Tohara Ya Nguo Za Ndani Za Wanawake Katika Kufanya Wudhuu – Je Zinapokuwa Zina Maji Maji Huwa Ni Najisi?
SWALI:
Assalam aleykum,
poleni sana na majukum mlionayo ya kujibu maswali yetu inshaallah allah subnhahu wa-taala awalipeni leo dunian na kesho akhera, swali langu ni kwamba mara nyingi huona wadada wakivua nguo zao za ndani wanapotaka kutia udhu na kuzivaa baada ya kuswali nadhani hii ni kuhofia kwamba inawezekana nguo zao za ndani hazko safi (twahara aidha labda ni manii au madhii) sasa je kama mtu uko mahali ambapo huwezi fanya hivyo inakuwaje itabd usisali hadi utakapopata mahali pa kujitazama kama uko safi au la? Na kama kwenye nguo yako ya ndani ina majimaji ya light yellow yamekauka je hyo inaweza kuwa ni madhii inakubidi uoge ndo uswali na
Samahani ndugu zanguni najua mna memgi ya kufanya ila nawaombeni mnijibu mapema kidogo ili nitoe wasiwasi nlionao mana nahisi
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu utohara wa nguo. Ni jambo linalofahamika kuwa yapo masharti ya kukubaliwa Swalaah ya mmoja wetu na moja wapo ni usafi pamoja na utohara wa nguo Muislamu anazoswalia akiwa ni mwanamme au mwanamke. Allaah Aliyetukuka Anamuagiza Mtume Wake na hivyo kwa kumwambia na kutuambia: “Na nguo zako, zisafishe” (al-Muddaththir [74]: 4). Mbali na kuwa tohara wa nguo ni katika masharti ya kukubaliwa Swalaah, pia Muislamu kila wakati anatakiwa yeye kuwa mswafi pamoja na nguo zake kuwa hivyo.
Katika vitu viwili ambavyo umevitaja ni muhimu kwetu kuvielewa pamoja na hukmu yake, navyo ni manii na madhii. Vitu hivi viwili vina hukmu tofauti katika sheria. Manii si najisi lakini yakimtoka mwanamme au mwanamke ima kwa kuota au kwa kujamiiana au kwa sababu nyengine yoyote ile hatoweza kuswali mpaka aoge josho la janaba. Ilhali madhii ni najisi lakini huhitajii kuoga yanapokutoka kwa ajili ya kufikiria ngono au kwa sababu nyengine yoyote ile. Jambo ambalo linafaa kufanywa ni kuosha ile sehemu katika suruali ya ndani au nguo nyengine yoyote kwa maji kisha ukaivaa kwa ajili ya Swalaah na ikiwa imekauka inatosha kwako kukwaruza sehemu hiyo kisha ukaswali ukiwa umeivaa.
Wapo wengine huwa na wasiwasi tu hata baada ya kuiosha nguo hiyo anaona hawezi kuswali akiwa ameivaa lakini
Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:
Tofauti Baina Ya Manii Na Madhii Na Hukumu Zake Za Ghuslu
Mwanamke Akitokwa Na Majimaji, Je, Aoge Janaba?
Na Allaah Anajua zaidi.