Ummah Wetu Wa Kiislam Utakuwa Wa Kwanza Kuingia Peponi

 

Ummah Wetu Wa Kiislam Utakuwa Wa Kwanza Kuingia Peponi

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 كَانَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً فَبَعَثَ اللَّـهُ النَّبِيِّينَ مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ وَأَنزَلَ مَعَهُمُ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِيَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ فِيمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ ۚ وَمَا اخْتَلَفَ فِيهِ إِلَّا الَّذِينَ أُوتُوهُ مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۖ فَهَدَى اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا لِمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِهِ ۗ وَاللَّـهُ يَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٢١٣﴾ 

 

Watu walikuwa ummah mmoja kisha Allaah Akatuma Nabiy wabashiriaji na waonyaji na Akateremsha pamoja nao Kitabu kwa haki ili kihukumu baina ya watu katika ambayo wamekhitilafiana kwayo. Na hawakukhitilafiana katika hayo isipokuwa wale waliopewa hicho (Kitabu) baada ya kuwajia hoja bayana kwa kufanyiana baghi na uhusuda baina yao. Allaah Akawaongoza wale walioamini kuendea haki katika yale waliyokhitilafiana, kwa idhini Yake. Na Allaah Humwongoza Amtakaye kuelekea njia iliyonyooka. [Al-Baqarah: 213]

 

Ibn 'Abbaas amesema kuhusu kauli hii: "Kulikuweko na vizazi (karne) kumi baina ya Aadam (‘Alayhis-salaam) na Nuwh (‘Alayhis-salaam), wote wakiwa katika dini ya haki. Kisha tena wakakhitilafiana, hivyo Allaah Akatuma Rusuli kama waonyaji na wabashiriaji" [Tafsiyr Ibn Kathiyr].

 

 

 

Idadi ya Rusuli ni 124,000 wakiwemo Wajumbe 313 kama ilivyo kauli ya wengi wa ‘Ulamaa wa Ahlus-Sunnah wal Jama’ah. Rusuli 25 wametajwa majina yao katika Qur-aan. [ Aysarut-Tafaasiry – Abuu Bakr Al-Jazaairy 1:191].

 

 

Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) alisema kuhusu kauli:

 

 فَهَدَى اللّهُ الَّذِينَ آمَنُواْ لِمَا اخْتَلَفُواْ فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِهِ

 

Allaah Akawaongoza wale walioamini kuendea haki katika yale waliyokhitilafiana, kwa idhini Yake. [Al-Baqarah: 213]

 

 

 

Akasema kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

 ((نَحْنُ الْآخِرُونَ الْأَوَّلُونَ يَوْم الْقِيَامَة نَحْنُ أَوَّل النَّاس دُخُولًا الْجَنَّة بَيْدَ أَنَّهُمْ أُوتُوا الْكِتَاب مِنْ قَبْلنَا وَأُوتِينَاهُ مِنْ بَعْدهمْ فَهَدَانَا اللَّه لِمَا اِخْتَلَفُوا فِيهِ مِنْ الْحَقّ بِإِذْنِهِ فَهَذَا الْيَوْم الَّذِي اِخْتَلَفُوا فِيهِ فَهَدَانَا اللَّه لَهُ فَالنَّاس لَنَا فِيهِ تَبَع فَغَدًا لِلْيَهُودِ وَبَعْد غَد لِلنَّصَارَى)) البخاري, مسلم , مسند أحمد

 

“Sisi ni (Ummah) wa mwisho lakini ni wa kwanza siku ya Qiyaamah. Sisi ni wa kwanza kuingia Peponi ingawa wao (Mayahudi na Manaswara) walipewa Kitabu kabla yetu nasi tumepewa baada yao. Allaah Ametuongoza katika haki katika waliyokhitilafiana kwa idhini Yake. Hii ni siku (Ijumaa) waliyokhitilafiana, nasi Allah Ametuongoza nayo Hivyo watu wanatufuata kwani kesho (Jumamosi) ni siku ya Mayahudi na inayofuatia (Jumapili) ni ya Manaswara”. [Al-Bukhaariy, Muslim, Musnad Ahmad na wengineo]

 

 

Ibn Wahb amesema kwamba 'Abdur-Rahmaan bin Zayd bin Aslam amesema kuwa baba yake amesema kuhusu Aayah hii:

 

 فَهَدَى اللّهُ الَّذِينَ آمَنُواْ لِمَا اخْتَلَفُواْ فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِهِ

Allaah Akawaongoza wale walioamini kuendea haki katika yale waliyokhitilafiana, kwa idhini Yake. [Al-Baqarah: 213]

 

 

 

  • Wamekhitilafiana kuhusu siku ya Jamaa (Ijumaa); Mayahudi wamesema ni Jumamosi, Manaswara wamesema ni Jumapili, Allaah Akaongoza Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kufuata Ijumaa.

 

  • Wamekhitilafiana kuhusu Qiblah; Manaswara wameelekea Mashariki na Mayahudi wameelekea Baytul-Maqdis (Palestina), Allaah Akaongoza Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Qiblah sahihi (Ka'bah iliyoko Makkah).

 

 

  • Wamekhitilafiana kuhusu Swalah; wengine wanarukuu lakini hawasujudu, wengine wanasujudu lakini hawarukuu, wengine wanaswali huku wakizungumza na wengine huku wanatembea. Allaah Amewaongoza Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika haki.

