Kisa Cha Hijaab Ya Khawla

 

Kisa Cha Hijaab Ya Khawla

 

Na Ukht Khawla Kutoka Japan 25/10/1993[1]

 

Imekusanywa Na: Dr. Swaalih As-Swaalih

 

Imetafsiriwa Na: Naaswir Haamid

 

www.alhidaaya.com

                                                               

 

“Maoni kupitia Hijaab” ni tokeo la kielimu la maisha katika Hijaab.

 

Imeandikwa na Khawla Nakata; ni ufahamu wa Hijaab kama unavyoonekana kupitia macho ya mwanamke wa Kijapani ambaye ameufuata Uislamu.

 

 

Simulizi Yangu Katika Uislamu:

 

Kama walivyo Wajapani wengi, sikufuata dini yoyote kabla ya kuingia katika Uislamu nchini Ufaransa. Nilijikita na fani ya lugha/fasihi ya Kifaransa katika Chuo Kikuu. Walimu wangu wakuu walikuwa ni Sarte, Nietchze na Camas, ambao fikra zao ni zile zisizofungamana na Allaah (za kikafiri). Wakati huo huo, hata hivyo, nilikuwa na shauku kubwa ya dini, sio kwa sababu ya haja iliyopo ndani mwangu, lakini kwa sababu ya kupata ukweli.

Kipi kinafuata baada ya kufa kwangu halikuwa na maana sana hata kidogo; namna ya kuishi ndio ulikuwa mkazo wangu.[2] Kwa kipindi kirefu, nilikuwa na aina ya hisia kwamba sitekelezi yale ninayohitajika na nilikuwa napoteza muda wangu. Iwapo Allaah yupo au hayupo ilikuwa ni sawa kwangu; nilikuwa nahitajia kuelewa ukweli na kuchagua njia yangu ya kuishi daima pamoja na Allaah au bila ya Allaah.

 

Nilianza kusoma vitabu kuhusiana na dini tofauti isipokuwa Uislamu. Sikupatapo kufikiria kwamba Uislamu ulikuwa ni Diyn yenye nafasi muhimu kuisoma. Ilikuwa kwangu, kwa wakati huo, [Uislamu ni] aina ya ujinga uliopitwa na wakati kwa akili ya kawaida (namna gani nilikuwa mjinga!). Nilifanya urafiki pamoja na Wakiristo, ambao pamoja nao nilisoma Biblia, kufikia kuelewa baada ya miaka michache baadaye uwepo wa Allaah. Lakini ilinibidi kuutambua utata kwa sababu sikuwa na “hisia” ya Allaah hata kidogo, isipokuwa kupata uhakika kwangu kwamba yeye yupo. Nilijitahidi kusali kanisani, lakini bila ya mafanikio. Sikuwa na hisia yoyote isipokuwa tu kutokuwepo Allaah.

 

Kisha nikasoma Ubudha, nikiwa na matarajio kwamba nitakuwa na uwezo wa kumuhisi Allaah kupitia Zen au Yoga. Nikaona mambo mengi ndani ya Ubudha kwamba yalionekana kuwa ni sahihi kama nilivyoona kwa Ukiristo, ingawa kulikuwa na mambo mengi ambayo sikuyaelewa au kuyakubali. Kwa maoni yangu, iwapo Allaah yupo, ni lazima Akuwepo kwa kila mtu[3] na ukweli uwe ni mwepesi na wa wazi kwa kila mtu. Sikuelewa kwa nini watu waache maisha ya kawaida kwa kujikurubisha wao wenyewe kwa Allaah.

 

