10-Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: Sura Ya Nane: Hadhi Na Cheo Chake

 

10- Shaykh Al-Islam Ibn Taymiyyah: SURA YA Nane: Hadhi Na Cheo Chake

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Mhuishaji[1]

 

Shaykh al-Islaam alikuwa ni katika mstari wa mbele miongoni mwa wahuishaji (Dini) wa kipindi hichi. Kwa sababu changamoto zake kwa wakati ule, watu waliokuwa wakimchukia katika zama zake walimtuhumu kuwa ni murtadi na watawala wakamtupa jela mara kadhaa.

 

Hata hivyo, Ibn Taymiyyah alikuwa ni Mwanachuoni mkubwa kwa wakati wake. Kiundani ni kwamba amesoma Fiqh kwa mujibu wa madhehebu ya Hanbali lakini hakujifunga nayo.

 

Alisoma vyanzo vya Shar’iah ya Kiislamu kwa undani wake na kuwa mtaalamu wa sayansi ya Kiislamu ambayo ikijulikana kwa enzi zile. Zaidi ya hayo, alipitia maandiko ya madhehebu mbalimbali ambayo yamepotea kutoka kwenye Uislamu, alisoma vitabu vya dini ya Kikiristo, Kiyahudi na madhehebu mbalimbali na aliandika kwa upana uchambuzi wake katika hayo yote.

 

Ibn Taymiyyah pia alichukua nafasi yake katika Jihaad dhidi ya Wamongoli ambao waliiteka sehemu za mashariki na kaskazini mwa dola la Abbasiyyah na kwa wakati ule walikuwa ni tishio kwa Misri na Afrika Kaskazini.

 

Wanafunzi wa Ibn Taymiyyah walikuwa miongoni mwa Wanachuoni wakubwa wa Kiislamu kwa wakati wao na walibeba kwa kizazi kinachofuata mabango (elimu) ya Ijtihaad na kuwarudisha katika vyanzo safi vya Uislamu alivyovinyanyua yeye. Miongoni mwao ni Ibn al-Qayyim, Mwanachuoni mkubwa katika nyanja za Fiqh na Hadiyth, adh-Dhahabiy, mtaalamu katika uchambuzi wa Hadiyth na Ibn Kathiyr, mtaalamu wa Tafsiyr, Taariykh na Hadiyth.

 

Allaah Alimfanya Yeye Kuwa Ni Mtu Wa Daraja Ya Juu Na Mpambanuzi Wa Ukweli Na Uongo[2]

 

Hili ni jambo ambalo pia likijulikana. Yeye (Allaah Amrehemu) hakuwa na kitabu hata kimoja au fatwa isipokuwa kwamba alichagua ndani yake maandiko mazito na ushahidi yakinifu juu ya yote, na akaingiza pia neno la ukweli pamoja na ushahidi mwingi wa wazi na ushahidi ambao yeyote atakayezipitia akiwa na dhana safi, moyo wake utakuwa ubaridi kwa hoja na dalili hizo na hatimaye utafungika kwamba ni ukweli usio na shaka. Katika maandiko yake yote unaona kwamba iwapo Hadiyth ni sahihi, moja kwa moja anaichukua na anaifanyia kazi, na kuiweka mbele juu ya maoni ya Mwanachuoni au Mujtahid yeyote.

 

Mfuatiliaji asiyefungamana na upande wowote atagundua kwamba maneno yake yalikuwa yanaenda kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah, na wala haendi kinyume na maneno yake kwa maneno ya mtu mwengine, hata ikiwa kwamba mtu huyo awe vipi, na wala hakuwa na hofu ya mtawala, mamlaka, mijeledi, au upanga kwa kufanya hivi, na wala hatayatupa (maneno yake) kwa maoni ya mtu mwengine yeyote. Alikamatana vyema kabisa kwa mshiko wa kisawasawa, akiifanyia kazi Maneno Yake Mtukufu:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا ﴿٥٩﴾

 

Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Rasuli na wenye madaraka katika nyinyi. Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli mkiwa mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri zaidi. [An-Nisaa: 59]

 

Na: 

 

