Kuzaa Nje Ya Ndoa Na Kutaka Kuolewa Na Huyu Mwanamme Aliyezaa Naye
SWALI:
Assalam wallakum, nina swali linanikosesha raha. Sijawahi kuolewa, nimezaa. Baba mtoto anataka kunioa kwani kumekiri makosa. Je inawezekana?
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani kwa swali lako kuhusu kutaka kuolewa na mwanamme aliyekuzalisha bila ya ndoa.
Kwanza, tunataka kukujulisha kuwa swali
Pili, kabla ya kukujibu kuhusu kuwezekana kuolewa na mwanamme huyo ni kukufahamisha kuwa kitendo ulichofanya ni katika madhambi makubwa. Kwa hiyo, inatakiwa nyote wawili muombe msamaha kutoka kwa Allaah Aliyetukuka kwa kutimiza masharti yafuatayo:
1. Kujiondoa katika maasiya.
2. Kujuta kufanya maasiya hayo.
3. Kuweka azma ya nguvu kuwa hutarudia tena kosa
Baada ya nyinyi kuomba msamaha kwa kutimiza masharti hayo na kupita kipindi ambacho kitaonyesha na kudhihirisha manadiliko kwenu ya kitabia ba naadili, basi mnaweza kuoana kwa sharti kuwa yule mtoto hatoitwa kwa ubini wa mume wako ambaye kibayolojia ni baba yake lakini kishari’ah si baba yake. Mtoto huyo hataweza kumrithi baba huyo wala baba kumrithi mtoto huyo.
Kwa muhtasari ni kuwa hakuna makatazo ya nyinyi kuweza kuoana.
Ingia katika viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi kuhusu suala
Ndoa Ya Waliozini Kwa Mtazamo Wa Ahlus Sunnah Wal Jama'ah
Watoto Baada Ya Ndoa Ya Uzinifu
Wazinifu Waliotubu Wanaweza Kufunga Ndoa Na Waliotakasika
Nini Hukmu Ya Watoto Wa Nje Ya Ndoa?
Ndoa Inafaa Baada Ya Kumchezea Mwanamke?
Avunje Ndoa kwa sababu Walizini Kabla ya Ndoa?
Wamezini Kisha Wakaoana Bila Kufanya Tawbah Kwa Kuwa Walikuwa Hawajui, Nini Hukmu Ya Ndoa Yao?
Avunje Ndoa kwa sababu Walizini Kabla ya Ndoa?
Na Allaah Anajua zaidi