Nilikuwa katika upotevu mkubwa ni lipi la kufanya hadi kufikia hatima ya shauku ya kumtafuta Allaah. Ikafikia baadaye kwamba nikakutana na Muislamu wa Ki-Algeria. Amezaliwa na kukulia Ufaransa, hakujuwa hata kuswali na maisha yake yalikuwa mbali sana kutoka katika [sifa za] Muislamu mwenye msimamo; ingawa, alikuwa na imani ya kweli kuhusiana na Allaah. Hata hivyo, imani yake bila ya elimu ilinikuna na kuniamulia kuusoma Uislamu. Kwa kuanzia, nilinunua tafsiri ya Kifaransa ya Qur-aan, lakini sikuweza kusoma zaidi ya kurasa mbili. Ilionekana kuwa ni ya maajabu na iliyo doro. Nikaachana na jitihada zangu kuifahamu peke yangu na nikaenda Msikitini mjini Paris kumtaka mtu kunisaidia. Ilikuwa ni siku ya Jumapili na kulikuwa na mtoa muhaadhara wa kike. Wanawake walinikaribisha kwa ukarimu. Ilikuwa ni mara yangu ya mwanzo kukutana na Waislamu wanawake wenye kuufanyia kazi Uislamu. Kwa mshangao wangu, nilijisikia mwepesi kuwa pamoja nao, ingawa mara zote nilijisikia ni mgeni katika mahusiano ya Wakiristo. Nikaanza kuhudhuria muhaadhara wa kila mwisho wa wiki na kusoma kitabu nilichopewa na mmoja wa Muislamu wa kike. Kila dakika ya muhaadhara na kila kurasa ya kitabu zilikuwa, kwangu, ni ufunuo, vikinipa ridhaa ya kiroho ya hali ya juu ambayo sikupata kuielewa hapo kabla. Nilikuwa na hisia ya kimaajabu kwamba nilikuwa nikiingizwa katika ukweli. Kilichokuwa kizuri mno, Subhaana Allaah (Ametakasika Allaah), ni hisia yangu ya kuwepo karibu kabisa na Allaah ninapokuwa katika utulivu wa Sajdah (kusujudu).

 

Simulizi Ya Khawla Kuhusiana Na Hijaab

 

“Miaka miwili iliyopita nilipoufuata (nilipouamini) Uislamu nchini Ufaransa, majadiliano yaliyoizunguka uvaaji wa Hijaab yalikuwa ni mada nzito sana. Watu wengi walifikiri kuwa ni dhidi ya kanuni ya skuli za umma ambazo zinalazimika kuweka msimamo usiofungamana na dini. Mimi, ambapo sikuwa bado ni Muislamu kipindi hicho, sikuelewa hata kidogo ni kwa nini walikuwa na wasiwasi kwa kitu ambacho ni kidogo mno mfano wa kiskafu (kishungi) kidogo kinachovaliwa kichwani mwa mwanafunzi Muislamu... lakini, hatimaye, Wafaransa ambao walipambana na tatizo kubwa la ongezeko la takwimu za kutokuwepo ajira na usalama wa miji mikubwa kufikia kuwa ni wasiwasi juu ya wafanyakazi wahamiaji kutoka nchi za Kiarabu. Wakajisikia kuchukizwa na muonekano wa Hijaab ndani ya mitaa yao na skuli zao.

 

Ndani ya nchi za Kiarabu, kwa upande mwengine, wimbi kubwa la kurudi kwa Hijaab lilionekana haswa miongoni mwa kizazi cha vijana, dhidi ya matarajio, yaliyoaminiwa na baadhi ya Waarabu na wengi wa Wamagharibi, wa kupotea kwake kuonekana kama ambavyo mzizi wa Kimagharibi ulivyochipuwa.

 

Kurudi kwa nembo za Kiislamu zilizozaliwa upya hivi sasa kwa Hijaab mara nyingi imeonekana kuwa ni jaribio la Waislamu Waarabu kurudisha ufakhari na alama yao ambazo zimeendelea kudumazwa kwa sera za ukoloni na uchumi. Kwa Wajapani, utiifu halisi wa Waarabu kwa Uislamu inaweza kuonekana kama ni aina ya utamaduni usiotaka mabadiliko au utamaduni ulio dhidi ya Umagharibi, ambao Wajapani wenyewe wamejitambua katika enzi za Meiji kukutana kwa mara ya kwanza na tamaduni za Kimagharibi, na ni kwa sababu ya namna walivyorudisha pigo dhidi ya mtindo wa maisha ya Kimagharibi na namna ya uvaaji wa Kimagharibi. Mwanaadamu daima amekuwa na tabia ya kuwa na msimamo na kugeuka kinyume dhidi [ya mambo ambayo] ni mepya na hayajazoeleka bila ya kutambua iwapo ni zuri au baya kwake. Baadhi ya watu bado wanawafikiria wanawake Waislamu kusisitiza kuvaa Hijaab ambayo ni “nembo pekee ya hali ya unyanyasaji kwa sababu wapo kifungoni mwa utumwa kutokana na tamaduni [zao] na hawana uelewa tosha wa hali zao mbovu kabisa. Iwapo tu, pengine wanafikra, harakati za ukombozi wa mwanamke na uhuru unaziamsha akili za wanawake, basi wataitupilia mbali hiyo Hijaab.”

