Talaka Baada Ya Kuzini? Anaweza Kumrudia Mkewe Baada Ya Talaka Moja Au Tatu?

SWALI:

As/aleikum warahmatulahi wabarakatu

ndugu zangu naomba mnifahamishe nipate kuelewa,ilitokeya kijana kazini njee naye anamkee,basi ikawa mkee wake anashaka kubwa kwa mume wake, nyumbani hakukaliki kwa matatizo na ugomvi hawana raha ikafika wakati mkee kuomba talaka, nilivo muuliza kijana akanambiya matendo aliyo yatenda hajuwi vipi kafika humo(disco) mpaka ikatokeya akaanguka kwenye zina naye sio mtuu wakwenda sehemu hizo. sio mlevi wala hakutumiya kitu chochote cha ulevi, nakijana huyo alikuwa anasoma njee U.K, basi kurudi ao kumaliza masomo akarudi kwao, kurudi kwao aka'owa ,basi shangazi yake alikasirika sana sababu haku owa binti yake alikuwa anategemeya kama huyo kijana mtoto wa kaka yake atamu owa binti yake.basi kwakukasirika shangazi yake yakamtoka maneno bila kukumbuka kama mungu yuko akawambiya huyo kijana na mkee wake hivi, yeye hata ona raha mpaka wa'achane yani wapeyane talaka.basi ikawa mtoto wakike yanamtokeya mauza uza usiku akilala namume wake na mambo marefu sana>>>>>> basi kijana huyo kuona roho hayiko radhi na mambo awo alivo mukhuni mkee wake na anavo mpenda akaona labda akimwambiya mkee wake dhamiri ya moyo wake atapumzika na ataepusha shari ikabidi amwambiye mkee wake kama kazini na mwanamke mwengine. sasa su'ali langu , hali hiyo inajuzu kurudiyana na mkee wake awo ni kama talaka ? na kama nitalaka inafaa mimi kama rafiki yake kumuowa mkee wake baadaye nimuache amuowe, na ikiwa inafaa kumuowa lazima nijmaa(nilale naye) huyo mkee? haiwezekani bila kulala naye nikamuacha kamuowa?  na atubu vipi ? sababu yeye karudi kwa mwenye'ezimungu na anatubiya tobat nasiha,na anajuta saaana hata kama hakufanya tendo hilo kwa yeye kutaka.

Shukrani
wallahu wali taufik

 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Kutokana na maelezo hayo, inaelekea kwamba kuna maswali manne baada ya matukio hayo ya rafiki yako, nayo ni haya kama ulivyoyataja, nasi tutajibu moja moja:

  1. hali hiyo inajuzu kurudiyana na mkee wake awo ni kama talaka ?

Ikiwa huyo kijana amefanya zinaa kisha akamjulisha mkewe na ukatokea ugomvi kama ulivyoeleza, haina maana kwamba amempa talaka, na ataendelea kuishi na mkewe  kama kawaida bila ya kuhesabika kuwa ni talaka ila tu ikiwa ameitamka yeye mume talaka au ameandika mahali kumpa mkewe.

 

  1. na kama nitalaka inafaa mimi kama rafiki yake kumuowa mkee wake baadaye nimuache amuowe

Ikiwa huyo mume amempa talaka moja tu, basi anaweza kumrudia mkewe kwani imeruhusiwa hivyo kutokana na maneno ya Allaah سبحانه وتعالى:

                   الطَّلاَقُ مَرَّتَانِ

          T'alaka ni mara mbili [Al-Baqarah:229]

          Ikiwa amempa talaka mara tatu zisizokuwa zimetolewa kwa usemi mmoja, yaani kampa talaka kwa muda mbali mbali, au zisizokuwa sehemu moja, basi ndipo itabidi mwanamke aachike kabisa na mume hatokuwa tena halali kwake kumrudia mpaka huyo mwanamke aolewe na mume mwingine na kulala naye, na baada ya kuachwa na mume mwingine tena hapo ndipo mumewe wa mwanzo anaweza kumrudia. Allaah سبحانه وتعالى  Anasema:

 

الطَّلاَقُ مَرَّتَانِ فَإِمْسَاكٌ بِمَعْرُوفٍ أَوْ تَسْرِيحٌ بِإِحْسَانٍ فَإِن طَلَّقَهَا فَلاَ تَحِلُّ لَهُ مِن بَعْدُ حَتَّىَ تَنكِحَ زَوْجًا غَيْرَهُ فَإِن  طَلَّقَهَا فَلاَجُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يَتَرَاجَعَا إِن ظَنَّا أَن يُقِيمَا حُدُودَ اللّهِ وَتِلْكَ حُدُودُ اللّهِ يُبَيِّنُهَا لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ

Talaka ni mara mbili. Kisha ni kukaa kwa wema au kuachana kwa vizuri..Na kama amempa talaka (ya tatu) basi si halali kwake baada ya hayo mpaka aolewe na mume mwengine. Na akiachwa basi hapana ubaya kwao kurejeana wakiona kuwa watashikamana na mipaka ya Allaah. Na hii ni mipaka ya Allaah Anayoibainisha kwa watu wanao jua [Al-Baqarah: 229-230] 

Tufahamu kuwa talaka ya kutoa mara moja katika sheria inaitwa Twalaqul Bidi‘iy (Talaka ya Kuzuliwa) kwani huwa imekwenda kinyume na sheria tukufu ya Kiislamu. Na hii ni ima kumpatia talaka mke  akiwa katika damu ya hedhi, nifasi au talaka tatu kwa mara moja au sehemu moja.

