05-Swabrun Jamiyl: Subira Katika Kuondokewa Na Vipenzi, Jamaa Wa Karibu
05 - Subira Katika Kuondokewa Na Vipenzi, Jamaa Wa Karibu
Hatima ya mwana Aadam ni kuiaga hii dunia kwa kuwa ni makazi ya muda na starehe ndogo tu kulingana na maisha ya milele Peponi na mazuri yake yaliyoahidiwa katika Qur-aan na Sunnah. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ ۗ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۖ فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ ۗ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ ﴿١٨٥﴾
Kila nafsi itaonja mauti. Na hakika mtalipwa kikamilifu ujira wenu Siku ya Qiyaamah. Basi atakayewekwa mbali na moto na akaingizwa Jannah kwa yakini amefuzu. Na uhai wa dunia si lolote ila ni starehe ya udanganyifu. [Aal-‘Imraan: 185]
La kutanabahi zaidi ni kwamba hakuna ajuaye wapi au lini mtu itamifikia siku na wakati wake wa kufariki. Hakuna yeyote aliyepewa ujuzi wake hata Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakutambulishwa. Na hili ni jambo miongoni mwa mambo matano ambayo Ametaja Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwamba ujuzi uko Kwake Pekee:
إِنَّ اللَّـهَ عِندَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ وَيُنَزِّلُ الْغَيْثَ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْأَرْحَامِ ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَّاذَا تَكْسِبُ غَدًا ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ بِأَيِّ أَرْضٍ تَمُوتُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ ﴿٣٤﴾
Hakika Allaah Ana elimu ya Saa na Anateremsha mvua na Anajua yale yaliyomo katika tumbo la uzazi na nafsi yoyote haijui nini itachuma kesho, na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani, hakika Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Luqmaan: 34]
Muumini akumbuke kwamba watoto, mke au mume, wazee, ndugu, jamaa wa karibu, marafiki ni amana kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na hizi amana tumepewa ili tuzichunge na ziwe ni utulivu wa nyoyo na viliwazo vya macho yetu. Amana hizi ni mtihani kwetu kutazamwa kama tutazichunga na kutekeleza kama tulivyoamrishwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Hivyo basi Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ana haki kuichukua amana Yake wakati wowote ule Alioupanga kumalizika muda wa kuchunga amana hiyo. Na Muumini asichukizwe na majaaliwa ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), bali anapoondokewa na kipenzi chake, aridhike kwa kushukuru na kuvumilia. Pia tumefunzwa kwamba mtu anapopatwa na msiba aombe du’aa ifuatayo ili Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amjaalie kilicho bora kuliko kilichomuondokea.
((إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ اللَّهُمَّ أْجُرْنِي فِي مُصِيبَتِي وَأَخْلِفْ لِي خَيْرًا مِنْهَا)) متفق عليه
Innaa liLLaahi wa-innaa Ilayhi raaji’uwn, Allaahumma Ajirniy fiy muswiybatiy wa-Akhlifliy khayram-minhaa
((Hakika sisi ni wa Allaah, na hakika sisi Kwake wenye kurejea, ee Allaah, Nilipe kwa msiba wangu na Nipe badala yake kilicho bora kuliko huo [msiba])) [Muslim]
Kadhaalika, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametufunza kumtaazi [kumhani] aliyepatwa na msiba kwa kumuombea:
((إِنَّ للهِ ما أَخَذ، وَلَهُ ما أَعْـطـى، وَكُـلُّ شَيءٍ عِنْـدَهُ بِأَجَلٍ مُسَـمَّى. فَلْتَصْـبِر وَلْتَحْـتسِبْ))
