Kiasi Cha Maji Kuondosha Najsi
SWALI:
nikiasi gani cha maji kinaweza ku twaharisha maali ambapo kuna najisi? Naona nikijibiwa mapema nitapata amani ya roho. asante ndungu zangu,Mola awajaanlie mwisho mwema.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Ikiwa najisi ipo kwenye ardhi basi inatosha kumwaga maji sehemu hiyo mara moja. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliamrisha apatiwe maji ile sehemu ya Msikiti ambamo Bedui alikojoa (Al-Bukhaariy na Muslim).
Ikiwa najisi haipo kwenye ardhi, kwa mfano mbwa au nguruwe ameramba chombo panahitajika paoshwe mara saba mojawapo ikiwa ni kwa mchanga (Muslim).
Hukumu hii ni ya ya kijumla kwa vyombo na vyenginevyo kama nguo, godoro na kadhalika.
Ikiwa najisi ni ya mkojo, mavi, damu na mfano wake, unaiosha kwa maji mpaka sura yake, rangi, ladha na harufu yake iondoke. Hivyo, utumiaji wa maji hauna kiasi maalumu ila kila yakiwa kidogo ni bora zaidi. Utazame kuwa hutafanya israfu na ubadhirifu katika hilo. Ikiwa utatumia sabuni na madawa mengine ya kusafishia pia inajuzu.
Kwa maelezo zaidi bonyeza viungo vifuatavyo:
- 009 Najisi Zinazosamehewa
- 010 Namna Ya Kuzitwaharisha Aina Mbalimbali Za Najisi Ambazo Matini Imekuja Kuzibainisha
- 011 Je, Ni Lazima (kutumia) Maji Katika Kuondosha Najisi? Au Inajuzu Kuondosha Kwa Vimiminika Vinginevyo Au Mada Nyinginezo?
Na Allaah Anajua zaidi