Masuala Kumi Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislam - 01
Masuala Kumi Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislaam – 01
Imefasiriwa na: Naaswir Haamid
Ndani ya makala hii, tutajaribu kusafisha masuala yanayoeleweka vibaya ambayo yamekithiri mno kuhusu Uislaam. Kabla ya kurukia kwenye orodha ya masuala hayo moja kwa moja, ni muhimu kueleza kwa ufupi kuhusu msingi mzuri wa chanzo cha Uislaam.
Uislaam ni jina la njia ya maisha ambayo Allaah Anatuhitaji tuifuate. Tunaepuka jina la dini kwa sababu ndani ya jamii nyingi zisizo kuwa za Kiislamu, kuna mgawanyo wa “dini na taifa”. Mgawanyo huu hautambuliki hata kidogo ndani ya Uislaam: Allaah Anashughulika zaidi kwa yale yote tunayoyafanya, ikiwemo siasa, jamii, uchumi, na nyanja nyenginezo za jamii yetu. Hivyo, Uislamu ni njia kamilifu ya maisha.
Chanzo cha Uislaam ni Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa), Allaah wa kila kitu vinavyotambulika na visivyotambulika kwetu. Yeye ni Mmoja, na Asiyefanana na kitu. Allaah Ametufundisha kuhusu Uislaam kwa njia mbili: Qur-aan na Sunnah. Zote mbili; Qur-aan na Sunnah zilifikishwa kwetu, binaadamu, kupitia kwa Rasuli wa Allaah: Muhammad bin Abdillaah, (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Rasuli wa Allaah hakuwa zaidi na sio pungufu kuliko Nabiy aliye na mwisho wa Allaah Asiye na mwisho.
Qur-aan ni kitabu chenye Neno hasa la Allaah. Ilikabidhiwa kutoka kwa Allaah kwa Malaika Wake (Jibriyl ‘Alayhis-salaam), na kutoka kwa Malaika huyo kwa Rasuli wa Allaah aliyeifikisha kwetu. Qur-aan inagusa mada pana za aina tofauti, zikiwemo ushahidi wa kushinikiza dai lake la kuwa ni Neno la Allaah, simulizi za vizazi vya mwanzo, kanuni ambazo mwanaadamu anatakiwa kuzifuata, na habari kuhusu Siku ya mwisho (Qiyaamah). Qur-aan inaonyesha kwamba inalindwa kubadilika na yeyote mwengine isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), na hili linathibitishwa kwa miaka yake 1442 ya kumbukumbu. Nakala za mwanzo na za mwisho zipo sawa sawa.
Sunnah ni msamiati unaotumika kueleza namna Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alivyoishi maisha yake. Maisha ya Nabiy ni mfano kwa Waislam wote, au wale waliokubali kuufuata Uislaam. Chochote alichofanya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kuzungumza au alichokikubali, ni chanzo cha Uislaam kama namna ilivyo kwa Qur-aan. Madaraka ya Nabiy hayachupi mpaka: maisha yake yalimilikiwa na kile Allaah Alichokitaka, na Nabiy hakuongeza au kupunguza kwenye Uislaam kwa yale matakwa yake binafsi. Maisha yake yalikuwa kama vile mkewe alivyomuita:
“Qur-aan inayotembea”.
Qur-aan na Sunnah ndio njia mbili pekee ambazo Allaah Ametufundisha moja kwa moja kuhusu Uislaam. Hili linatupeleka kwenye kanuni ya upambanuzi lakini iliyo nyepesi:
Kama mwanamme au mwanamke atajihusisha kwenye imani au tendo ambalo linapingana wazi wazi na Qur-aan au Sunnah, basi imani au tendo hilo haliwezi kutambulika kuwa ni la ‘Kiislam’.
Kanuni hii inatumika ikiwa ama mwanamme au mwanamke ni Muislam au asiye Muislam. Hivyo, hatuwezi kufananisha Uislaam na Waislamu. Uislaam ni njia ya maisha; Waislamu ni watu wanaodai kufuata njia hiyo ya maisha. Muislamu huenda akadai kufuata Uislaam, lakini akawa mkosa. Kwa mnasaba wa masuala yanayoeleweka vibaya, tunaweza kuielezea tena kanuni hiyo hapo juu kwa njia tofauti kidogo:
Baadhi ya masuala yanayoeleweka vibaya kuhusu Uislaam hakika yametokana na imani zisizo sahihi na matendo ya Waislam, na mengine hakika yametokana na athari ya kukosa elimu na uongo unaorudiwa kila mara 'stereotype' na wasiokuwa Waislam.
Masuala tofauti yanayoeleweka vibaya yanaorodheshwa chini. Badala ya kutaja masuala hayo kwa wepesi wa namna yalivyo wenyewe, pia tumehusisha ndani yake sababu za kwanini watu mara nyengine wanalichukua kuwa ni suala linaloeleweka vibaya. Hivyo, kila ingizo ndani ya orodha inapewa mtindo ufuatao:
Maelezo ya Suala Linaloeleweka Vibaya kwa sababu:
- hoja 1
- hoja 2
- n.k.
Baada ya kila suala linaloeleweka vibaya na sababu zake zinazoyumkinika, tunaonesha kwa ufupi kwa nini suala hilo ni la uongo kwa kuonesha kwamba yawezekana kuwa ni moja au zaidi ya mambo matatu yafuatayo:
1. Hoja ni ya uongo
2. Hoja haileti mantiki inayopelekea kueleweka vibaya
3. Habari ndogo ndogo zilizo kuu zimedharauliwa
Majibu yetu kwa masuala yanayoeleweka vibaya yamepatikana kutoka Qur-aan na Sunnah. Upatikanaji mwengine wowote hauna mnasaba: Uislaam ni njia ya maisha, ni msingi uliojikita kisawasawa kwenye kujiridhisha kiuwanazuoni, kujiridhisha huko kunaegemezwa katika maarifa.
Suala Nambari 1 Linaloeleweka Vibaya
Uislaam ni ‘dini ya amani’ kwa sababu
v
Neno la Kiarabu la Islaam linatokana na neno la Kiarabu ‘As-Salaam’ lenye maana ya amani.
Jibu
Inawezekana kukutana na mshangao kufikiria kwamba suala hili ni miongoni mwa yanayoeleweka vibaya, lakini ukweli ni hivyo. Mzizi wa neno Islaam ni “as-silm” lenye maana ya “kunyenyekea” au “kujisalimisha”. Linaeleweka kuwa na maana ya “kunyenyekea kwa Allaah”. Ingawa kwa azma kuu yeyote iliyosababisha Waislamu walio wengi kudai kwamba Uislaam kimsingi unatokana na amani, hili sio kweli. Allaah Anasema ndani ya Qur-aan (iliyotafsiriwa):
قُولُوا آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَمَا أُوتِيَ النَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿١٣٦﴾
Semeni: Tumemwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na Al-Asbaatw na aliyopewa Muwsaa na ‘Iysaa na waliyopewa Manabii kutoka kwa Rabb wao, hatutofautishi baina ya mmoja yeyote miongoni nasi ni Waislamu (tunajisalimisha) Kwake. [Al-Baqarah: 136]
Mzizi unaofuata baada ya hapo unawezekana kuwa ni “As-Salaam” (amani), hata hivyo maandiko ya Qur-aan yanadhihirisha wazi kwamba Allaah Ameshaazimia kwa uwazi shabaha ya maisha haya kuwa ni unyenyekevu Kwake Yeye. Hili linatufanya kuwa na unyenyekevu Kwake wakati wowote, ikiwa ni vipindi vya amani, vita, urahisi au ugumu.