 

Ni nukta ya fikra ya kijinga inayokubaliwa na watu ambao wana elimu ndogo ya Uislamu. Wao, ambao wamejikubalisha katika usekula na dini mseto, kwa urahisi hawawezi kueleza kwamba mafundisho ya Uislamu ni ya ulimwengu wote na yenye kudumu milele. Hata hivyo, wapo wanawake zaidi na zaidi, kupindukia Utaifa wa Kiarabu, sehemu zote duniani wakiufuata Uislamu kama ni Diyn sahihi na wakifunika nywele zao. Mimi si chochote isipokuwa ni mfano wa wanawake hawa. Hijaab kwa hakika ni nembo ya maajabu kwa wasiokuwa Waislamu.

 

Kwa wao, Hijaab sio tu kufunika nywele za mwanamke lakini pia kuficha kitu ambacho wao hawaruhusiki kuingia, na ni hivyo kwa sababu ndio hawajisikii raha. Kwa uonekano wa nje, kwa uhakika wake, hawawezi hata siku moja kuona lililo nyuma ya Hijaab. Nimekuwa nikiivaa Hijaab tokea nilipokuwa Muislamu miaka miwili iliyopita... Nchini Ufaransa, baada tu ya kurejea kwangu ndani ya Uislamu, nikavaa kiskafu, nikifananisha kwa rangi ya nguo, nyepesi kichwani mwangu, ambao kwa watu watahisi kuwa ni aina ya ulimbwembwe fashion.[4] Sasa hivi nchini Saudi Arabia, ninajifunika mwili wangu wote weusi kutoka juu ya kichwa hadi kidole cha mguuni yakiwemo macho... Wakati nilipoamua kuuamini Uislamu, sikufikiria kwa umakini kuhusiana na iwapo nitaweza kuswali Swalah tano kwa siku au kuvaa Hijaab.

 

Labda nilikuwa na wasiwasi kwamba nitapata jibu baya, na kwamba hilo litaathiri maamuzi yangu ya kuwa ni Muislamu. Nimeishi katika ulimwengu ambao ulikuwa hauna chochote kuhusiana na Uislamu hadi nilipoutembelea, kwa mara ya mwanzo, Msikiti wa Paris. Si Swalah wala Hijaab iliyokuwa imezoeleka kwangu. Sikujiamini mwenyewe kuswali na kuvaa Hijaab. Lakini shauku zangu za kuwa Muislamu zilikuwa na nguvu kubwa [hadi] kuwa na wasiwasi kuhusiana na yale yanayonisubiri baada ya kurejea katika Uislamu. Kwa hakika, ilikuwa ni miujiza kwamba nimeufuata Uislamu, Allaah Akbar.

 

Kwa Hijaab nikajisikia kuwa tofauti. Nikajisikia mwenyewe kutakasika na kuhifadhika. Nikahisi uhusiano na Allaah. Kwa kuwa ni mgeni, nikahisi baadhi ya wakati kutokuwa na raha katika sehemu za jamii, nikistaajabiwa na watu. Pamoja na Hijaab, sikuweza kuonekana. Nikaona kwamba Hijaab imenipatia makaazi kutokana na mitazamo michafu. Nilikuwa pia na furaha kubwa na fakhari kwa Hijaab ambayo si tu ni alama ya utiifu wangu kwa Allaah lakini pia ni ufunuo wa imani yangu... ukiachana na hilo, Hijaab inatusaidia kutambuana mmoja kwa mwengine na kushirikiana katika hisia za kidada. Hijaab pia imenipatia faida ya kuwakumbusha watu wanaonizunguka kwamba Allaah yupo na kunikumbusha mimi kujikurubisha kwa Allaah.[5] Inaniambia: “kuwa muangalifu. Ni lazima ujichunge mwenyewe kuwa ni Muislamu.” Kama ambavyo askari anavyokuwa na umakini zaidi wa kazi yake anapokuwa na sare za kazi, nilikuwa na hisia kali zaidi ya kuwa Muislamu pamoja na Hijaab.

