Kanuni Za 'Aqiydah
Kanuni Za 'Aqiydah
Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah
Imefasiriwa na: Abuu Sumayyah
Maandiko ya ziada katika mfumo wa ‘hati mlazo’ baada ya kila nukta, ni Mukhtasari wa maneno ya Ibn Taymiyyah aliyomo kwenye kitabu chake kiitwacho Majmuw’ Al-Fataawa.
1. Kila kitu kinachokubaliana na Kitabu (Qura-an) na Sunnah sahihi hukubalika kwao na kile ambacho kiko kinyume na hivyo havikubaliwi nao.
Kitu cha kwanza ambacho hutofautisha kati ya Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah na wengine wote ni Manhaj na mahali ambapo huchukua mafundisho ya Diyn yao kwenye vyanzo vyenye mashiko wanapopokea iymaan, ufahamu, ‘Ibaadah, kuamiliana na watu, njia na mwenendo wa tabia zao. Chanzo cha elimu na ukweli katika matawi yote ya elimu ya Diyn miongoni mwa Ahlul Sunnah Wal Jamaah ni Kitabu na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Hakuna kauli isipokuwa kauli ya Allaah inayotangulizwa na hakuna uongozi isipokuwa uongozi wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) unaotangulizwa.
2. Hakuna hata mmoja aliyesalimika kufanya makosa (kwenye Diyn) isipokuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
Ahlus-Sunnah huamini kwamba hakuna aliyekuwa salama kufanya makosa kwenye masuala ya Diyn isipokuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) peke yake, Maulamaa Hawajasalimika kufanya makosa isipokuwa kauli ya yoyote miongoni mwao hukubaliwa au hurudishwa ila ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) pekee. Hivyo basi kauli au taarifa za Maulamaa wa Ahlus-Sunnah kutokana na umuhimu wake huweza kufuatwa kwa mujibu wa Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) si kwa kuitangulia kauli hiyo au kuiweka nyuma.
3. Ijmaa’ ya Salafus-Swaalih (Swahaba) inazingatiwa kama uthibitisho wa kishari’ah wa kushikamana nao kwa wale waliokuja baada yao.
Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah wanaamini ya kwamba wale walioelimika sana miongoni mwa viumbe vya Allaah ukizingatia masuala ya Diyn baada Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) na wema waliotangulia baada ya wao (Salafus-Swaalih) iwapo watakubaliana kwenye jambo lolote lihusianalo na Diyn basi haliwezi kuwa ni la makosa na hairuhusiwi kwa yoyote yule kuliwacha kwani Ijmaa’ ni uthibitisho wa kishari’ah ambao ni lazima kushikamana nao kwa wale waliokuja baada yao na wote wanaoshikamana na Ijmaa’ ndio walioshikamana na Jamaa’ah.
4. Ahlus-Sunnah huwa hawapokei au kuthibitisha kauli au Ijtihaad isipokuwa kama ilipitia kwenye vyanzo vitatu: Kitabu (Qur-aan), Hadiyth sahihi na Ijmaa’ ya wema waliotangulia (Salafi).
Ahlus-Sunnah hushikamana na mwenendo (Sunnah) ambao amekuja nao Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kushikamana na Jamaa’ah ya Mtume na Maswahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na atakayefuata mwenendo wao na athari zao huwa hapokei Ijithaad au kauli hata kama imekuja kutoka kwa nani yule mpaka iwe imejulikana chanzo chake yaani Kitabu (Qur-aan), Hadiyth sahihi na Ijmaa’ ya wema waliotangulia (Salaf).
5. Sunnah huwa hawaendi kinyume na Qur-aan Na Sunnah kwa kutumia akili zao, rai na Qiyaas.
Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah huwa hawategemei kufuata au kushikamana ila kwa kufuata mashiko kama walivyofanya na yeyote atakayechukua kutoka kwao na kushikamana na Jamaa’ah, kufuata Manhaj yao kisha akashikamana na misingi/kanuni zao (huyo ndio atakuwa ameshika kishiko chenye uhakika) Kwani Maswahaba (Radhiya Allaahu anhum) walijifunza tafsiyr ya Qur-aan na Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kutoka kwake, kisha wakawafundisha (waliofuata baada yao; Taabi’iyn) lakini hawakujiweka mbele ya Allaah na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kutumia maoni, matamanio, na akili zao na mfano ya hayo.
6. Jamaa’ah (ni kundi lililoungana kwa misingi ya Haki, ambao Mtume [Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam] alikuja nao kwa kauli na matendo) ni njia ya kuokoka hapa Duniani na kesho Aakhirah.
Hivyo basi Ahlus-Sunnah ni wale wanaoshikamana na Jamaa’ah ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), wako mbali na maeneo ya kutengana na kutofautiana, wanashikamana na Kitabu na Sunnah na Ijmaa’ (makubaliano ya Maswahaba), wakionekana kuwa mbali na maeneo ya makundi mapotofu na wazushi ambao wanatenganisha na kugawa kutoka kwenye umoja na hili kwa sababu Jamaa’ah (kwa uoni wao) ndio kundi la uokozi katika maisha ya hapa duniani na kesho Aakhirah.
7. Huwa hawajifaradhishi kufungamana na mafunzo yatokayo kwa mtu asiye na Mashiko (dalili), wanatakiwa wachukue mafunzo kutoka kwa mtu mwenye mashiko (dalili).
Na Ahlus-Sunnah wanaamini kwa kile alichokuja nacho Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ukamilifu wake, hata hivyo, tofauti kati ya yule anaejua na asiejua huzingatiwa kwa kufahamu ya kwamba Mjumbe wa Allaah alilithibitisha na alilifanya. Na huu ni msingi mkubwa: mitihani mingi imeupelekea (Ummah) kugawanyika kwa kutokuwepo ufahamu huu.
Swalaah na salaam zimfikie Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watakaowafuata mwenendo wao mpaka siku ya Qiyaamah.