09-Kwa Ajili Ya Allaah Kisha Historia: Uzinduzi I

 

Nilimuuliza Imamu Al Khuiy kuhusu maneno ya Amirl muuminin ya kuharamishwa mut’a siku ya khaibara na kuhusu na maneno ya Abii Abdilah ya kumjibu muulizaji wa ndoa isiyo tangazwa,je ilikuwepo katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)? Akasema: maneno ya Amirl muuminin kuhuau kuharamishwa mut’a siku ya khaibara, uharamu huo ni kuwa hiyo ya khaibar tu, baada ya hapo haikuendelea tena

Uharamu huo.

Na  ama usemi wa Abii abdillah akijibu swali alilo ulizwa , imamu Alkhuuiy  anasema kuwa Abii abdillahi alisema  hivyo kwa taqiyya (kudhihirisha kinyume na unavyo amini),na suala hili wamelikubali wamnazuoni wetu.

Mimi nasema: Kwa kweli maneno ya  wanazuoni wetu hayakua sahihi, kwa sababu kuharamishwa mut’a siku ya khaibar kuliambatana na kuharamishwa  punda wa kufugwa na uharamishwaji wa punda wa  kufugwa,umeendelea kufanyiwa kazi toka siku hiyo ya khaibar mpaka leo hii,na itaendelea mpaka siku ya Qiyama.

Kwa hiyo madai ya kuwa mut’a iliharimshwa siku ya khaibar tu nimadai matupu yasiyo kuwa na ushahidi, hasa ukizingatia kuwa uharamu wa punda ambao ndio mwenza wa mut’a uliendelea mpaka leo hii.

Na zaidi ya hayo ingekua kuharamishwa mut’a ni kwa ajili ya sku ya khaibari tu, basi yangepatikana maelezo ya wazi kutoka kwa mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ya  kufuta uharamu huo,muhimu ni kwamba tusisahau ya kua sababu ya kuhalalishw mut’a ilikua ni safari na vita , basi iweje iharamishwe katika vita hiyo na wenye  kupigana wana haja zaidi na kitu hicho (mut’a) hasa ukizingatia wako mbali na wake zao na wajakazi wao,halafu tena ije ihalalishwe wakiwa nyumbani katika hali ya amani?!

    Hakika maana ya Amiril-muminina (Alayhis Salaam) kwamba mut’a iliharamishwa siku ya khaibara maana yake ni kwamba mwanzo wa kuharamishwa mut’a ilikua ni siku ya khaibar, lakini maneno ya wanazuoni wetu ni kuchezea maelezo ya kisheri si vinginevyo.

 

Ukweli ni kwamba kuharamishwa mut’a na punda wa kufuga ni vitu vinavyokwenda pamoja iliteremka hukumu ya kuharamishwa kwake siku ya khaibar na itaendelea hivyo mpaka Qiama wala hakuna sababu ya kuleta maelezo ya mbali katika maneno ya Amiril-muminina (Alayhis Salaam)kwa sababu ya kutaka kushibisha matamanio ya nafsi na kutafuta wanawake wazuri ili kustarehe nao kwa jina la dini.

 

Ama maneno ya Abii Abdillah, katika kumjibu yule muulizaji kua ni taqiyya, mimi nasema kujibu hoja hiyo kwamba muulizaji alikuwa nikatika wapambe wa Abii abdillahi kwa hiyo hapakuwa na sababu ya kuleta Taqiyya kwa hiyo maneno yake hayakua ya taqiyya hasa ukizingatia maneno yenyewe yanakubaliana na maneno yaliyo nukuliwa kutoka kwa miril-muminina (Alayhis Salaam) kwamba mut’a iliharamishwa siku ya khaibar.

 

Hakika ya mut’a ambayo wameiruhusu wanazuoni wetu, inampa haki mwanamume kustarehe na idadi kubwa ya wanawake isiyo wezwa kudhibitiwa,hata  kama wanawake elfu moja kwa wakati mmoja.

Watu wengi waliofanya mut’a wamesha wakusanya mtu na mama yake mtu na mtoto wake mtu na shangazi yake au na mama yake mdogo,nae hajui.

