Maji Yanayodondokea Nguo Wakati Anapokwenda Msalani Yanatengua Wudhu? Na Nguo Inanajisika?

SWALI:

 

ASALAM ALEHKUM

 

POLENI NA KAZI, NA MWENYEZI MUNGU ATA WAJAALIA NGUVU ZAIDI ILI MUWEZE KUTUSAIDIA SISI.

SWALI YANGU KAMA IFUATAVYO. JE NIKIENDA KUJISAIDIA CHOONI ALAFU NIKASTANCHI KWA MAJI NIKA RUDIA KUVAA NGUO YA NDANI NIKASWALI ALAFU BAADAE NIKIENDA CHOONI TENA NASTANJI. JE YALE MAJI YATAKAYO DONDOKEA KWENYE NGUO YANGU YA NDANI YATANITENGUA UDHU NA NGUO ITAKUWA AIFAI KUSWALIA.


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu maji yenye kudondokea nguo ya ndani wakati wa kustanji.

Inavyotakiwa kwa Muislamu kufanya ni kuhakikisha kuwa mkojo wote umemalizika wakati wa kustanji. Maadamu mkojo haudondoki na umekwisha, baada ya kujisafisha yale maji uliyojisafishia hayakutengui wudhuu wako.

 

Soma zaidi masuala ya Fiqh ndani ya kiungo hiki:

 

Swahiyh Fiqhus Sunnah

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share