 

Mara, nikaanza kuivaa Hijaab kabla ya mimi kutoka nyumbani mara zote ninapokwenda Msikitini. Lilikuwa ni tendo la kiasili na la hiari ambalo kwalo hakuna aliyenilazimisha kulitenda. Wiki mbili baada ya kurejea katika Uislamu, nikarejea Japan kuhudhuria ‘arusi ya mmoja wa dada zangu, na nikaamua kutorejea nchini Ufaransa. Kwa kuwa sasa nimekuwa ni Muislamu na kuona kwamba lile nililokuwa nikilitafuta, lugha/fasihi ya Kifaransa kutokuwa na hamu nayo tena. Nikawa na shauku zaidi ya kujifunza Kiarabu.[6]

 

Kwangu mimi... ilikuwa ni jaribio kuishi mji mdogo nchini Japan, kutengwa moja kwa moja na Waislamu. Lakini utenganifu huo ukanisaidia kuutia nguvu uaminifu wangu wa kuwa Muislamu. Kama ambavyo Uislamu unavyomzuia mwanamke kudhihirisha mwili na kuvaa nguo zinazoudhihirisha mwili wote, nikalazimika kuachana na nguo nyingi kama vile skati fupi mini-skirts na viblauzi vifupi vyenye nyuzi nusu half-sleeve blouses. Kwa uhakika, ulimbwembwe wa Kimagharibi haufanani hata kidogo pamoja na Hijaab. Nikaamua, hivyo, kujishonea nguo mwenyewe. Nikamuomba rafiki yangu anayeelewa kushona nguo kunisaidia, na ndani ya wiki mbili nikatengeneza nguo yenye “suruali” pantaloon baada ya kufuata mtindo wa “nguo ya Kipakistani” Pakistani dress. Sikujali hata kidogo watu kuangalia “ulimbwembwe” wangu wa kimaajabu.

 

Wiki mbili zimepita tokea niliporudi Japan, pale hamu yangu ilipopanda zaidi katika kusoma Kiarabu na Uislamu ndani ya nchi ya Waislamu kwamba nikaamua kujikubalisha. Nikaenda Cairo ambapo nilikuwa namtambua mtu mmoja tu.

 

Nilikuwa nimepotea kabisa kutambua kwamba familia ya wenyeji wangu haizungumzi Kiingereza. Kwa mshangao wangu, zaidi, dada aliyeuchukua mkono wangu kuniongoza ndani ya nyumba, alikuwa amejifunika mwili wote kwa weusi kutoka juu hadi mguuni ikiwemo uso. Ulimbwembwe huo hivi sasa umezoeleka na nimeufuata kuuvaa mwenyewe mjini Riyaadh, lakini kwa kipindi hicho, nilikuwa na mshangao mkubwa kuona hivyo.

 

Niliwahi kuhudhuria mara moja nchini Ufaransa mkutano mkubwa kwa Waislamu, na katika mnasaba huo, nikaona kwa mara ya mwanzo mwanamke akiwa na nguo nyeusi pamoja na chenye kufunika uso ‘Niqaab’. Uonekano wake miongoni mwa wanawake katika nguo yenye kukolea rangi na kiskafu ilikuwa ni yenye mshangao mkubwa na nikajisemea: “huyo hapo, mwanamke aliye utumwani mwa mila za Kiarabu bila ya kuelewa mafundisho sahihi ya Uislamu”, kwa sababu nilielewa baadhi ya mambo kuhusiana na Uislamu kwa wakati huo na nikafikiria kwamba kuufunika uso ilikuwa si chochote zaidi ya mila isiyopatikana ndani ya Uislamu.

 

Picha iliyokuja kichwani mwangu baada ya kumuona mwanamke aliyejifunika mjini Cairo haikuwa mbali sana na [fikra] hiyo [niliyoipata Ufaransa]; amezidisha mno – hilo si halisi... jitihada zake za kujaribu kukimbia kuonekana na mwanamme yeyote pia linaonekana kuwa si la kawaida.

 

Dada aliyevaa nguo nyeusi aliniambia kwamba nguo niliyoshona mwenyewe haifai kutoka nayo nje. Sikufurahikia naye kwa sababu nguo yangu ilitimiza masharti ya nguo ya Muislamu... Nikanunua kitambaa cheusi na kutengeneza nguo refu na shungi refu linaloitwa “Khimaar” ambalo linafunika kiuno na mikono yote mizima. Nilikuwa hata tayari kufunika uso kwa sababu ilionesha kuwa ni vizuri “kuepuka vumbi”, lakini dada yule akasema kwamba hakuna haja ya kufanya hivyo. Sihitajiki kuufunika uso kwa hoja hiyo ilhali dada hawa wanaivaa kwa sababu ya kuamini kuwa ni wajibu wa Diyn. Ingawa dada wengi niliokutana nao walijifunika uso, hawakuwa ni wengi zaidi ya watu kidogo ndani ya mji wote wa Cairo, na watu wengine walipigwa na butwaa na kuchukizwa kwa muonekano wa Khimaar jeusi. Hakika Wamisri vijana wa kawaida au wenye msimamo mkubwa wa Magharibi walijaribu kuwa mbali na wanawake wanaovaa Khimaar, wakiwaita “dada wale” the sisters. Wanaume nao wakiwatendea kwa heshima fulani na upole maalumu mitaani au ndani ya basi bus. Wanawake hao wakipenda kwa udugu wa kidada na kubadilishana salaam (kiamkio cha Kiislamu) mitaani hata bila ya kujuana...

 

Kabla ya kurejea kwangu ndani ya Uislamu, nilipendelea kuvaa suruali za kiaina dhidi ya skati za kike, lakini nguo ndefu nilizoea kuzivaa nilipokuwepo Cairo ziliniridhisha kwa muda mchache. Inanifanya kujisikia kwamba nimevaa nguo maridhawa zaidi kana kwamba nimekuwa ni mtoto wa Mfalme. Ninajisikia kuwa na utulivu zaidi ndani ya nguo ndefu kuliko suruali pantaloon...

 

Dada zangu walikuwa ni wazuri na wenye kungaa katika kivazi chao cha Khimaar, na walionekana kuwa na muenekano wa kiucha Allaah katika nyuso zao... [Kwa] kila Muislamu aliyejiegemeza maisha yake kwa Allaah. Ninawaza kwa nini watu wasiosema chochote kuhusiana na “shungi” za “Dada wa Kikatoliki” wanavyoikana shungi ya dada Muislamu Muslimah, wakiitambua kama ni alama ya “ugaidi” au “unyanyasaji”.

 

Nilitoa jibu baya pale dada wa Kimisri aliponiambia kuvaa hivi hata nitakaporejea Japan... Iwapo nitajionesha katika nguo refu jeusi kama hiyo mitaani nchini Japan, watu wanaweza kufikiria kwamba mimi ni mwendawazimu.[7] Wakiwa wameshangazwa na nguo yangu, hawatapendelea kunisikiliza, kwa lolote nitakalosema. Wataukataa Uislamu kwa sababu ya muenekano wangu, bila ya kujaribu kuelewa mafundisho yake.[8] Hivyo, nikajibizishana naye.

 

Miezi sita baadaye, hata hivyo, nikawa nimezoea kuvaa nguo refu na kuanza kufikiria kuivaa hata niwapo nchini Japan. Hivyo, kabla tu ya kurejea Japan, nikatengeneza baadhi ya nguo zenye rangi hafifu na Khimaar nyeupe, nikifikiria kwamba zitakuwa ni zenye kustaajabisha kidogo kuliko zile nyeusi.

 

Nilitendewa vizuri na Wajapani kwa Khimaar yangu nyeupe na sikukutana na ukanaji au kejeli yoyote. Ilionekana wao kutambua uhusiano wangu kwa Diyn bila ya kujua ni dini gani. Nikasikia mwanamke kijana nyuma yangu akimnong’oneza rafiki yake kwamba mimi nilikuwa ni “Mlokole wa kike wa Kibudha”...

 

Mara moja nilipokuwepo ndani ya basi, nilikaa na babu kizee aliyenuliuza ni kwa nini nimevaa nguo ya aina ya kiajabu. Nikamueleza kwamba mimi ni Muislamu na ndani ya Uislamu wanawake wanaamrishwa kuufunika mwili wote na uzuri wao, ili kutowashughulisha wanaume ambao ni wepesi kwa aina hii ya kutamanisha. Alionekana kuvutiwa na maelezo yangu, pengine kwa sababu alikuwa hakubaliani na kivazi cha kutamanisha cha wanawake vijana wa leo. Aliondoka ndani ya treni akinishukuru na kuniambia angependelea kupata muda zaidi wa kuzungumza na mimi kuhusiana na Uislamu.

 

Baba yangu alinionea huruma pale ninapotoka nje hata katika siku ya joto kali katika msimu wa kiangazi pamoja na guo refu na mtandio wa kichwa, lakini niliiona Hijaab kuwa ni muwafaka kwa ajili ya kuepuka kupiga jua la moja kwa moja katika kichwa na shingo... Nikajisikia vibaya kuyaona mapaja meupe ya ndugu yangu wa kike aliye kijana kwa sababu ya kuvaa suruali fupi. Mara kadhaa nimekuwa nikichukizwa hata kabla ya kurejea kwangu ndani ya Uislamu kwa kuyaona makalio na mapaja ya mwanamke yakionekana kutokana na kuvaa nguo nyepesi zinazobana umbo. Nikajisikia kana kwamba nimeona kitu ambacho hakifai kuonekana. Iwapo muenekano kama huo unanichukiza ambao ni wa jinsia ya aina moja, sio taabu kutambua ni athari gani nakuwa nayo iwapo ni mwanamme.

 

Ni kwa nini uufiche mwili kutokana na uasili wake? Unaweza kujiuliza hivyo. Lakini fikiria ilikuwa ni tusi miaka hamsini iliyopita, nchini Japan kuogelea kwa nguo za kuogelea. Hivi sasa tunaogelea na bikini bila ya hayaa. Iwapo utaogelea, hata hivyo, bila ya nguo ya juu, watu watasema wewe kuwa huna aibu, lakini nenda pwani ya Ufaransa ya Kusini, ambapo wanawake wengi, vijana na vizee, wanajianika juani bila ya nguo ya juu topless. Iwapo utaenda pwani fulani ukanda wa magharibi nchini Marekani, watu wasiovaa nguo wanajianika juani wakiwa utupu kama wa kuzaliwa. Kwa upande mwengine, kwa enzi za kale, mpiganaji wa usiku alitetemeka kutokana na kuona kidogo kiatu cha mwanamke mwenye kuvutia.

 

Inaonesha ni kwa namna gani tafsiri ya “sehemu za siri” inavyobadilishwa. Ni kwa namna gani utaweza kumjibu mwenda utupu mwanamke iwapo atakuuliza kwa nini unaficha makalio na mapaja yako ingawa [viungo] hivyo ni vya asili kama vilivyo mikono na uso? Ni kwa namna sawa kwa Hijaab ya Muslimah. Tunaamini kwamba mwili wetu wote isipokuwa mikono na uso ni sehemu faragha kwa sababu Allaah Ametueleza hivyo.[9] Ndio maana tunavificha kwa wanaume wanaoweza kutuoa ajnabiyy. Iwapo utaweka kitu siri, kinazidisha thamani yake. Kuuweka mwili wa mwanamke kuwa ni siri unaongeza uzuri wake. Hata kwa jicho la jinsia sawa, umbo la shingo ya dada wa kike inavutia zaidi kwa sababu ni kawaida yake kuwa inafunikwa. Iwapo mwanamme atakosa hisia za aibu na kuanza kutembea utupu na kuchupa mpaka hadi “kufanya mapenzi” mbele za watu wengine, hatakuwa na tofauti kuliko mnyama. Nafikiria kwamba mila ya wanaume imeanza pale wanaume walipotambua hisia za aibu.

 

Baadhi ya wake wa Kijapani (wanavaa) vipodozi vyao usoni pale tu wanapotoka nje, hawajali ni kwa namna gani wanavyoonekana ndani mwao. Lakini ndani ya Uislamu, mke anajitahidi kujipendeza haswa kwa mumewe na mume anajitahidi kuonekana mzuri ili kumridhisha mkewe. Wana aibu hata baina yao wenyewe na mbele ya mmoja kwa mwengine. Unaweza kusema kwa nini tuna “aibu zilizochupa mpaka” kuficha mwili isipokuwa kwa uso na mikono, hili ni kwa ajili ya kutoziamsha shahawa za mwanamme, kama inavyokuwa kwa mwanamme anapomuangalia mwanamke kwa matamanio ya kimapenzi.

 

Lakini tatizo la unyanyasaji wa kijinsia ambalo unapigiwa kelele mno hivi leo unaonesha ni kwa namna gani wanaume walivyo dhaifu kuhimili aina hii ya mvuto. Hatuwezi kutegemea kinga ya unyanyasaji wa kijinsia eti tu kwa kuziomba tabia nzuri na kujizuia kiasili... Kama ambavyo inavyofasiriwa skati fupi kumaanisha kusema: “Iwapo unanitaka, unaweza kunichukua”, lakini Hijaab ina maana tofauti kabisa: “Mimi nimeharamika kwako”.

 

Miezi mitatu baada ya kurejea kutoka Cairo, nikaondoka Japan kwenda Saudi Arabia, na mara hii nikiwa pamoja na mume wangu. Nilitayarisha nguo ndogo nyeusi kuufunika uso... Nilipowasili Riyaadh, nikaona kwamba wanawake wote wakijifunika uso. Wageni wasiokuwa Waislamu bila ya shaka wanavaa nguo nyepesi tu zisizovutia bila ya kufunika kichwa, lakini

Waislamu wageni pia wanafunika uso.[10] Ama kwa wanawake wa Kisaudi, wote wakionekana kujifunika vizuri kutoka juu hadi mguuni. Katika kutoka kwangu mara ya kwanza, nikavaa Niqaab na kutambua kwamba ilikuwa ni nzuri sana. Pale tu unapoizoea, hakuna mashaka yoyote.

 

Isipokuwa, nilijisikia kawaida kama nimekuwa ni mtu muadilifu na mahsusi. Nikajisikia kana kwamba ni mmiliki wa kipande kilichoibiwa aliyefaidika na thamani yake ya siri: Nina hazina ambayo huielewi na ambayo huruhusiki kuiona. Mgeni anaweza kuona baadhi ya wanaume wanene na wanawake waliojifunika nguo nyeusi anayemfuata katika mitaa ya Riyaadh kama ni kikatuni cha uhusiano wa unyanyasaji-unyanyaswaji au uhusiano wa umiliki-umilikiwa, lakini ukweli ni kwamba wanawake wanajisikia kama kwamba wao ni Wafalme wanaolindwa na kuongozwa na watumwa wao.

 

Katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo mjini Riyaadh, nikaziba sehemu tu zilizo chini ya macho. Lakini nilipotengeneza nguo ya kipupwe, nikatengeneza kwa mnasaba huo huo nguo nyepesi katika sehemu ya macho. Himaya yangu ikaimarika na halikadhalika utulivu wangu. Hata mbele ya kundi la wanaume, sikujisikia vibaya. Nikajisikia kana kwamba nimekuwa muwazi mbele ya macho ya wanaume. Ninapoonesha macho, baadhi ya wakati sijisikii vizuri pale macho yangu yanapokutana na macho ya mwanamme bila ya kukusudia, haswa kwa sababu Waarabu wana macho makali. Sehemu inayofunikwa na macho inazuia, kama vile macho ya jua sun-glasses, muonekano wa macho kwa mtu nisiye muelewa.

 

Khawla anaelezea zaidi kwamba wanawake Waislamu “wanajifunika kwa heshima yao wenyewe. Anakataa kumilikiwa na macho ya wasiomuhusu na kuwa ni zana yake. Anajisikia taabu kwa wanawake wa Kimagharibi ambao wanazionesha sehemu zao za faragha kama ni zana za mwanamme asiyemuelewa stranger. Iwapo mtu ataiona Hijaab kwa muonekano wa nje, mtu hataweza kuona kilichofichika ndani. Kuiona Hijaab kwa nje na kuishi nayo kwa ndani ni vitu viwili tofauti kabisa. Tunaona vitu tofauti. Pengo hili linaeleza tofauati iliyokuwepo ya kuufahamu Uislamu.

 

Kutoka kwa nje, Uislamu unaonekana kama ni ‘jela’ isiyokuwa na huruma. Lakini kuishi nayo ndani, tunajisikia salama na uhuru na fakhari ambao haujapatapo kuonekana kabla.... Tunauchagua Uislamu dhidi ya kile kinachoitwa uhuru na furaha. Iwapo ni kweli kwamba Uislamu ni Diyn ambayo inamnyanyasa mwanamke, kwa nini kuna wanawake wengi Ulaya, Marekani, na Japan wanaoacha [kwa unaoitwa] uungwana na uhuru kwa ajili ya kuutumikia Uislamu? Ninataka watu wafananishe na hilo.