Inna liLLaahi maa Akhadha walahu maa a’twaa, wakullu shay-in ‘Indahu biajalim-musammaa, faltahtasib waltaswbir
((Kwa hakika ni cha Allaah Alichokichukua na ni Chake Alichokitoa, na kila kitu Kwake kina muda maalum, basi vumilia na taka malipo kwa Allaah)) [Al-Bukhaariy na Ahmad]
Naye Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipofiwa na kipenzi chake; mwanawe Ibraahiym akiwa ni mtoto mchanga, alihuzunika na kuvumilia subira njema:
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ (رضي الله عنه) قَالَ: دَخَلْنَا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى أَبِي سَيْفٍ الْقَيْنِ وَكَانَ ظِئْرًا لإِبْرَاهِيمَ فَأَخَذَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِبْرَاهِيمَ فَقَبَّلَهُ وَشَمَّهُ. ثُمَّ دَخَلْنَا عَلَيْهِ بَعْدَ ذَلِكَ وَإِبْرَاهِيمُ يَجُودُ بِنَفْسِهِ فَجَعَلَتْ عَيْنَا رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ تَذْرِفَانِ فَقَالَ لَهُ عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ عَوْفٍ (رضي الله عنه) وَأَنْتَ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ فَقَالَ: ((يَا ابْنَ عَوْفٍ إِنَّهَا رَحْمَةٌ)) ثُمَّ أَتْبَعَهَا بِأُخْرَى فَقَالَ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ الْعَيْنَ تَدْمَعُ, وَالْقَلْبَ يَحْزَنُ, ولاَ نَقُولُ إِلاَّ مَا يَرْضَى رَبُّنَا, وَإِنَّا بِفِرَاقِكَ يَا إِبْرَاهِيمُ لَمَحْزُونُونَ)) البخاري
Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: “Tulingia pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa sonara Abuu Sayfi na alikuwa mume wa mnyonyeshaji Ibraahiym [mtoto wa Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam]. Akamchukua na akambusu na kumnusa (kwa kumbusu). Kisha akaingia nyumbani kwa Abuu Sayf na wakati huo Ibraahiym alikuwa katika pumzi yake ya mwisho na macho ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yakaanza kutoa machozi. ‘Abdur-Rahmaan bin ‘Awf (Radhwiya Allaahu 'anhu) akasema: “Hata wewe unalia?” Akasema: ((Ee Ibn ‘Awf! Hii ni rahmah)) Kisha akalia zaidi na akasema: ((Macho yanatoa machozi na moyo unahuzunika lakini hatusemi isipokuwa yanayomidhisha Allaah. Ee Ibraahiym hakika tuna huzuni kwa kufarikiana nawe)) [Al-Bukhaariy]
Katika Hadiyth ifuatayo, tunapata mfano mzuri kabisa ya subira kuhusu kisa cha Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) na Abu Twalhah alipofariki mtoto wao ambaye alikuwa mwana pekee walioruzukiwa wakati huo:
عَنْ أَنَسِ (رضي الله عنه) قَالَ : كَانَ ابْنٌ لأَبِي طَلْحَةَ يَشْتَكِي ، فَخَرَجَ أَبُو طَلْحَةَ فَقُبِضَ الصَّبِيُّ ، فَلَمَّا رَجَعَ أَبُو طَلْحَةَ قَالَ : مَا فَعَلَ ابْنِي ؟، قَالَتْ أُمُّ سُلَيْمٍ وَهِيَ أُمُّ الصَبِيّ: هُوَ أَسْكَنُ مَا كَانَ، فَقَرَّبَتْ إِلَيْهِ الْعَشَاءَ فَتَعَشَّى، ثُمَّ أَصَابَ مِنْهَا، فَلَمَّا فَرَغَ قَالَتْ: وَارُوا الصَّبِيَّ، فَلَمَّا أَصْبَحَ أَبُو طَلْحَةَ أَتَى رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَأَخْبَرَهُ فَقَالَ: ((أَعْرَسْتُمُ اللَّيْلَةَ؟))، قَالَ : نَعَمْ، قَالَ : ((اللَّهُمَّ بَارِكْ لَهُمَا)). فَوَلَدَتْ غُلاَمًا، فَقَالَ لِي أَبُو طَلْحَةَ : احْمِلْهُ حَتَّى تَأْتِيَ بِهِ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَبَعَثَ مَعَهُ بِتَمَرَاتٍ فَقَال: ((أَمَعَهُ شَيْءٌ ؟)) قَالَ نَعَمْ: تَمَرَاتٌ، فَأَخَذَهَا النَّبِيُّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَمَضَغَهَا ثُمَّ أَخَذَ مِنْ فِيهِ فَجَعَلَهَا فِي فِي الصَّبِيِّ، ثُمَّ حَنَّكَهُ وَسَمَّاهُ عَبْدَاللَّهِ. متفق عليه .
