Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Kufundisha Baada Ya ‘Ishaa

SWALI:

 

Mtume saw alitoa mawaidha au kufundisha baada ya sala ya isha?


 

JIBU: 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. 

Shukrani kwa swali lako kuhusu ufundishaji wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya ‘Ishaa.

Kwanza tunapenda kukukumbusha unapomtaja Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kumuombea rahma na amani, basi andika kwa utajo uliokamilika na unaofahamika badala ya kuandika kwa ufupi saw, kumbuka hiyo ni heshima zaidi na mapenzi zaidi. Tunaweza kuandika mambo mengine kwa urefu yakaeleweka lakini tunapomuombea kipenzi chetu tunamfupishia. Haifai na haipendezi.

Ama kuhusu swali lako ulilouliza, ni kuwa hakuna tulipoona mafunzo sahihi ya kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwahi kufundisha baada ya Swalaah ya ‘Ishaa kwa kuwa kwa mujibu wa maelekezo yake katika Hadiyth ni kuwa kusiwe na mazungumzo baada ya Swalaah hiyo.

Sababu ya maelekezo hayo yake ni watu wapate fursa ya kulala mapema na kuinuka usiku kwa ajili ya Tahajjud na pia kuwahi Swalaah ya Alfajiri.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share