Alinijia mwanamke akinisimulia  tukio lilomfikia alinieleza  kuwa  mmoja wa  wa mabwana wakubwa ,naye ni assayed Huseini Al sadri alikua amefanya nae mut’a kabla ya miaka ishirini na kupata mimba na alipo maliza haja yake alimuacha, na baada ya muda akapata mtoto wa kike,na aliapa kua mimba hiyo ni ya huyo bwana mkubwa , kwa sababu  hakufanya na mtu yoyote wakati huo isipokuwa bwana mkubwa huyo.

Baada ya kukua yule binti na kuwa msichana mzuri anae faa kuolewa, mama aligundua  kuwa binti yake ana mimba,basi alipo muuliza mimba kaipata wapi , binti akamueleza  mama yake kuwa ni ya yule bwana mkubwa alie tajwa alifanya nae mut’a na akapata mimba, mama akapata mshutoko na akachanganyikiwa ,na akamueleza binti yake kuwa huyo mtu (alie mpa mimba) ndie baba yake, na kumueleza kisa chote . vipi mtu anafanya mut’a na mama kisha inakuja siku nyingine anafanya mut’a na mtoto wake mwenyewe?

Kisha akanijia mwana mke huyo akinisimulia kuhusu msimamo wa bwana mkubwa huyo alietajwa kuhusiana na huyo mwanamke na binti yake.

 

Matukio ya aina hii ni mengi sana, kuna watu wamesha fanya mut’a na mabinti kisha wakaja kufahamu kuwa ni dada zao walipatikana kupitia mut’a, wengine wamefanya mut’a wake wa baba zao,

Hakuna anayeweza kueleza matukio yote ya aina hii yaliyo tokea kwa sababu ya mut’a na sisi tumeyashudia wenyewe.

 

 

Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala) anasema:

 (وليستعفف الذين لايجدون نكاحا حتى يغنيهم الله من فضله)  

{Nawajizuie na machafu wale wasipate cha kuolea, mpaka Mwenyezi Mungu atakapo watajirisha kwa fadhila zake} Surat An Nuur, Aya: 33. 

Aya inatufundisha kwamba asiyeweza kuoa ndoa ya sheria  kwa sababu ya kutokuwa na uwezo basi ni wajbu wake kujizuia  mpaka Mwenyezi Mungu atakapo mruzuku kwa fadhila zake ili aweze kuoa.

Basi ingelikuwa mut’a ni halali mtu asingeliamrishwa kujizuia na kusubiri mpaka atakapopata  wepesi wa kuoa, badala yake angeelekezwa kufanya  mut’a kwa ajili ya kuondoa haja yake  badala ya kuumia na matamanio.

Na Mwenyezi Mungu(Subhaanahu wa Ta’ala) amesema:

(ومن لم يستطع منكم طولا أن ينكح المحصنات المؤمنات فمن ما ملكت أيمانكم من فتياتكم المؤمنات)- إلى قوله- (ذلك لمن خشي العنت منكم وأن تصبروا خير لكم والله غفور الرحيم)

{Na asie weza miongoni mwenu kupata mali ya kuolea wanawake waungwana,waislamu, na aoe katika wajakazi wenu waislamu ,na Mwenyezi Mugnu anajua sana imani zenu ninyi kwa ninyi, …endelea mpaka mwenyezimungu aliposema…. hilo ni kwa wale wanaoogopa kufanya uchafu katika nyinyi na mwenyezimungu ni mwingi wa kusamehe na kurehemu.} Surat An-Nisaai, Aya:25

Mwenyezi mungu anawaelekeza  wale ambao hawawezi kuoa kwa kutokua na uezo wawaoe wajakazi wao na mwenye kushindwa kuoa mjakazi pia  basi na avumilie,kama mut’a ingekuwa halali angemuelekeza kufanya hivyo, asinge muamrisha kusuburi.

Tumeona ni lazima kunukuu hoja nyingine kutoka kwa maimamu (Alayhis Salaam) zinazo thibitisha kuharamishwa kwa mut’a!

  1. Imepokewa kutoka kwa Abdullahi bin Sinani amesema : nilimuuliza Abii Abdillah (Alayhis Salaam) kuhusu mut’a akasema:{usiichafue nafsi yako kwa jambo hilo} Buharu Al-Anwar  100/318. na uharamu wa mut’a hapa uko wazi kwa sababu maneno ya wa abii Abdillah (Alayhis Salaam) kua mut’a ina chafua nafsi ina maana ni haramu, na kama ingelikua ni halali isingelikua katika hukumu hii,na al Sadiq hakutosheka kwa hilo bali alisema wazi kua mut’a ni haramu.

 

  1. Amesema Amar: Abuu Abdillah aliniambia mimi na Suleiman bin Khalid (mmeharamishiwa mut’a) Furuu- al Kafiy 2/48,Wasailu Al shia 14/450).

    Na alikua (Alayhis Salaam) akiwakejeli jamaa zake na kuwatahadharisha na mut’a akisema:basi haioni haya mmoja wenu  kuona mahali amepewa mimba mtu mwema katika ndugu zake au jamaa zake? (Al-Furuu 2/43, Al Wasaail 14/450)

 

  1. Na alipomuuliza Aly bin Yaqtin Abal Hasan (Alayhis Salaam) kuhusu mut’a akamjibu: unaitakia nini Mwenyezi Mungu amekutosheleza na hilo. (Al –Furuu 2/43.Al Wasail 14/449).

Ni kweli kabisa kwamba Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala) amewatosheleza watu na mut’a kwa kuwaikea ndoa ya kudumu ya kisheria.

Na  kwa sababu hiyo haikupokewa kuwa kuna  mtu yeyote aliwahi kufanya mut’a na mwanamke katika Ahlul-Bayt (Alayhis Salaam) basi lau ingelikua ni halali wangelifanya  hivyo, na hilo linatiwa nguvu na habari isemayo kwamba Abdallah bin Umair aliesema kumwambia abii Jafar (Alayhis Salaam) {inakufurahisha kuwaona wake zako na binti zako na dada na mabinti wa  Maami zako  wakifanya hivyo? Abuu Jafar (Alayhis Salaam) akampuuza wakati alipo taja wanawake zake na mabinti wa ammi zake (Al-Furuui 2/42, Atahdhiyb 2/186)

 

Na  kutokana na haya inathibitika kwa  kila  muislamu alie na akili kuwa mut’a ni haramu,kwa kwenda kwake  kinyume na Qur-an na sunna  na maneno ya wanazuoni (Alayhis Salaam) .

Na atakayezitazama aya za Qur-an tukufu na hoja nyingne zilizotangulia katika kuharamisha mut’a akiwa ni mwenye kutafuta haki na kuipenda  basi hatukuwa na hukumu zaidi yakuona kuwa maelezo yote yalio kuja kuthibitisha mut’a ni batili, kwa sababu ya kupingana kwake na Qur-an na sunna zilizopokelewa kutoka kwa Ahlul-Bayt (Alayhis Salaam) na kwa sababu ya uharibifu mkubwa unaopatikana katika ndoa hiyo kama tulivyo eleza hapo nyuma.

 

Inalojulikana Kuwa dini ya kiislamu imekuja kuhimiza maadili mema na kukataza  yaliyo maovu,na imekuja kuwahakikishia mambo mazuri  yatakayo wasimamishia maisha yao,na hapana shaka kua mut’a si katika mambo yaliyo na maslahi katika  maisha ya watu, na tukichukulia kwamba mut’a ina maslahi basi ni maslahi ya mtu mmoja, kwa sababu inasababisha madhra mengi kama tulivyo yataja  huko nyuma.

 

Hakika kuenea kwa mut’a imeleta tabia yakuazimana tupu (maana yake ni kumtoa mtu mkewe au mjakazi wake kumpa mwenzake afanye nae mut’a au afanye vyovyote apendavyo,mtu akita kusafiri anamuacha mke wake kwa jirani yake au rafiki yake au yeyote amtakae,  anamruhusu afanye naye chochote apendacho muda wote wa safari na sababu ya kufanya hivyo inaeleweka nayo nikuwa mume anataka atulizane kwa mke wake hatozini wakati yeye hayupo!!