Ama kusema kuwa rafiki yake amuoe kwa kusudi la kutaka kuhalalisha arudie kuolewa na mumewe wa mwanzo baada ya talaka tatu,  jambo hili halifai kwani hapo inategemea Niya. Na madamu umeshataja Nia katika jambo hili, basi tayari umeshaweka Niya ya kukusudia kuhalalisha ndoa hiyo ya kurudiwa na mumewe wa mwanzo, kwa hiyo haifai kabisa kwani kila jambo linategemea na Niya kama alivyotufundisha Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  katika Hadiyth ifuatayo:

 

عن أَمِيرِ المُؤمِنِينَ أَبي حَفْصٍ عُمَرَ بنِ الخطَّابِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ : سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: ((إِنَّما الأَعْمَالُ بالنِّيَّاتِ وإنَّما لكُلِّ امْرِىءٍ ما نَوَى، فَمَنْ كانَتْ هِجْرَتُهُ إلى اللهِ ورَسُولِهِ فَهِجْرَتُهُ إلى اللهِ ورَسُولِهِ، ومَنْ كانَتْ هِجْرَتُهُ لِدُنْيا يُصِيبُها أو امْرأةٍ يَنْكِحُها فَهِجْرَتُهُ إلى ما هَاجَرَ إليه)). البخاري ومسلم

Kutoka kwa Amiri wa Waumuni, Abu Hafs 'Umar Ibn Al Khattaab رضى الله عنه ambaye alisema : Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyeezi  Mungu صلى الله عليه وسلم akisema:((Vitendo vinategemea (vinalipwa kwa) niya na kila mtu atapata kwa mujibu wa kile alichokusudia.  Kwa hivyo yule aliyehama  kwa ajili ya Allaah na Mtume wake, uhamaji wake ni kwa ajili ya Allaah na Mtume wake, na  yule ambae uhamaji wake ulikuwa ni kwa ajili ya manufaa ya kidunia au kwa ajili ya kumuoa mwanamke (Fulani) uhamaji wake ulikuwa kwa kile kilichomuhamisha)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

3.     na ikiwa inafaa kumuowa lazima nijmaa(nilale naye) huyo mkee? haiwezekani bila kulala naye nikamuacha kamuowa?

Jibu hili linaambatana na jibu la pili kwamba: Madam imeshawekwa Niya ya kutaka tu kuhalalisha ndoa arudiane na mumewe wa kwanza basi haifai kwa vyovyote hivyo.

 4-     na atubu vipi?

Milango ya Tawbah iko wazi kwa Waislamu, na Allaah  سبحانه وتعالى Anapokea Tawbah hata kama madhambi makubwa vipi. Hii ni Rahma ya Allaah kwa waja Wake.  

إِنَّمَا التَّوْبَةُ عَلَى اللّهِ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السُّوَءَ بِجَهَالَةٍ ثُمَّ يَتُوبُونَ مِن قَرِيبٍ فَأُوْلَـئِكَ يَتُوبُ اللّهُ عَلَيْهِمْ وَكَانَ اللّهُ عَلِيماً حَكِيماً

Hakika toba inayokubaliwa na Allaah ni ya wale wafanyao uovu kwa ujinga, kisha wakatubia kwa haraka. Hao ndio Allaah Huwakubalia toba yao, na Allaah ni Mjuzi na ni Mwenye hikima  [An-Nisaa 17]

Ni vizuri kuharakisha kuomba Tawbah kwani kuna hatari katika kuchelewesha kama tunavyoona katika aya na Hadiyth zifuatazo:

 

وَلَيْسَتِ التَّوْبَةُ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ حَتَّى إِذَا حَضَرَ أَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ إِنِّي تُبْتُ الآنَ وَلاَ الَّذِينَ يَمُوتُونَ وَهُمْ كُفَّارٌ أُوْلَـئِكَ أَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا

Wala hawana toba wale wafanyao maovu mpaka yakamfikia mmoja wao mauti, kisha hapo akasema: Hakika mimi sasa nimetubia. Wala wale wanaokufa na hali wao ni makafiri. Hao tumewaandalia adhabu chungu  An-Nisaa 18]

 قال صلى الله عليه وسلم: ((إن الله يقبل توبة العبد ما لم يغرغر)) رواه أحمد والترمذي وصححه النووي

Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema:((Hakika Allaah  huikubali toba ya mja wake kabla ya roho kufika kwenye mkoromo wa mauti))  [Imesimuliwa na Ahmad na Kusahishwa na An-Nawawy]

         Na Kabla ya kuchomoza jua upande wa Magharibi

 

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وآله وسلم  قال: ((من تاب قبل أن تطلع الشمس من مغربها تاب الله عليه))  رواه مسلم

Kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم kasema: ))Atakayetubu kabla ya kuchomoza jua upande wa Magharibi, Allaah سبحانه وتعالى Atamkubalia toba yake))  [Muslim]

 

Na Allaah Anajua zaid

Share