053-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Wajibu Wa Kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

 

Wajibu Wa Kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

Alimsikia mtu (صلى الله عليه وآله وسلم) akiomba du’aa bila ya kumtukuza Allaahتعالى   , wala kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) hivyo akasema: ((Huyu mtu ameharakiza)). Kisha akamwita na kumwambia yeye na wengineo: ((Anaposwali mmojawenu, aanze kwa kumsifu Mola wake, (عزرجل) na kumtukuza kisha amswalie [katika usimulizi mmoja: amswalie] Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kisha aombe anayotaka)).([1])

Pia, “alimsikia mtu akimtukuza na kumsifu Allaah na kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Swalah, hivyo Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: ((Omba na utaitikiwa, uliza utapewa))([2])

 

 

 

 



[1]Ahmad, Abu Daawuud, Ibn Khuzaymah (1/83/2) na Al-Al-Haakim ambaye amekiri ni Swahiyh na Adh-Dhahabiy amekubali.

[2] An-Nasaaiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

Share