Pia kuna njia nyingine ya kuazimana tupu, pindi anapofika mgeni kwa watu, na wakataka kumkirimu basi mwenye nyumba atamuazima mgeni mke wake katika muda wote wa kukaa pale,

Atamuhalalishia kila kitu, la kusikitisha nikwamba wanatowa riwaya nyingi katika kuthibitisha hayo wakidai kwamba zimepokewa kutoka kwa imamu Al-ssaadiq na baba yake abii jaafar amani ya mungu iwe juu yao.

 

Amepokea Al Tusiy toka kwa Mohammed Bin Abii Jafar (Alayhis Salaam) amesema, niliuliza: {Je mtu anaweza akamhalalishia nduguye kulala na mjakazi wake? Akasema ndio si vibaya ni halali kwake kile alicho halalishiwa.} (Al Istibsaar 3/136.).

 

Amepokea AL- KULAINIY na  Al- tausiy kutoka kwa Mohammed bin Mudharib amesema aliniambia Abuu Abdillah(Alayhis Salaam):( ewe Mohamed mchukue mjakazi  huyu akuhudumie na umuingilie utapoondoka turejeshee) Al Kafiy, Al Furuu 2/200, Al Istibsaar 3/136).

Nikasema: Lau wangekusanyika watu wote wakaapa kuwa maimamu wawili Al sadiq na Al Baaqir (Alayhis Salaam) kwa wamesema mneno haya nisinge kubali.

Hakika maimamu wawili hawa (Alayhis Salaam) haifanani kusema maneno maovu kama haya.

 

Hawawezi  kuruhusu kitendo kiovu kinachopingana na tabia tukufu za kiislamu , kitendo kama hiki ni udayuthi (kutokua na wivu)  hapana shaka kuwa viongozi (Alayhis Salaam) wameirithi elimu hii tangu na tangu yakinasibishwa maneno haya na matendo haya kwao,ina maana kuwa yamenasibishwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na yakinasibishwa na mtume basi itakuwa ni sheria ya Allah (jambo ambalo haliwezekani)

 

Tulipoitembelea India na huko tukakutana na viongozi wa kishia kama bwana Al Naqwiyu na wengineo tukapita katika kundi la  Mahindus na wanaoabudu N’gombe na ibada za kipuuzi na wengineo wanaofuata  dini za  kijahili, na tukasoma sana kuhusu dini zao lakini hatukukuta dini yoyote kati ya dini zao inayo halalisha kitendo hicho kwa wafuasi wake.

 

Itawezekana vipi kwa kidini ya kiislamu ihalalishe kitu kichafu kama hiki ambacho kina kwenda kinyume na vipimo vidogo tu vya kitabia?

 

Tulitembelea chuo kimoja cha kiislamu kilichopo  Iran  tukawakuta mabwana wakubwa wakihalalisha kuazimana tupu , na miongoni waliotoa fatwa ya  kuruhusu jambo hilo ni Asayyid Lutfillahi Asaafiy na wengineo,kwa hiyo suala la kuazimana tupu limeenea  Iran yote,na  likaendelea kufanyika tendo hilo mpaka baada ya kuangushwa Shaha  Mohammad Ridha Bahlawiy nakuja kwa Ayatullahi Al udhma Al imam al Khomainiyu , Al muusawiy na baada  ya kufa Al imam Al Khomaniyu tendo hilo liliendelea na hii ikawa moja ya sababu ambazo zilipelekea kufeli dola ya kwanza ya kishia katika zama hizi,mashia katika ulimwengu mzima walikua wakiiangalia kwa makini dola hiyo, kufeli kwa dola hiyo ni katika mambo yaliyo changia mabwana wakubwa wengi kujitenga nayo na kuuipiga vita ,  huyu hapa rafiki yetu mwanazuoni Assayid Musa Al muusawiy aliyaita mapinduzi ya Irani kuwa ni mapinduzi yasiyo na matumaini  na akatunga  vitabu na akaeneza maqala nyingi katika kuipiga vita hiyo na kubainisha makosa yake.

 

Anasema bwana Jawad Al muusawiy hakika mapinduzi ya kiislamu ya Ira si kwa ajili ya uislamu hata kidogo isipokua ni jina tu.

Na alikua Ayatullahi al udhma Asayid Mohamed Kadhim Shari Ya’tamidariy ni miungoni mwa wapiganaji wakubwa wa mapinduzi hayo kwa upotokaji wa wazi aliouona unaenda kinyume na misingi ya uislamu.

