052-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Tashahhud Ya Mwisho Na Uwajibu Wake
Tashahhud Ya Mwisho
Wajibu Wa Tashahhud Hii
Kisha baada ya kumaliza Rak’ah ya nne, alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akikaa kwa ajili ya Tashahhud ya mwisho. Aliwaamrisha kuhusu hii na akifanya kama alivyofanya katika Tashahhud ya kwanza isipokuwa “alikaa mutawarrikan”([1]) “paja lake la kushoto likiwa ardhini na miguu yake yote miwili ikitokeza kutoka upande mmoja (yaani upande wa kulia)”([2]) “Aliweka mguu wake wa kushoto chini ya paja (la kulia) na muundi”([3]) “mguu wake wa kulia akiuinua”([4]) au mara nyingine “akiulaza pamoja ardhini”([5]) “paja lake la kushoto lilifunika goti lake (kushoto) akiliegemeza”([6])
Ameweka mfano wa kumswalia yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Tashahhud,
[1] Al-Bukhaariy.
[2] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni. Ama katika Swalah ya rakaa mbili
[3] Abu Daawuud na Al-Bayhaqiy ikiwa na isnaad Swahiyh.
[4] Muslim na Abu ‘Awaanah.
[5] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni
[6] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni