Kuna Watu Bado Wenye Uhusiano Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Hata Kama Wa Mbali?

SWALI:

 

ASSALAM ALEYKUM. KILA SIFA NJEMA ANASTAHIKI MOLA WA VIUMBE VYOTE ALLAH TABARA WATAALA. HIVI KATIKA ULE UKOO WA MTUME MUHAMMAD SWALALAHU ALEY WASALIM. BADO KUNA CHEMBE YA MTU AMBAYE ANA JINASIBISHA NA ULE UKOO YANI ANA UNDUGU NA MTUME HATA KAMA WA MBALI?

 


 

 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu kuwepo kwa watu wenye unasaba na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Ndio wapo wataendelea kuwepo kwani hilo ndilo alituarifu kwayo Mtume mwenyewe (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametueleza kuwa katika mwisho wa zama kabla ya Qiyaamah atakuja Mahdi anayetarajiwa kutoka katika kizazi chake. Hivyo, kizazi chake kipo na kitaendelea kuwepo.

 

 

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo kamili:

 

 

Ufafanuzi Wa Ahlul Bayt (Masharifu) Na Kizazi Chake

 

Vizazi Vya Mtume Vipo Bado Na Je Ni Kweli Kuwa Hawatawakiwi Kupokea Sadaka?

 

Usharifu Nini Maana Yake? Je Ukoo Wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Uko Kweli?

 

Kizazi Cha Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) Bado Kinaendelea?

 

Masharifu Wasioswali Wana Maovu Na Maasi Watukuzwe? Je, Wao Bora Kuliko Mja Anayefuata Sheria?

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share