Maajabu Matano Ya Dunia

Maajabu Matano Ya Dunia

 www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Asalaam  Alaikum  Warahmatulhaahi  Wabarakaatuhu,  mimi  sijambo [ Al Hamdulillaah] kama  nanyi  hamjambo viongozi  wetu wa Dini  ya kweli basi ni kheri. Naomba msaada mnijibu.

 Maajabu matano ya Dunia.

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Vitu ambavyo vinajulikana kuwa ni maajabu ya dunia ni saba kwa mujibu wa wataalamu wasiokuwa Waislamu.

 

Maajabu yote haya ni katika majengo yaliyotengenezwa na watu katika zama tofauti. Orodha hii ambayo tunaiandika, wametofautiana sana watu kwayo kwani vigezo ambavyo vinatumika havieleweki na hata na wenyewe walioviweka, hivyo kila kikundi au mtu ana orodha yake kulingana na muono wao/wake. Vile vinavyojulikana ni kama vifuatavyo:

 

 

1. The Great Pyramid ya Giza aliyozikwa Mfalme Khufu.

2. The Hanging Gardens ya Babeli (Babilon) huko Iraq, yaliyotengenezwa na Mfalme Nebuchadnezzar II.

3 . The Statue (sanamu) ya Zeus huko Olympia, Greece.

4. The Temple (Hekalu) la Artemis huko Ephesus.

5.The Mausoleum (kaburi lililojengewa) la Mfalme Maussollos wa Ufursi (Iran) huko Halicarnassus.

6.  The Collossus huko Rhodes, bandari ya Wayunani katika kisiwa cha Mediterenia.

7. The Lighthouse (Nyumba ya mwangaza) huko Alexandria.

 

 

Wengine wamesema Taj Mahal ambayo ipo Agra huko India ni miongoni mwa maajabu ya dunia.

 

Ukiangalia vitu vyote hivi vinavyosemekana ni maajabu havina asili yoyote na Uislamu wala Waislamu, hivyo ni jambo ambalo hatufai kujishughulisha nalo na kupoteza wakati mwingi.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share