وَفِي رِواية الْبُخاري: قَالَ ابن عُيَيْنَة: فَقَالَ رَجُلٌ مِنْ الأَنْصَارِ فَرَأَيْتُ لَهُمَا تِسْعَةَ أَولاَدٍ كُلُّهُمْ قَدْ قَرَأَ الْقُرْآنَ، يعني منْ أوْلاَدِ عَبْدُ الله الْمَوْلُود.
وَفِي رِوَايَة مسلم:
مَاتَ ابْنٌ لأَبِي طَلْحَةَ مِنْ أُمِّ سُلَيْمٍ فَقَالَتْ لإَهْلِهَا: لاَ تُحَدِّثُوا أَبَا طَلْحَةَ بِابْنِهِ حَتَّى أَكُونَ أَنَا أُحَدِّثُهُ. فَجَاءَ فَقَرَّبَتْ إِلَيْهِ عَشَاءً فَأَكَلَ وَشَرِبَ. ثُمَّ تَصَنَّعَتْ لَهُ أَحْسَنَ مَا كَانَتْ تَصَنَّعُ قَبْلَ ذَلِكَ. فَوَقَعَ بِهَ، فَلَمَّا أنْ رَأَتْ أَنَّهُ قَدْ شَبِعَ وَأَصَابَ مِنْهَا قَالَتْ: يَا أَبَا طَلْحَةَ! أَرَأَيْتَ لَوْ أَنَّ قَوْمًا أَعَارُوا عَارِيَتَهُمْ أَهْلَ بَيْتٍ فَطَلَبُوا عَارِيَتَهُمْ, أَلَهُمْ أَنْ يَمْنَعُوهَا؟ قَالاَ. فَقَالَتْ فَاحْتَسِبْ ابْنَكَ. قَالَ فَغَضِبَ ثُمَّ َقَالَ: تَرَكْتِنِي حَتَّى تَلَطَّخْتُ ثُمَّ أَخْبَرْتِنِي بِابْنِي؟ فَانْطَلَقَ حَتَّى أَتَى رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَأَخْبَرَهُ بِمَا كَانَ. فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((بَارَكَ اللَّهُ لَكُمَا فِي لَيْلَتِكُمَا)) قَالَ: فَحَمَلَتْ قَالَ: فَكَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي سَفَرٍ وَهِيَ مَعَهُ وَكَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا أَتَى الْمَدِينَةَ مِنْ سَفَرٍ لاَ يَطْرُقُهَا طُرُوقًا فَدَنَوْا مِنْ الْمَدِينَةِ, فَضَرَبَهَا الْمَخَاضُ فَاحْتُبِسَ عَلَيْهَا أَبُو طَلْحَةَ، وَانْطَلَقَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: يَقُولُ أَبُو طَلْحَةَ إِنَّكَ لَتَعْلَمُ يَا رَبِّ إِنَّهُ يُعْجِبُنِي أَنْ أَخْرُجَ مَعَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا خَرَجَ، وَأَدْخُلَ مَعَهُ إِذَا دَخَلَ، وَقَدْ احْتَبَسْتُ بِمَا تَرَى. تَقُولُ أُمُّ سُلَيْمٍ: يَا أَبَا طَلْحَةَ مَا أَجِدُ الَّذِي كُنْتُ أَجِدُ، انْطَلِقْ فَانْطَلَقْنَا، وَضَرَبَهَا الْمَخَاضُ حِينَ قَدِمَا فَوَلَدَتْ غُلاَمًا. فَقَالَتْ لِي أُمِّي يَا أَنَسُ لاَ يُرْضِعُهُ أَحَدٌ تَغْدُوَ بِهِ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَلَمَّا أَصْبَحَ احْتَمَلْتُهُ فَانْطَلَقْتُ بِهِ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ. وَذَكَرَ تَمَامَ الْحَدِيث
Kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Alikuwa mtoto wa Abuu Twalhah akiugua. Abuu Twalhah akasafiri. Mtoto akafariki. Abuu Twalhah aliporudi aliuliza: “Vipi hali ya mwanangu?” Ummu Sulaym - mama wa mtoto - akamwambia: “Ametulia zaidi ya alivyokuwa”. Akampelekea chakula cha jioni akala, kisha akalala na mkewe [wajakamiiana]. Alipomaliza, Ummu Sulaym akamwambia: “Kamzikeni mtoto”. Abuu Twalhah alipopambaukiwa, alimwendea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwelezea yaliyotokea. Akamwuliza: ”Je, usiku mlifanya harusi (mlijamiiana)?” Akamjibu: “Ndio”. Akaomba: ((Ee Allaah! Wabarikie)). Akazaa