Kutambua Madhii Na Wapi Hasa Yapo Katika Nguo – Kiasi Gani Cha Madhii

 

SWALI:

 

Asalaam aleykum warahmatullah taala wabarakat. Ama baada ya salaam ningependa kwanza kutumia nafasi hii kuwapongeza na kuwashukuru kwa jitihada njema kabisa za kuuelimisha ummah juu ya mas-ala mbalimbali ya kidini, namuomba allah aikubali kazi yenu inshaallah.

 

Swali langu leo ni kuhusiana na "MADHII"

Swali hili lilishaulizwa kabla na mmoja wetu, alhamdullillah nilipata fursa ya kuyasoma majibu yako, lakini kutokana na ugumu wa hili jambo sikuweza kusuluhisha tatizo hili kwa kutumia ushauri ulioutoa. KAMA TUJUAVYO MADHII HUMTOKA MTU WAKATI WOWOTE, HUWA WAZI PALE MTU ANAPOPATWA NA MATAMANIO YA JUU SANA LAKINI VINGINEVYO SI WAZI NA NI VIGUMU KUJUA KAMA YAMEKUTOKA, JE NINI NI KIPIMO CHA KUKUJULISHA KUWA HUENDA MADHII YAMEKUTOKA? IKIWA UMETAMBUA KUWA MADHII YAMEKUTOKA NA HUENDA YAMEGUSA NGUO YAKO YA NDANI KWA MUJIBU WA MAJIBU YAKO YA AWALI ULISEMA NI TOSHA KUNYUNYUZIA MAJI KTK SEHEMU ILIYOADHIRIKA, JE UTAIJUA VIPI HIYO SEHEMU ILIYOINGIWA NA MADHII?

 

 

SWALI LA PILI:

 

mimi ni msichana ambae sijiolewa na nimesoma kwamba mtu akitoka manii ni lazima aoge ndipo afanye ibada ukweli siyajuwi isipokuwa nimesoma kuwa ni kama maji mazito na yana harufu swali je ni wingi gani yanapotoka na jee kuna tofauti wa wingi kwa mwenye kujimai na mwenye kutamani kwa kufikiri

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu madhii.

 

Hakika ni kuwa madhii humtoka mtu akiwa na matamanio ya kutaka kufanya tendo la ndoa. Hakika hakuna kipimo cha kuweza kujua kuwa madhii yamekutoka isipokuwa ule utokaji wake hukujulisha hilo kwani madhii humtoka mtu akiwa macho tofauti na manii ambayo yanaweza mtu akiwa amelala au yuko macho. Ikiwa hali ni hiyo, yanapotoka utahisi na hivyo kujua sehemu yalipoingia.

 

Ikiwa hukuweza kutambua yameingia katika sehemu gani ya nguo, japokuwa jambo hilo ni muhali, ni wewe kuinyunyiza nguo yote kwa maji au kuiosha. Kwa kufanya hivyo utaondoa tatizo linalokukabili.

 

Manii yanapomtoka mtu akiwa amelala au yuko katika kitendo cha jimai basi hata yakiwa kidogo anapaswa kuoga ili awe safi kwa ajili ya ‘Ibaadah kadhaa. Kwa hiyo, ile hali ya kutokwa na manii tu inakubidi uoge.

 

Tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho upate manufaa zaidi:

 

Tofauti Baina Ya Manii Na Madhii Na Hukumu Zake Za Ghuslu

 

Hukmu Ya Wadii Na Madhii

 

008 Nini Hukumu Ya Majimaji (utoko) Yanayotoka Kwenye Utupu Wa Mwanamke Na Kile Kiitwacho Unyevunyevu Wa Utupu Wa Mwanamke?

 

 

Mwanamke Akitokwa Na Majimaji, Je, Aoge Janaba?

 

Na Allaah najua zaidi

 

Share