Biashara Ya Vitu Vilivyokatazwa Na Serikali Japo Dini Haikuharamisha
SWALI:
Asalamu aleykum sheikh. Swali yangu ni kuhusu haramu na halali. nauliza hivi hapa nchini kwetu kuna vitu serikali imeharamisha, hata
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani kwa swali lako kuhusu biashara zilizokatazwa na serikali.
Huenda kukawa na biashara ambazo Kiislamu ni halali, lakini zikapigwa marufuku na serikali.
Kufanya shughuli kama hizo ni halali kishari’ah kufanywa, hata hivyo kwa kufanya
Kwa minajili hiyo kwa nini Muislamu ajiingize katika matatizo kwa kufanya biashara hizo ambazo atakuwa anazifanya kwa siri na huenda zikampelekea katika madhambi makubwa
Uislamu unazingatia kuwa wanyama wana haki ya kuishi kama wanaadamu na wanauliwa tu kwa maslahi ya wanaadamu kama kula nyama
Kwa ajili hiyo, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametoa ruhusa hata kwa muhrim kuwaua wanayama wa tano lakini wote hawa hawana maslahi na wanaadamu. Nao ni nnge, panya, mbwa mwenye kichaa, kunguru na kipanga (al-Bukhaariy).
Ama kumuua tu mnyama kwa sababu ya ngozi, pembe au kimchezo ni jambo ambalo halifai isipokuwa anapoleta maafa kwa wanaadamu. Hivyo, ni afadhali uachane na biashara hiyo na uanze kufanya nyingine njema isiyo na utata.
Na Allaah Anajua zaidi