mvulana. Abuu Twalhah akaniambia: “Mbebe umpeleke kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)”. Akapeleka na tende kadhaa. Akauliza: ((Ana kitu?)) Akajibu: “Ndio, tende kadhaa” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akazichukua akazitafuna kisha akachukua zile tende zilokuwa mdomoni mwake akazitia katika kinywa cha mtoto, halafu akamsugulia nazo (ili mtoto afyonze na kumeza) na akampa jina la ‘Abdullaah” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Katika riwaayah nyingine ya Al-Bukhaariy: “Ibnu ‘Uyaynah amesema: “Mtu mmoja katika Answaar alisema: “Nikawaona watoto tisa wamehifadhi Qur-aan” Yaani watoto wa ‘Abdullaah huyu aliyezaliwa”
Na katika riwaayah nyingine ya Muslim imesema: “Abuu Twalhah alifiwa na mtoto aliezaa naye kwa Ummu Sulaym. Ummu Sulaym akawaambia jamaa zake: “Msimweleze Abuu Twalhah mpaka mimi niwe ndiye nitakayemweleza” Alivyorudi, akampelekea chakula cha jioni, akala na akanywa, halafu akajipamba kuliko anavyojipamba siku zote. Akamjamii. Ummu Sulaym alipoona kuwa Abuu Twalhah ameshiba na amemjamii alimwambia: “Ee Abuu Twalhah! Niambie lau watu wameazima kitu kwa watu fulani kisha wao wakataka kitu chao kilichoazimwa je, walioazima wana haki ya kuwanyima?” Akajibu: “Hapana!” Akamwambia: “Basi taraji thawabu kwa msiba wa mwanao”. Abuu Twalhah akakasirika na akasema: “Umeniacha mpaka nimejichafua [kwa jimai] halafu ndio unaniambia habari ya mwanangu?” Akaenda kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamweleza mambo yalivyokuwa. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akawaombea: ((Allaah Awabarikie katika usiku wenu)). Ummu Sulaym akabeba mimba. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa yumo safarini, naye [Ummu Sulaym] yuko naye. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapoingia Madiynah kutoka safari alikuwa haiingii usiku. Wakakaribia Madiynah. Ummu Sulaym akaanza kusikia uchungu wa uzazi. Abuu Twalhah akabaki nyuma. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaendelea na safari. Abuu Twalhah akasema: “Ee Allaah! Hakika Unajua kwamba mimi hufurahishwa kusafiri pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anaposafiri, na hupenda kurudi naye anaporudi, na nimezuilika kama Uonavyo”. Ummu Sulaym akasema: “Ee Abuu Twalhah! Sisikii tena uchungu niliousikia, tuondoke!” Tukaondoka. Akapatwa na uchungu wa kuzaa walipokuwa wameshaingia Madiynah. Akajifungua mvulana. Mama yangu akaniambia: ‘Ee Anas, asinyonyeshwe na yeyote mpaka uende naye kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)”. Kulipopambazuka, nilimbeba nikaenda naye kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)…” Akaendela mpaka mwisho wa Hadiyth.
