Sababu Za Kukhitilifiana ‘Aliy na Mu’aawiyah (رضي الله عنهما)
SWALI:
ASSALAM ALYKUM.
bismi llah rahman rahiim
Mimi napenda nipate ufafanuzi wa kutosha kuhusu hatua ya Ally kuamua kumpiga vita Mu'awiyah. Kwani invoonekana Ally ndio aliondoka madina kumfata muawiah. Kwani hiki kitu kinanisumbua
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu kutofautiana baina ya ‘Aliy bin Abi Twaalib na Mu’aawiyah (Radhiya Allaahu ‘anhuma).
Hakika ni kuwa katika kisa hiko cha kutofautiana kwa Maswahaba wawili hao yameongezwa mengi yasiyo ya sawa kwa sababu ya ushabiki.
Na haswa upande wa Mashia wameweka na kuongeza mengi juu suala
Kabla ya kuingia katika suala
Makundi hayo mawili yalikutana ana kwa ana, na ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamtuma mwakilishi wake, Qa‘qaa’ bin ‘Amr (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwenda kuzungumza na uongozi wa upande wa pili. Mazungumzo hayo yalileta natija nzuri na hivyo maharamia ambao walimuua ‘Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘anhu) wakaona wachukue fursa ya kuleta vurugu usiku ili watu wa makundi hayo mawili wapigane. Na bila shaka waliweza kufanikiwa na kuleta hasara kubwa katika ummah wa Kiislamu.
Tatizo lililotokea baina ya ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye ndiye aliyekuwa Khalifah na Mu’aawiyah (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye alikuwa liwali wa Shaam kuanzia wakati wa ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) ni tatizo la ijtihadi. Kwa muono wa ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) ilikuwa waliotekeleza uhalifu wachukuliwe hatua kwa taratibu ilhali Mu’aawiyah (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye alikuwa na uhusiano wa kidamu na ‘Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa anataka kisasi kichukuliwe mara moja.
Tatizo
Kwa hiyo, tofauti iliyokuwepo baina ya ‘Aliy na Mu’aawiyah (Radhiya Allaahu ‘anhuma) niya kiijtihadi na kisiasa na wala sio ya kimadhehebu
Na Allaah Anajua zaidi