Mwanamke Anayo Haki Ya Kuwatii Wazee Wake Kudai Talaka Kwa Mumewe Ambaye Wamekaa Miaka Kumi Bila Kupata Kizazi?
SWALI:
Assalam Alaykum WarahmatuhLwah Wabarakatuh, Ni wajibu wangu kutoa shukrani kwenu za dhati kwa kazi yenu nzuri ya kuipeleka mbele dini ya Allwah Subhana HuwaTaala malipo yenu yawe pepo juu ya
Suala langu ni kuwa je mwanamke anayo haki ya kuwatii wazee wake juu ya kudai Talaka kwa mumewe ambae wamekaa kipindi kikubwa kiasi cha miaka kumi 10 hawajapata kizazi?
Ikiwa ndio au hapana kuna dalili yoyote kutoka katika Qur-an au Sunnah za Bwana Mtume Salalwah Alayhim musaalaam. Natarajia kupata mashirikiana na jawabu zuri kutoka kwenu.
Maasaalaam
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani kwa swali lako kuhusu mwanamke kuomba talaka kutoka kwa mume asiyezaa.
Hakika katika
Thawbaan (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Mwanamke yeyote mwenye kumuomba mumewe talaka bila ya sababu yenye nguvu, basi harufu ya Peponi ni haramu kwake” (Abu Daawuud).
Mambo ya kufanya ni yafuatayo ili kutatua tatizo
1. Wanandoa wende kupimwa kwa daktari na kutazamwa tatizo lililopo.
2. Ikiwa ni mume au mke basi wawe ni wenye kufanya dawa kwani inaweza kuwa ni ugonjwa na hakuna ugonjwa ila una dawa.
3. Wanandoa wamuombe
Na Insha Allaah Allaah Atawapatia mtoto wa kheri bila ya kuachana. Na hata
Na Allaah Anajua zaidi