Tunapata pia mafunzo kutoka katika kisa cha Ummu Salamah alipofiwa na mumewe na baada ya kuomba du’aa alivyomfunza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaolewa naye (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
عَنْ أُمِّ سَلَمَةَ (رَضِيَ الله عَنْهَا) قَالَتْ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ: ((مَا مِنْ مُسْلِمٍ تُصِيبُهُ مُصِيبَةٌ فَيَقُولُ مَا أَمَرَهُ اللَّهُ، إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ، اللَّهُمَّ أْجُرْنِي فِي مُصِيبَتِي وَأَخْلِفْ لِي خَيْرًا مِنْهَا، إلاَّ أَخْلَفَ اللَّهُ لَهُ خَيْرًا مِنْهَا)) قَالَتْ: فَلَمَّا مَاتَ أَبُو سَلَمَةَ قُلْتُ أَيُّ الْمُسْلِمِينَ خَيْرٌ مِنْ أَبِي سَلَمَة أَوَّلُ بَيْتٍ هَاجَرَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم). ثُمَّ إِنِّي قُلْتُهَا فَأَخْلَفَ اللَّهُ لِي رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ). قَالَتْ: أَرْسَلَ إِلَيَّ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) حَاطِبَ بْنَ أَبِي بَلْتَعَةَ يَخْطُبُنِي لَهُ. فَقُلْتُ: إِنَّ لِي بِنْتًا وَأَنَا غَيُورٌ فَقَالَ: ((أَمَّا ابْنَتُهَا فَنَدْعُو اللَّهَ أَنْ يُغْنِيَهَا عَنْهَا وَأَدْعُو اللَّهَ أَنْ يَذْهَبَ بِالْغَيْرَةِ)) مسلم
Kutoka kwa Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amesema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Hakuna Muislamu anayefikwa na msiba akasema Alivyoamrishwa na Allaah: ‘Innaa liLLaahi wa innaa Ilayhi raaji’uwn, Allaahumma Ajirniy fiy muswiybatiy wa-Akhlif-liy khayram-minhaa’ [Hakika sisi ni wa Allaah, na hakika sisi Kwake wenye kurejea, ee Allaah, nilipe kwa msiba wangu na nipe badala yake kilicho bora kuliko huo [msiba)]’, hakuna ila Allaah Atampa kilicho bora kuliko [msiba] huo)). Abuu Salamah alipofariki akasema: Muislamu gani ni bora kuliko Abuu Salamah ambaye familia yake ilikuwa ya kwanza kuhama Hijrah kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)? Kisha nikaisema [du’aa hiyo] na Allaah Akanipa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) badala yake. Akasema: Rasuli wa Allaah, akamtuma Abuu Balta’ah anipose kwake nikasema: Mimi nina binti [anayenitegemea] nami nina tabia ya wivu. Akasema: ((Ama kuhusu binti yake tutamwomba Allaah Amtajirishe kwake [asiwe na jukumu naye], na namuomba Allaah Amuondoshee tabia ya wivu na hamaki)) [Muslim]
Hadiyth zifuatazo pia zinatupa fadhila za mwenye kusubiri baada ya kufiwa na ahli wake:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ : ((يَقُولُ اللَّهُ تَعَالَى: مَا لِعَبْدِي الْمُؤْمِنِ عِنْدِي جَزَاءٌ، إِذَا قَبَضْتُ صَفِيَّهُ مِنْ أَهْلِ الدُّنْيَا، ثُمَّ احْتَسَبَهُ إِلاَّ الْجَنَّةُ)) البخاري
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Ta’aalaa amesema: Mja Wangu Muumini hana jazaa Nitakapomchukulia mpenzi wake katika watu wa dunia kisha akatarajia thawabu isipokuwa [atapata] Jannah)) [Al-Bukhaariy]
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ (رضي الله عنه) قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : ((مَا مِنَ النَّاسِ مُسْلِمٌ يَمُوتُ لَهُ ثَلاَثَةٌ مِنَ الْوَلَدِ لَمْ يَبْلُغُوا الْحِنْثَ، إِلاَّ أَدْخَلَهُ اللَّهُ الْجَنَّةَ بِفَضْلِ رَحْمَتِهِ إِيَّاهُمْ)) البخاري
Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Muislamu yeyote atakayefiwa na watoto watatu wasiofikia umri wa kubaleghe, Allaah Atamuingiza Jannah kutokana na fadhila ya rahmah Yake kwao)) [Al-Bukhaariy]
وعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ : ((لاَ يَمُوتُ لأَحَدٍ مِنَ الْمُسْلِمِينَ ثَلاَثَةٌ مِنَ الْوَلَدِ فَتَمَسَّهُ النَّارُ إلاَّ تَحِلَّةَ الْقَسَمِ)) مسلم
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Watoto watatu wakifariki wa Muislamu yeyote, moto hautamgusa isipokuwa kitimizwe kiapo)) [Muslim]
[kiapo cha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika Suwrat Maryam Aayah: 71]
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ لِنِسْوَةٍ مِنَ الْأَنْصَارِ: ((لاَ يَمُوتُ لِإِحْدَاكُنَّ ثَلاَثَةٌ مِنَ الْوَلَدِ فَتَحْتَسِبَهُ إِلاَّ دَخَلَتِ الْجَنَّةَ)) فَقَالَتِ امْرَأَةٌ مِنْهُنَّ : أَوِ اثْنَيْنِ يَا رَسُولَ اللَّهِ قَالَ: ((أَوِ اثْنَيْنِ)) متفق عليه
Kutoka kwa Abuu Huraryah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amewaambia wanawake wa Answaar: ((Yeyote miongoni mwenu atakayefiwa na watoto watatu akataraji [malipo], ataingia Jannah)) Akasema mmoja wa wanawake miongoni mwao: “Au hata wawili ee Rasuli wa Allaah?” Akasema ((Au hata wawili)) [Al-Bukhaariy, Muslim]
Anayemshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika kifo cha mpenzi wake hujengewa nyumba Peponi inayoitwa Baytul-Hamd:
عَنْ أَبِي مُوسَى الأَشْعَرِيِّ (رضي الله عنه) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((إِذَا مَاتَ وَلَدُ الْعَبْدِ قَالَ اللَّهُ لِملاَئِكَتِهِ: قَبَضْتُمْ وَلَدَ عَبْدِي ، فَيَقُولُونَ: نَعَمْ. فَيَقُولُ: قَبَضْتُمْ ثَمَرَةَ فُؤَادِهِ. فَيَقُولُونَ نَعَمْ. فَيَقُولُ مَاذَا قَالَ عَبْدِي؟ فَيَقُولُونَ: حَمِدَكَ وَاسْتَرْجَعَ. فَيَقُولُ اللَّهُ: ابْنُوا لِعَبْدِي بَيْتًا فِي الْجَنَّةِ وَسَمُّوهُ بَيْتَ الْحَمْدِ))
Kutoka kwa Abuu Muwsa Al-Ash’ariyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Anapofariki mtoto wa mja, Allaah Huwaambia Malaika: Mmechukua roho ya mwana wa mja Wangu? [Malaika] Husema: Ndio! Kisha Husema: Mmechukua tunda la moyo wake! Husema: Ndio. Kisha Husema: Amesema nini mja Wangu? Husema: Amekusifu na amesema kauli ya istirjaa’. Allaah Husema: Mjengeeni mja Wangu nyumba Jannah na iiteni ‘Baytul-Hamd’ [Nyumba ya Shukurani])) [Ahmad, At-Tirmidhiy na ameipa daraja Swahiyh Al-Albaaniy]
Istirjaa’ ni kusema [Innaa liLLaahi wa innaa Ilayhi raaji’uwn]
Basi uzuri ulioje wa fadhila na malipo mema kabisa kutoka kwa Rabb Mtukufu ambaye Haendi kinyume na ahadi Zake.
Mauti ni haki na hapana budi ila kuyakabili kwani dunia ni nyumba ya kupita na Aakhirah ndiko kwenye makazi ya kudumu milele. Bali dunia ni kama shamba la kufanyiwa juhudi kupandikiza mazuri na Aakhirah ndiko kwenye mavuno yake. Na duniani hakuna amana, hugeuka baina ya kheri na shari, baina ya dhiki na furaha, baina ya siha na afya baina ya utajiri na umaskini, hata mtu awe tajiri vipi bila shaka atakumbana na shari au dhiki fulani. Ama Aakhirah tumeahidiwa neema nyingi nzuri kabisa ambazo macho hayajapatapo kuona, wala masikio kusikia, wala kufikiria katika akili ya mwana Aadam. Na huko tumeahidiwa kukutana na vipenzi vyetu waliokuwa na msimamo wa Dini. Na pia kukutana na kipenzi chetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Manabii, na Maswiddiqiyn na Mashuhadaa, na waja wema wengineo. Na madamu hali ni hivyo, basi hakuna khiari ila kuvumilia na kuwa miongoni mwa waliosifiwa kuwa ni wenye kuvuta subira.
Kwa hiyo Muumini awe na matarajio ya kuipata Jannah yenye neema tele na kuokoka na moto. Na hilo litathibitika kwa subira kwani ndio ngazi ya kuifikia.