Zingatio: Kebehi Dhidi Ya Waislamu
Zingatia: Kebehi Dhidi ya Waislamu
Na: Naaswir Haamid
Rabb Alipotueleza kwamba Ameturidhia Uislamu kuwa ni Diyn yetu na kwamba haitakubaliwa imani nyengine yoyote basi hapo sote twahitajika kufuata njia sahihi za Qur-aan na Sunnah bila ya kuterereka.
Sasa inakuwa ni kizungumkuti pale Muislamu mwenzetu, ambaye anauma zaidi kuliko kafiri, kuanza kusema kuna Muislamu mwenye msimamo mkali. Cha kujiuliza huyu Muislamu mwenye msimamo mkali ni yule anayemfuata Ibilisi ama anayejitahidi kusimamisha Uislamu kwa mujibu wa mafundisho sahihi ya Qur-aan na Sunnah? Huyu ni yule anayeipinga bid’ah ama anayeifuata bid’ah?
Inakuwa ni vigumu kumpatia tafsiri yenye kujitosheleza juu ya huyu aitwaye Muislamu mwenye msimamo mkali, je huyu ni yule Muislamu anayejitahidi muoenekano wake uwe unafanana na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuanzia ndevu hadi kivazi chake? Kama ni hivyo, je binti wa Kiislamu anayevaa hijabu yake naye tumuite Muislamu mwenye msimamo mkali?
Ni vyema Waislamu wakaelewa kwamba hakuna Muislamu mwenye msimamo mkali, na kama wapo, je hao wenye msimamo wa kati au wa chini ni kina nani? Haya matamshi ya Muislamu mwenye msimamo mkali ni lazima yatolewe, yaachwe yamalizie kwenye vinywa vya hao makafiri, katu yasitoke ndani ya vinywa vya Waislamu.
Kebehi hizi zimekuwa ni nyingi hadi kufikia kuwa ni kinyaa na kiroja, kwa Muislamu kuzungumza ‘jihadi’, kwa lipi kubwa? Muislamu anaogopa kuitwa ‘fundamentalist’. Tunashindwa kuelewa kwamba Jihadi ndio kitetezi chetu pale njia za busara zinaposhindikana kueleweka. Tujiulize, taifa jinamizi la Mayahudi la Izraili, litumike njia gani za kuing’oa? Ni jihadi tu pale patakaposimama Uislamu chini ya amri ya kiongozi wa Kiislamu mmoja; hakuna njia nyengine. Na ndio tunaona umuhimu wa Waislamu wote kuwa ‘siasa kali’ kama inavyodaiwa na wote kusimama kwa kitambulisho chao kimoja cha ‘Uislamu’ na sio utaifa wala ukabila.
Waislamu ni lazima waanze mikakati ya kujisafisha wenyewe kimatendo na kimavazi. Yale matendo ya kukebehiana huyu ana msimamo mkali, Muislamu poa, Muislamu mwenye siasa kali, shekhe/ustadhi na kadhalika ni vyema yakafikia kikomo.
Juu ya yote, kwa wale wanaoielewa na kuipenda Diyn yao, ni budi kuelewa kwamba hizi kashfa hazijaanza leo, hata Nabiy wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alifanyiwa kebehi kuliko hizi, alifikia hadi kuitwa mchawi. Kizuri zaidi ni kwamba Nabiy hakurudi nyuma katika kuipigania Diyn yetu, ndio aliongeza zaidi jitihada usiku kwa mchana. Nasi tuige mwendo wa Nabiy wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na tusirejeshwe nyuma kwa kauli hizi.