وَمَا اخْتَلَفْتُمْ فِيهِ مِن شَيْءٍ فَحُكْمُهُ إِلَى اللَّـهِ ۚ ﴿١٠﴾

 Na katika lolote lile mlilokhitilafiana, basi hukumu yake ni kwa Allaah. [Ash-Shuwraa: 10]

 

Sikupatapo kusikia mtu yeyote aliyejulikana kama alivyo yeye katika umakini wa hali ya juu wa kufuata Qur-aan na Sunnah, jitihada zake katika kuzichambua maana zake, na matendo yake yaliegemea katika amri zake. Hakupatapo kupitia jambo ambalo Wanachuoni hapo kabla wametoa hukumu isipokuwa yeye akichagua iliyo na nguvu na iliyo karibu na Qur-aan na Sunnah kutokana nazo. Allaah Alimbariki kwa sifa hii, na Akamfanya kuwa ni mtu mwenye amri kwa watu wa enzi zake.

 

Hii ilifikia hali hadi kwamba watu wanaotoka sehemu za mbali kumtumia kwake yeye kwa fataawa kuhusiana na hali zao, na huwa wakimuuliza awasaidie kuondosha utata wao waliokuwa nao kuhusiana na hili na lile. Hivyo, huwatuliza nyoyo zao kwa majibu yenye kutosheleza, yanayoshikika, na mara zote huegemeza msimamo wake kwa uthibitisho ulio wazi kutoka kwa maelezo halali ya Wanachuoni, hadi kwamba mtu yeyote mwenye uoni, elimu, na hayaa aliyeacha utashi wake na kukutana nazo huzikubali, na ukweli huwa wazi kwao.

 

Iwapo mtu atasikika kumpinga au kuvamia heshima yake, mara zote hutokezea kuwa hao ni watu wanaotambulikana na watu wengi kuwa ni watendaji maovu, na yeyote anayependa kuthibitisha haya ninayosema, mwache aangalie kwa jicho la uoni, kwani hatoona Mwanachuoni kutoka ardhi yoyote anayemfuata Imaam huyu na kutambua sifa na uongozi aliotunukiwa na Allaah, na humsifu kwa kila mkusanyiko isipokuwa kwamba katika nyuma ya kila Mwanachuoni wao ni wafuasi wakorofi wa Qur-aan na Sunnah, na wenye kushughulishwa (na dunia) katika kuitafuta Akhera na (ingawa) ni wenye kuitaka, na wao ni wenye kuwepo mbali kutokana na ukwepaji au kuwa na ujinga nayo.

 

Vivyo hivyo, hutopata kuona Mwanachuoni hata mmoja akimpinga yeye na kuchukuliwa kwa uadui isipokuwa kwamba ni mwenye bidii miongoni mwao katika kuzitafuta lahwa za dunia, na ni wa juu wao katika kujionesha na kutafuta sifa, na ni wa mwisho wa ustaarabu katika tabia njema, mwenye kushirikiana na wanyanyasaji katika majaribio yao, na mwenye pupa miongoni mwao kusema uongo. Ukiangalia wale waliokuwa wakimpenda na wale wasiompenda kuanzia kwa asiyejua (hata) kusoma, utaona wao kwamba kuwa ni waadilifu kama vile nilivyoyaelezea hayo makundi mawili ya Wanachuoni hapo juu. Nimejaribu kuonesha na kufikiria kwa yale niliyosema hapo juu, na nimegundua kwamba ni haswa kabisa kama nilivyoeleza.

 

Naapa kwa Allaah, sitoacha mbele ya yeyote kuzungumza haya, na yeyote mwenye shaka kwa ninayosema, basi na ajifikirie yeye mwenyewe na ataona kwamba yale ninayosema iwapo atajiondolea ufuniko wa shahawa zake. Hii si kesi isipokuwa kwa sababu Allaah Ametambua usafi makini wa Imaam huyu, na ukweli na kujitolea kwake katika kutafuta Ridhaa za Rabb wake na kuifuata Sunnah ya Nabiy Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).[3]

 

 

Hadhi Yake Miongoni mwa Wanachuoni wa Enzi Zake

 

Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah (Allaah Amrehemu) alikuwa na hadhi bora miongoni mwa Wanachuoni wa enzi zake. Hii ni kutokana na sababu nyingi, kama vile uwezo wake wa kusawazisha mambo ambayo yenye utata kwa Wanachuoni wengine wa enzi zake, kama vile suala la kuwapiga vita Matartar na suala la upotofu uliotoka kwa kundi la Maraafidhah.[4] Ibn Taymiyyah aliyapigia mbizi masuala haya na kuyatolea ufafanuzi kwa watu.

