingekuwa kubwa zaidi na maradufu ya alivyotoa! Je, bado huoni
Hivyo ni wajib wako hivi sasa kukumbuka ihsani yake na umrudishe kama anavyotaka kwa Dhirhams, na tena tunakshauri umrudishie haraka iwezekanayo na umshukuru kwa ihsani yake na hasa kwa vile hakutaka umlipe thamani ile ile na umuombee Allaah (Subhanaahu wa Ta’ala) Ambariki.
Na Allaah Anajua zaidi