Pia kuna mabwana wakubwa wengi ninao wajua mimi mwenyewe waliilaumu serekali ya imamu khomeyniy na kuiasi.

 

Na yanayo sikitisha sana ni kwamba mabwana wakubwa wametoa fatwa ya kuruhusu kuazimana wanawake, kuna familia nyingi kusini mwa iraki na Baghdadi pia katika maeneo ya mapinduzi  zinaendelea kufanya jambo hili kwa kufuata fatwa za mabwana wakubwa wengi kama vile:  Asaysatani na Asadri na Ashyrazy na Al tabatabaiy na  Al burujardy na wengineo,na wengi wao wakiwa wageni sehemu kwa mtu basi wana muazima mke wake wakimuona ni mzuri ataendelea kukaa nae hivyo mpaka aondoke!!.

 

Hakika wajibu wetu ni kuwatahadharisha watu juu ya kitendo hiki kibaya na wala wasikubali fatwa za mabwana wanao ruhusu tendo hili baya ambalo nguvu zilizo jificha nyuma ya pzia zina mchango mkubwa sana katika kuliingiza jambo hili katika dini na kulieneza kwa watu.

 

Mambo hayakuishia hapo bali wali halalisha tendo la Qaumu luti kwa wanawake na zikapokewa riwaya nyingi zilizonasibishwa kwa viongozi(Alayhis Salaam) amepokea Atuusiy kutoka kwa Abdillah bin Abii Al Ya’fur akisema: (nilimuuliza Abaa Abdillah (Alayhis Salaam)kuhusu  mtu anaye muingilia mkewe nyuma, akasema: si vibaya kama ataridhika,nikasema  likowapi neno la Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) lisemalo

(فأتوهن من حيث أمركم الله)

{Waendeeni katika njia aliyowamrisha Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) basi akasema  hii ni  kwa kutafuta mtoto,basi  tafuteni watoto kwa njia aliyowaamrisha Mwenyezi Mungu, kwani Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) amesema:

(نساؤكم حرث لكم فأتوا حرثكم أنى شئتم)

{Wanawake wenu ni mashamba yenu yaendeeni mashamba yenu mpendavyo} Al-Istibsaar 3/243.

 

Pia Atuusiy kapokea kutoka kwa Musa bin Abdillahi kutoka kwa mtu mmoja akisema: (nilimuuliza Abal- Hassan Aridhaa (Alayhis Salaam) mtu kumuingilia mkewe nyuma, akasema: imehalalishwa na aya katika kitabu cha Mwenyezi Mungu, aliposema Lut (Alayhis Salaam)

(هـؤلاء بناتي هن أطهر لكم)

(Mabinti zangu hawa kwenu ni tahara) alijua kuwa wao hawataki njia ya kawaida ya kimaumbile, Al-Istibsaar 3/243.

Na amepokea Atuusiy kutoka kwa Ally bin Hakam amesema, nilimsikia Safwani akisema: nilimuambia Alridha(Alayhis Salaam) (hakika ya mtu mmoja wa karibu yako ameniamrisha nikuulize mas-ala anakuogopa na anakuonea haya kukuuliza,akasema ni yapi hayo? Akasema:je mtu anaruhusiwa kumuendea  mkewe nyuma? Akasema: ndiyo inafaa kufanya hivyo.) Al Masdar Al Sabiq.

 

Hakuna shaka kuwa habari hizi zimepingwa na Qur-an kwani Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala) anasema

(يسألونك عن المحيض قل هو أذى فاعتزلوا النساء في المحيض ولاتقربوهن حتى يطهرن) البقرة :222

{Na wanakuuliza kuhusu hedhi, waambie ni uchafu basi jitengeni nao wakiwa katika hedhi na wala msiwangilie mpaka wataharike} Sura 2 Aya  222.

