Vipapatio Vya Kuku Kwa Sosi Ya Ukwaju
Vipapatio Vya Kuku Kwa Sosi Ya Ukwaju
Vipimo
Vipapatio vya Kuku - 1 kilo
Kitunguu saumu (thomu) iliyokunwa - 2 vijiko vya supu
Tangawizi mbichi iliyokunwa - 2 vijiko vya supu
Ndimu - 1
Chumvi - kiasi
Mafuta ya kukaangia - Kiasi
Namna Ya Kupika.
- Changanya vipatatio na tangawizi mbichi, kitunguu thomu, chumvi, ndimu. Roweka (marinate) kwa muda kiasi uwezacho.
- Tia mafuta katika karai, kaanga vipatatio hadi vigeuke rangi na kuwiva.
- Eupa weka katika chujio vichuje mafuta. Kisha weka katika karatasi inayonyonyoa mafuta izidi kuondosha mafuta.
- Tayarisha sosi ya Ukwaju
Vipimo Vya Sosi Ya Ukwaju:
Pilipili mbichi ziliosagwa -3
Bizari ya mchuzi - 2 vijiko vya supu
Bizari ya pilau/jiyra/cumin - 1 kijiko cha chai
Pilipili manga - 1 kijiko cha chai
Ukwaju Ulokamuliwa - 1 kikombe cha chai
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha:
- Katika kibakuli, tia viungo vyote, changanya vizuri.
- Mwagia katika vipatatio uchanganye vizuri.
- Weka katika treya ya oveni uvichome kidogo tu kiasi cha kubadilisha rangi ya vipatatio.