07-Wasiya Wa Mwisho Wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Si Ruhusa Kutegemea Qur-aan Pekee Na Kuacha Sunnah
Si Ruhusa Kutegemea Qur-aan Pekee Na Kuacha Sunnah
Ni kosa kubwa kabisa kufuata Qur-aan peke yake bila kufuata Sunnah. Tunaona madhehebu nyingi zilizo kengeuka zinadai kufuata Qur-aan, madhehebu ambazo zinategemea zaidi upotoshaji na kudhihirisha ufafanuzi usio sahihi.
Je, Swalah, Zakaah au Hajj vimeelezewa kwa urefu ndani ya Qur-aan? (kwa hakika jibu ni hapana); kwa hiyo lazima tuelewe Qur-aan kwa kupitia mwanga wa Sunnah ya Mtume [1].
Muislamu lazima atambue ya kuwa maamrisho na makatazo ya mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni lazima kufuatwa, kama ilivyo maamrisho na makatazo ya Allaah ni lazima kufuatwa.
“Al-Muqdam Bin Ma’ad Yakrib (Radhiya Allaahu ‘anhu) alisimulia ya kuwa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema,
“Ina yumkinika ya kuwa Hadiyth inamfikia mtu kutoka kwangu wakati anaegemea Arikah yake (mto au godoro au kochi) na akasema, “Kati yetu na nyie ni Kitabu cha Allaah; chochote tutakacho kikuta ni halali, tutakichukulia kuwa ni halali – Na chochote tutakacho kikuta kuwa haramu, tutakifanya haramu kwa hakika alichokikataza Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni sawa na Alichokataza Allaah,”[2]
Hii inatukumbusha mdahalo uliofanyika kati ya ‘Abdullaah Bin Mas’ud (Radhiya Allaahu ‘anhu) na Ummu Ya’aquub.
‘Alqamah alisimulia, ‘Abdullaah alimlaani Al-Waashimah– (wale wanaochoma miili/ngozi zao kwa sindano (tattoo), na sehemu ile wakatia ‘kohl’ au rangi ya buluu ili kuifanya ngozi ionekane buluu au kijani), al-Mutanammiswaat (wale wanaowataka wenzao waondoe au kunyoa nywele katika nyuso zao [nyusi]) na al-Mutafallijaat (wale wanaomtaka mtu atengeneze mwanya kati ya meno yao mawili ya mbele au kufanya wenyewe), wanaofanya kwa urembo, kubadilisha maumbile ya Allaah. Ummu Ya’aquub alisema, “Nini hiki? ‘Abdullaah alijibu, “Kwa nini nisimlaani yule aliyelaaniwa na Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na yule aliyelaaniwa ndani ya Kitabu cha Allaah! (Ummu Ya’aquub) Alisema, “WAllaah nimesoma yaliyoandikwa (yaani, mbele na nyuma ya Qur-aan (mwanzo hadi mwisho)) na sijayaona hayo.” Yeye (‘Abdullaah bin Mas’uud) akasema, “WaLlaahi, kama umesoma, ungelikuta hili.
“Na anachokupeni Mtume chukueni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho. ….” (59: 7).
Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwalaani watu tuliowataja hapo juu; Mola wetu (Subhaanahu wa Ta’ala) Alituamrisha tumfuate Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa hiyo anachotupa tukipokee; anachotukataza, tujiweke mbali nacho, na yeyote anayemlaani, tumlaani. Kwa hiyo chimbuko la wale watu chimbuko lake ni Kitabu cha Allaah.
Tunajifunza ya kuwa kufuata amri za Mtume ni kufuata amri za Qur-aan, ambapo kujiweka mbali na mambo aliyoyakataza ina maana kujiweka mbali na mambo yaliyokatazwa na Qur-aan. Chochote alichokataza Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kina uzito sawa na Alichokataza Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na alichoruhusu Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kina uzito sawa na Alichoruhusu Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Na kwa ajili hiyo hatutakiwa kutofautisha kati ya Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume.
[1] Shaykh wetu –Al-Albaaniy (Allaah Amuwie radhi) – aliandika makala muhimu kuhusu mada inayoitwa, “Manzilat as–Sunnah Fil-Islaam Wa-bayaan Annahu La Yastaghna ‘Anha bil–Qur-aan.”
[2] Ilisimuliwa na At-Tirmidhiy na imo katika, Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy, na Ibn Majaah, Swahiyh ibni Maajah, (12) pia Ad-Daarimiy na wengineo.