 

  • Wamekhitilafiana pia katika kufunga (Swawm); wengine wanafunga sehemu tu ya siku, wengine wanafunga kujizuia tu baadhi ya vyakula (vingine wanakula). Allaah Ameongoza Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika haki.

 

  • Wamekhitilafiana pia kuhusu Nabii Ibraahiym; Mayahudi wamesema "Alikuwa ni Myahudi" na Wakristo wakidai ni Mnaswara. Allaah Amemfanya ni Haniyfam-Musliman (Muongofu Muislamu) Allaah Ameongoza Ummah wa Muhammad katika haki.

 

  • Wamekhitilafiana pia kuhusu Nabiy 'Iysaa; Mayahudi wamemkanusha na kumzulia mama yake kuwa kafanya madhambi makubwa (ya zinaa), Manaswara wamemfanya ni Allaah (Mungu) na mtoto wa mungu (Allaah). Allaah Amemfanya kwa maneno Yake ni roho kutoka Kwake (Kwa Alivyoviumba) Allaah Ameongoza Ummah wa Muhammad katika haki" 

 

 

 

Kisha (muelezeaji) akamalizia maelezo hayo kwa kusema 

بِإِذْنِهِ

 

Kwa idhini Yake (Allaah) 

 

kama ilivyoendeleza Aayah hiyo tukufu kuwa sisi Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tumeongozwa na Allaah kwa Idhini Yake).

 

 فَهَدَى اللّهُ الَّذِينَ آمَنُواْ لِمَا اخْتَلَفُواْ فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِهِ

 

Allaah Akawaongoza wale walioamini kuendea haki katika yale waliyokhitilafiana, kwa idhini Yake. [Al-Baqarah:213]

 

 

Na katika Hadiyth ifuatayo ambayo 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesimulia kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapoamka usiku akisoma du'aa kujikinga na mambo waliyokhitilafiana:

 

عَنْ أَبِي سَلَمَةَ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، قَالَ سَأَلْتُ عَائِشَةَ بِمَا كَانَ يَسْتَفْتِحُ النَّبِيُّ ـ صلى الله عليه وسلم ـ صَلاَتَهُ إِذَا قَامَ مِنَ اللَّيْلِ قَالَتْ كَانَ يَقُولُ ‏ "‏ اللَّهُمَّ رَبَّ جِبْرَئِيلَ وَمِيكَائِيلَ وَإِسْرَافِيلَ فَاطِرَ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ عَالِمَ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ أَنْتَ تَحْكُمُ بَيْنَ عِبَادِكَ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ اهْدِنِي لِمَا اخْتُلِفَ فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِكَ إِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ ‏" ‏.‏

Amesimulia Abu Salamah Bin ‘Abdir-Rahmaah (رضي الله عنه): Nilimuuliza ‘Aaishah (رضي الله عنها): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alianzia na nini katika Swalaah zake anapoamka usiku? Akasema: Alikuwa akisema:

 

اللَّهُمَّ رَبَّ جِبْرَئِيلَ وَمِيكَائِيلَ وَإِسْرَافِيلَ فَاطِرَ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ عَالِمَ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ أَنْتَ تَحْكُمُ بَيْنَ عِبَادِكَ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ اهْدِنِي لِمَا اخْتُلِفَ فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِكَ إِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ ‏"‏ ‏

 

Allaahuuma Rabba Jibraaiyl wa Miykaaiyl wa Israafiyl, Fatwiras-Samawaati wal-ardhw, 'Aalimal-Ghaybi wash-Shahaadah, Anta Tahkumu bayna 'Ibaadika fiymaa kaanuw fiyhi yakhtalifuwn. Ihdiniy lima-khtulifa fiyhi minal-haqq Bi-Idhnika, Innaka Tahdiy man Tashaau ilaa Swiraatwim Mustaqiym.

 

 

Ee Allaah Rabb wa Jibriyl na Mikaaiyl na Israafiyl, Muanzilishi wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa ghaibu na dhahiri, Wewe Utahukumu baina ya Waja Wako katika yale ambayo walikuwa wakikhitilafiana. Niongoze mimi kwenye haki katika yale waliyokhitilafiana kwa Idhini Yako. Hakika Wewe Unamhidi Umtakae kwenye Njia Iliyonyooka. [Muslim, An-Nasaaiy, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah]

 

 

Zaidi ya du'aa hiyo inatupasa pia tuombe du'aa ifuatayo daima ili tubakie katika haki,

 

 اللَّهُمَّ أَرِنَا الْحَقّ حَقًّا وَارْزُقْنَا اِتِّبَاعه وَأَرِنَا الْبَاطِل بَاطِلًا وَارْزُقْنَا اِجْتِنَابه وَلَا تَجْعَلهُ مُتَلَبِّسًا عَلَيْنَا فَنَضِلَّ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا

 

Allaahumma Arinal-Haqqa Haqqan War-Zuqnat-tibaa'ah. Wa Arinal-Baatwila baatwilan War-Zuqnaj-tinaabah. Wa laa taj'alhu mutalabbisan 'alaynaa Fanadhwilla Waj-'alnaa Lil-Muttaqiyna Imaama.

 

 

Ee Allaah, Tuonyeshe yale yaliyo haki, Uturuzuku tuweze kufuata na kutekeleza. Na Tuonyeshe yaliyo batili (maovu) na Utuongoze tujiepushe nayo. Usituchanganye (usitufunike tusiiujue) hakika ya uovu ili tusipotee kuufuata, na Tujaaliye tuwe viongozi wa Wamumini[Takhiryj Al-Ihyaaa 3: 1318]

 

 

 

 

Share