 

Lau kama kumuingilia nyuma kunaruhusiwa angaliamrisha  kuacha  utupu wa mbele tu. Na (angesema jitengeni na utupu wa mbele wakiwa katika hedhi).lakini kwa sababu kumuingilia mwanamke nyuma ni haramu imeamrishwa kuziepuka sehemu zote mbele na nyuma ndio maana akasema (msiwa karibie) kisha  akabainisha  Mwenyezi Mungu  baada  ya hayo sehemu ya kuingiliwa mwanamke,akasema Allah (Subhaanahu wa Ta’ala):

 (فإذا تطهرن فأتوهن من حيث أمركم الله)البقرة:  222

{Wakishataharika basi waingilieni sehemu aliyo waamrisha Mwenyezi Mungu} Sura 2 Aya 222.

Na Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) ameamrisha kuwaingilia wanawake katika sehemu ya mbele aliposema:

(نساءكم حرث لكم فأتوا حرثكم أنى شئتم) البقرة:322

{Wanawake ni mashamba yenu yaingilieni mashamba yenu mpendavyo} Sura 2 Aya 223, na shamba ni sehemu ya kutafutia mtoto.

 

Hakika riwaya ya Abii Al Ya’fur kutoka kwa Abii Abdillah maana yake nikua kutafuta mtoto inakua katika tupu za mbele kwa maneno yake Allah (Subhaanahu wa Ta’ala)

(نساءكم حرث لكم فأتوا حرثكم أنى شئتم)

(wanawake wenu ni mashamba yenu} basi hii ni katika katafuta mtoto, maana ya riwaya hii nikuifanya tupu ya mbele ni kwajili ya kutafuta mtoto tu, ama kukidhi haja za kimwili ni kwa utupu wa nyuma na maelezo ya riwaya hii yako wazi katika kuleta ufahamu huu.

Na hili ni kosa kwa sababu utupu wa mbele siyo maalum kwa kutafutia mtoto tu bali pia kwa kukidhi haja na matamanio ya kimwili. na hiyo ndio hali halisi ya maisha ya ndowa tangu enzi za Adamu (Alayhis Salaam)mpaka qiama  na Abuu Abdillah hafanani kusema maneno maovu kama haya. na lau tungechukulia kwamba inafaa mtu kumuingilia mkewe nyuma basi kusingekuwa na maana mwenyezi mungu kusema

 (فإذا تطهرن فأتوهن من حيث أمركم الله)

{Basi wakishatwaharika waingilieni sehemu aliyowamrisheni mwenyezi mungu} kwa sababu sehemu ya kumuingilia mwanamke tayari inafahamika ni mbele au nyuma na hakuna sehemu nyingine ya tatu, (hii ni kwa kuchukulia ingefaa kufanya hivyo) kama wanavyo dai.

Lakini  ilipokua moja ya sehemu mbili hizi si halali  haifai kuiendea na nyingine ni halali basi ulihitajika ufafanuzi ni ipi sehemu inayofaa kuiendea  ikawa amri ya Allah(Subhaanahu wa Ta’ala) ni kuiendea sehemu ya kuotesha( shamba), na shamba ni ile sehemu ya kutafutia mtoto,na sehemu  hii ndiyo sehemu inayoendewa kwa kutafuta mtoto na kukidhi haja za kimwili pia.

 

Ama riwaya iliyonasibishwa kwa Al-ridha (Alayhis Salaam) katika kuruhusu kuliwatiwa wanawake na kutoa hoja  ya maneno ya nabii Luti (Alayhis Salaam).

Basi mimi ninasema :hakika tafsiri ya maneno ya Allah (Subhaanahu wa Ta’ala)

(هــؤلاء بناتي هن أطهر لكم) هود:78 

{Mabinti zangu hawa kwenu ni tahara) Sura Huud Aya:78 imepatikana katika aya nyingine usemi wake Allah(Subhaanahu wa Ta’ala)(ولوطا إذ قال لقومه

 إنكم لتأتون الفاحشة ما سبقكم بها من أحد من العالمين*أئنكم لتأتون الرجال وتقطعون السبيل) العنكبوت :28

{Na Lut alipowaambia watu wake kuwa ninyi mnaleta uchafu haukufanywa na yeyote katika viumbe walio kabla yenu, Ninyi mna waingilia wanaume na kukata nasab} Al Ankabuut 28-29.