 

Mnamo mwaka 701H, Myahudi mmoja kutoka Khaybar akidai kwamba alikuwa na barua kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ambayo ikipinga (hukumu sahihi ya) Jizyah[5] ambayo Mayahudi (na wengine wasio Waislamu) walilazimika kuilipa kwa Waislamu. Ibn Taymiyyah aliweka bayana uongo wake na kuipitia mapungufu yake na kuitoa thamani barua hiyo ya uongo kutokana na maelekezo ya Hadiyth na pia kwa kuegemezea elimu ya historia.[6]

 

Wakati huo huo, Ibn Taymiyyah akiwa jela mjini Cairo, Ibn Kathiyr anasema: “Masuala ya kishari’ah yaliyo magumu yalikuwa yakiletwa kwake kutoka kwa magavana na watu mahsusi, ambayo ‘Ulamaa walikuwa hawawezi kuyafanyia kazi, na yeye huyajibu kutoka kwa Kitabu na Sunnah katika namna ambayo akili huwekwa wazi.”[7]

 

Sababu nyengine ni nafasi yake katika Jihaad; alikuwa si tu kwamba ni askari mwenye nguvu lakini pia mueleweshaji na muongozaji. Alifuatwa baadaye kutoa ushauri na mikakati ya kivita.

 

La muhimu zaidi, moja kati ya sababu kuu zilizokuwa ni msukuwa wa kuhodhi nafasi bora kabisa miongoni mwa Wanachuoni na watu wanaofanana naye ni uwezo wake wa kuelezea elimu. Pale anapotoa mhadhara; anapofikisha mazungumzo; anapotoa hukumu ya kishari’ah; anapoandika barua au kuandika kitabu katika nyanja yoyote, huzalisha kiwango cha elimu ambacho kipo mbali kabisa na kuwashinda Wanachuoni wengine wa wakati wake. Hii ndio sababu ya Ibn Taymiyyah kuwa ni sehemu ya rejeo miongoni mwa watu. Popote watu wawili wanapokutana na mgogoro kuhusiana na suala – na huenda wakawa ni watu wenye elimu na wanafunzi mfano wa hao kama ilivyoonekana kwenye baadhi ya masuala – mawazo yake huwa ndio sababu ya masawazisho baina yao.

 

 

[1] Evolution of Fiqh uk. 144 cha Dr. Bilal Philips.

[2] The Lofty Virtues of Ibn Taymiyyah, uk. 30.

[3] Kama ilivyotajwa na al-Haafidh al-Bazzaar ndani ya kitabu cha ‘The Lofty Virtues of Ibn Taymiyyah’, uk. 30.

[4] Al-Bidaayah wa an-Nihaayah, 14/78.

[5] Ni kodi ya kichwa wanayolipa wasiokuwa Waislamu waliobaleghe katika dola ya Kiislamu kwa misingi maalum na wao kupata hifadhi na uhuru wa kuabudu na kuwasaidia wao na mafakiri wao na wasiojiweza. Hii ni kutokana na Qur-aan, Suwraah Tawbah, 29:

قَاتِلُوا الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَلَا بِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَلَا يُحَرِّمُونَ مَا حَرَّمَ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَلَا يَدِينُونَ دِينَ الْحَقِّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حَتَّىٰ يُعْطُوا الْجِزْيَةَ عَن يَدٍ وَهُمْ صَاغِرُونَ﴿٢٩﴾

Piganeni na wale wasiomwamini Allaah na wala Siku ya Mwisho, na wala hawaharamishi Aliyoyaharamisha Allaah na Rasuli Wake, na wala hawafuati Dini ya haki miongoni mwa wale waliopewa Kitabu, (piganeni nao) mpaka watoe jizyah (kodi) kwa khiyari, wakiwa hali ya kurudi chini kutii. [At-Tawbah: 29]

[6] Al-Bidaayah wa an-Nihaayah, 14/19.

[7] Al-Bidaayah wa an-Nihaayah, 14/46.

 

 

Share