Mtoto Atumie Njia Zipi Za Kumnasihi Mama Anapokosea Bila Kusababisha Kutokuelewana
Mtoto Atumie Njia Zipi Za Kumnasihi Mama Anapokosea Bila Kusababisha Kutokuelewana
SWALI:
ikiwa mama ana makosa juu ya mtoto na mtoto afanye nini kunjulisha mama eli mama afahamu bila kutoelewena na mamake na mtoto asifanye chuki na mamake.
JIBU:
AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho
Nasaha na kuamrisha mema na kukataza maovu ni muhimu ifanywe kwa njia nzuri, kwa hekima na mawaidha mazuri. Na haya yatakiwa yafanywe kwa yeyote yule sio mama tu kwani Allaah Aliyetukuka Anatuelezea:
ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ
Lingania katika njia ya Rabb wako kwa hikmah na mawaidha mazuri. [An-Nahl: 125].
Kwa minajili hili mtoto anaweza kutumia njia nyingi za upole na nzuri ili kurekebisha makosa hayo. Njia hizo ni kama:
1. Kumpatia mama vitabu kwa lugha anayoielewa kama vile Qur-aan na tafsiri yake, Muislamu anavyopaswa kuwa, Iymaan na maelezo yake, Siyrah ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Visa vya Manabii na Swahaba. Baada ya hapo unaweza kuja katika tatizo alilo nalo mama.
2. Kumpatia kanda za kusikiliza, video, VCD, DVD za mawaidha ya Kiislamu.
3. Kumhimiza kuhudhuria mihadhara, darsa na khutbah za Ijumaa.
4. Kumshirikisha na vikundi vya kinamama wenye Msimamo wa Sunnah.
5. Kutumia watu wake na wako wa karibu katika kurekebisha hali hiyo.
6. Na njia nyenginezo ambazo unaziona ni munasibu kutegemea na mazingira yenu.
Na Allaah Anajua zaidi