Kukata njia haina maana yale yanayo fanywa na majambazi peke yao laa sihivyo  ina maana pia ya kukata kizazi kwa  kuingilia sehemu isiyo kua ya kutafutia mtoto,yaani sehemu ya nyuma, basi lau kama watu wangeendelea kuingilia nyuma za wanaume na wanawake na wakaacha  kutafuta watoto watu wangelimalizika na kizazi kingelikoma.

Aya  hii tukufu pia  inatupa maana hiyo hiyo na khasa tunapoangalia kwa makini mtririko wa aya iliyo nyuma yake ,hakuna shaka kuwa haya  hayakujificha kwa  Imamu Al-ridha (Alayhis Salaam), hivyo inathibitika uongo wa  kuinasibisha habari hii kwake.

 

Hakika kuingilia nyuma wanawake halikusemwa hilo na mtu yoyote isipokuwa mashia Ithna asharia.

Jua kwamba mabwana wakubwa katika chuo cha kishia cha Annajaf na vyuo vyote vya kishia na kila mahali walipo wanakifanya kitendo hicho (kuwainglia wanawake nyuma)!

Na alikua rafiki yetu Al Hujatu Asyidu Ahmad Al wailiyu akisema tangu alipo ziona riwaya hizi alianza kukifanya kitendo hicho na ni mara chache ambazo anamuingilia mwanamke katika sehemu ya mbele.

Na kila  nilipokutana na mmoja kati ya hao mabwana wakubwa  na katika kila sehemu ninauliza uharamu na uharamu wa mwanamke kuingiliwa nyuma  basi  hunijibu kuwa ni halali na kutaja riwaya  mbali mbali zinazoruhusu jambo hilo nyengine ni hizi tulizo zitaja hapo nyuma.

Hawakutosheka kuruhusu kulawitiwa wanawake tu bali pia wengi kati yao wameruhusu  kulawitiwa hata wanaume hasa walio karibu baleghe.

Siku moja  tukiwa chuoni zilipatikana habari kuwa mtukufu Asayid Abdul Hussain Sharafu ddiyn  Al Muusawiy amefika Baghdad, na atafika chuoni ili akutane na mtukufu  Al Imamu Alu Kashifu Al Ghataa, na alikua Asayid Sharafu Ddiyn amepata umaarufu kwa mashia wote.  Khasa baada ya kutoka vitabu vyake alivyoviandika kama Al-muraajaati na Annsu na Al-ijitihadi.

 

Alipofika Annajaf allitembelea chuoni makaribisho yake yakawa makubwa kutoka kwa wana chuo walimu na wanafunzi na  katika kikao chao kilichofanyika katika ofisi ya al sayid Al Khashif Al Ghataa, kilicho kusanya idadi kubwa  ya mabwana wakubwa  na baadhi ya wanafunzi , nami nilikua ni mmoja  ya waliohudhuria, katikati ya kikao aliingia kijana mmoja akatoa salamu kisha akasema kumwambia Asayid Al Khashif Al Ghataa: bwana  nina swali,bwana Al kashiful-ghataa akamwambia: uliza swali lako kwa Asayid Sharaf Adiyn akalirusha swali kwa  mgeni wake Asayid Sharaf Adiyn kwa kumtukuza na kumuheshimu.

Muulizaji akasema: bwana mkubwa, mimi ninasoma London nikichukua digirii ya tatu (Ph.d), nami sijaoa, na nataka mwanamke atakayenisaidia huko, lengo lake hakuliweka wazi, akamjibu Asayid Sharaf Adiyn, oa kisha mchukue mkeo uwende nae.

Yule mtu akasema ni vigumu kwangu kuishi na mwanake kutoka kwetu katika nchi hiyo.

Asayid Sharaf Adiyn, akaelewa lengo lake, na akasema kwahivyo unataka kuoa mwanamke mwingereza? Yule mtu akasema ndio, akamwambia Sharaf Adyin: hilo hailifai, kumuoa myahudi au mkristo ni haramu, yule mtu akasema hivyo nifanyeje? Akamwambia Asayid sharaf Adiyn: mtafute mwanamke muislamu mkazi wa huko wa kiarabu au wa kihindi au jinsia yeyote nyingine, kwa sharti awe muislamu.