 

Mtu aliye kipofu kwa sababu ya chuki zisizokuwa na sababu inawezekana asiuone hivyo, lakini mwanamke aliye na Hijaab ni mzuri sana kama mtakatifu fulani aliye na msimamo binafsi, utulivu, na ustaarabu. Hakuna mguso hata mwepesi wa kivuli wala alama ya unyanyasaji unaoonekana katika uso wake. ‘Wao ni vipofu na wala hawawezi kuona’, inasema Qur-aan kuhusiana na wale wanaokana alama za Allaah, lakini ni kwa kipi chengine tunachoweza kueleza pengo hili katika kuufahamu Uislamu baina yetu na watu hao.” (3/1993)

 

 

Angalizo:

Makala ya Khawla ilipelekwa (mwishoni mwa 1993) katika Afisi ya Wanawake wa Kituo cha Uongofu wa Kiislamu, Buraydah, Al-Qaasim, KSA.

 

[1] Ukht Khawla alitembelea ofisi ya Wanawake wa Kituo cha Uongofu wa Kiislamu, mjini Buraydah, Al-Qaasim, Saudi Arabia mnamo 25/10/1993. Alisimulia maelezo haya pamoja na dada Waislamu ndani ya ofisi. Nimeona muhimu kuwapatia nafasi kwa kaka na dada wa Kiislamu kuelewa simulizi ya Khawla katika kuufuata Uislamu ikifuatiwa na fikra zake na ushauri kuhusiana na Hijaab.

 

[2] Hii ni fadhaa kwa watu wengi duniani na zaidi kwa Magharibi au nchi ambazo zimetawaliwa na tamaduni za Kimagharibi. Watu wanakuwa ni “wendawazimu” kushikamana pamoja zaidi na zaidi kwa yale wanayohitaji kuyapata (ya kidunia). Mambo madogo ya leo ni mahitajio makubwa kwa kesho! Njia ya wastani iliyoelezwa na Muumba, Allaah, inadharauliwa isipokuwa kwa wachache. (Dr. S. As-Swaalih).

 

[3] Allaah ni Allaah wa kila mtu. Hii ingawa inamaanisha kwamba Allaah ni lazima atakuwa ni mmoja. Hakuna uhusiano wa kitaifa kwa Allaah! Kwa kuwa ni Allaah wa kila mtu, Haamuru baadhi ya watu kumuabudia Yeye peke yake ilhali wakati huo huo akiwaruhusu wengine kuanzisha uadui dhidi Yake katika ibada. Nii inamaanisha kwamba ibada Zake ni lazima ziwe [za namna] moja na kwamba sio jukumu letu kutoa maana ya aina hii ya ibada. Njia ya ibada ipo mikononi mwa Mmoja na Allaah Mmoja Pekee wa Kweli tu, Allaah. Hii inahusisha Diyn Yake na Ameitaja njia hii: Uislamu.

 

[4] Anatoa fikra za utotoni mwake kuhusiana na mwamko wa dini na ufahamu wake

.

[5] Yaani ufahamu wa Allaah.

 

[6] Inajadiliwa kwa nguvu zote kwamba Waislamu wote wasiozungumza Kiarabu kujifunza Kiarabu. Itawasaidia kuelewa vizuri kuhusiana na Uislamu.

 

[7] Waislamu wengi wanawake wanajisikia kuwa na hisia kama hizi. Hivi ni vitimbi vya Shaytwaan kumjaribu kumuweka mbali Muslimah katika kumtii Allaah.

 

[8] Shaytwaan anamtaka Muislamu kujisikia “duni”. Muumini, hata hivyo, anakumbuka kwamba Uislamu unatoka kwa Allaah na mtu anayejadiliana naye si chochote zaidi ya kiumbe kilichoumbwa, ambaye atakufa na atarejea kujibu kutokana na kukana kwake Diyn ya Allaah. Hijaab kwa mwanamke na ndevu kwa wanaume ni lazima yaheshimiwe, kwanza, kwa Muislamu ili kujisikia kuwa na nguvu ya muonekano wao. Hili linaweza kufanikiwa kwa kukumbuka kwamba muonekano huu ni amri ya Allaah na Mjumbe Wake.

 

[9] Suala hili limejadiliwa ndani ya maandiko haya. Khawla anaelezea zaidi katika makala yake kwamba: “Hakuna haja ya kusema kwamba uso wa mwanamke ni moja kati ya sehemu bora kabisa. Ni rahisi kwa mtu “kuanza kumpenda” mwanamke kwa kuuona tu mara moja uso. Ni bora kwa mwanamke kuuficha uso wake.”

 

[10] Si wote. Uhakika kwamba nchini Saudi Arabia, Waislamu wengi wanawake kutoka nchi nyingi wanafunika nyuso zao.

 

 

Share