Utoaji Wa Zakaah Kutoka Katika Mshahara Na Duka
SWALI:
Assalam alaykum, mimi ni mwanamke nimeolewa na ninaishi nchini Japani na mume wangu. Swali langu ni mshahara wangu kwa mwezi ni yeni laki moja je ninatakiwa kutoa zakkah kiasi gani? Na pia nina miliki duka ambalo bado halijaanza kutoa faida ni miezi miwili sasa tokea nifungue duka
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani kwa swali lako kuhusu utoaji wa Zakaah.
Zakaah ni ‘Ibaadah na miongoni mwa nguzo ya Uislamu muhimu
1. Kuwa na Niswaab (kiwango cha chini) ambapo Muislamu akiwa nacho inampasa yeye kutoa Zakaah. Na kiwango hicho ni mtu kuwa na akiba ya pesa zinazotosha kununua gramu 82 za dhahabu
2. Akiba hiyo ipitiwe na mwaka katika kalenda ya Kiislamu bila ya kupungua kabisa.
Ikiwa umetimiza masharti haya mawili basi inakupasa kutoa Zakaah. Sasa ni kutazama akiba yako kwa mfano mshahara wako ni yeni laki moja, lakini akiba yako mwisho wa mwezi ni ngapi? Ikusanye hiyo akiba kila mwezi mpaka ifike hiyo Niswaab. Tarehe akiba yako itakapofikia Niswaab ndio utaanza kuhesabu mwaka, ikiwa baada ya mwaka kiwango ni vile vile au kimepanda itabidi utoe Zakaah. Na ikiwa hutofikia Niswaab hakuna Zakaah kwako mpaka uifikie hiyo Niswaab.
Ama duka nalo ni hivyo hivyo, utakusanya faida unayopata
Na Allaah Anajua zaidi