Yule mtu akasema: nimetafuta sana sijapata katika waislamu wakazi wa huko, anaefaa kuwa mke wangu mpaka nilifikia kutaka  kufanya mut’a pia sikupata, na hakuna mbele yangu khiyari yoyote zadi ya ima Uzinifu na ima kuoa na yote mawili haya  kwangu hayawezekani.

Ama zinaa niko mbali nayo kwakua ni haramu na  ndoa haiwezekani kama ulivyoona nami nakaa huko mwaka mzima au zaidi, kisha narudi likizo kwa muda wa mwezi mmoja ,na kama ujuavyo safari ni ndefu nifanyeje?

Alinyamaza Asayid Sharaf Adiyn kidogo na akasema: hakika tatizo lako hili ni zito, lakini usijali kwani niliwahi kusoma riwaya kutoka Imamu Jafar Al Sadiq (Alayhis Salaam) wakati alipojiwa na mtu anayesafiri sana na akamtolea shida na ikawa vigumu kuongozana na mke wake na ni vigumu kufanya mut’a katika mji anao safiri kiasi akawa anapata shida kama wewe, basi Abu Abdillahi akamwambia safari ikiwa ndefu kwako basi juu yako kumuoa mwanamume, hili ndilo jawabu la suala lako.

Aliondoka yule mtu akiwa na alama ya shaka kutokana na jibu hili,ama wale waliohudhuria akiwemo bwana mkubwa mkuu wa chuo hakutamka mmoja  wao chochote.

Alikamatwa  bwana mkubwa mmoja hapa chuoni akimlawiti mvulana mmoja mdogo katika wana funzi wa hapa chuoni, Habari zikawafikia watu wengi, siku iliyofuata alipokua  bwana mkubwa huyo akitembea katika bustani ,alimkaribia  bwana mkubwa mwingine miongoni mwa wanazuoni wa chuo ,na alikuwa amezipata habari , akasema  kwa lugha fasaha huku  akimfanyia mzaha:bwana unsema nini kuhusu kulawiti?yule mwengine  akamjibu kwa mzaha zaidi akisema kumwambia  na kwa ufasaha tena. Imependekezwa kuingiza kichwa cha dhakari tu,kisha wakajikohoza kwa nguvu wote wawili!!

Na yuko bwana mwingine miongoni mwa wanazuoni wa Hoza (chuo)anajulikana kw kulawiti , alimuona mtoto mdogo akitembea pamoja na bwana mkubwa  wengine miongoni mwa wanazuoni wa Hoza(chuo) vilevile,akaamuuliza,ni mtoto gani huyu uliye nae? Akamjibu: huyu mtoto wangu fulani (akamtaja jina) Akamwambia: kwanini  hakumleta kwetu ili tumsomeshe na kumpatia elimu ili  awe mwanazuoni kama wewe? Akamjibu kwa dharau: ewe mwanachuoni muovu mpuuzi unataka nikuletee ili umfanyie (hivi na vile)?! Na tukio amenizungumzia mtu muaminifu miongoni mwa waalimu wa Hoza (chuo)

.

 

Tumeona matukio mengi kama haya, na tuliyoyasikia ni mengi zaidi mpaka imefikia rafiki yetu mpemzi bwana Abasu amekusanya matukio mengi sana, na kuyaandika kwa upana na kwa tarehe zake  majina ya wahusika. Nae anakusudia kuyatoa katika kitabu anachotaka kukiita FADHAIHU AL-HOZATI AL-ILMIYAT FI AL-NAJAF (habari za kufedhehesha za chuo cha kishia cha najaf) kwa sababu ni wajibu kuuweka wazi ukweli kwa mashia wa kawaida masikini wasiojui  yanayo pita nyuma ya pazia, na wala  hawayajui wanayoyafanya mabwana wakubwa wa kishia , mpaka inafikia , mmoja wao  anampeleka mkewe au binti yake au dada yake,kwa ajili ya ziara au kutafuta mtoto au kupeleka zawadi kwa ajili ya Hussain) basi wanampokea mabwana wakubwa  hasa akiwa mzuri na kufanya nae machafu na kumfanyia kila uovu, hakuna hila wala nguvu isipokua kwa msaada wa Allah(Subhaanahu wa Ta’ala).

 

 

 

Share